Wanawake ni nguzo kuu ya Usalama wa Nchi

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,961
2,000
Salamu,

Kwa muda mrefu nimechunguza nikagundua nchi ambazo ni strong sana kwenye mambo ya usalama, wanawake wao hauwezi kukuta wanafanya mambo ya hovyo hovyo. Nchi hizo zimefanya juhudi za makusudi kabisa kuwaendeleza kitaaluma.

Ukiangalia nchi kama za Scandinavia, Canada, Israeli na Ujerumani, wanatumia wanawake wao sana kwenye tafiti, management na usalama. Nadhani ni kutambua maeneo ambayo nature ya mwanamke ina nguvu (they have natural instinct, they are emotional beings and have unique ability to see things on a wider scale).

Bahati mbaya wanawake wetu wameachwa kuwa wa kuchota maji, kupika, kufanya biashara za uchuuzi, kulima na sasa hivi kucheza vigodoro. Juhudi za hapa na pale zinafanywa kuwaendeleza kibiashara mfano kuwasisitiza kujiunga na vikundi nk. Kwa maoni yangu, haya yote siyo maeneo ambayo kama taifa tunaweza kunufaika na uwezo wao ambao ni unique.

Juhudi za makusudi inabidi zichukuliwe kuwaokoa wanawake wetu. Naona juhudi kubwa zinawekwa kuwafanya wafanyabishara, lakini wanawake wangetumika zaidi kwenye nyanja za USHAURI na UTAFITI hasa kwenye maeneo ambayo yanagusa familia moja kwa moja mfano usalama, uzalishaji wa chakula, afya, huko ndiyo tungefaidika nao zaidi.

Kuna story nyingi katika maandiko zinazoelezea jinsi mwanamke anavyoweza kutumika na maadui. Wote mnajua story ya Samson. Kuna story ya wakati wa Musa, yule kahaba aliyewahifadhi wapelelezi wa Israel. Kwenye kitabu cha Waamuzi kuna story ya yule mwanamke alimuangushia jiwe na kumuua Abimeleki, mtu aliyekuwa na nguvu sana, na kwa aibu isijulikane ameuawa na mwanamke akamwambia mlinzi wake amchome na upanga. Kuna story ya wakati wa Daudi, yule mwanamke aliyeokoa mji wake uliokuwa unavamiwa na jeshi la Israeli akiwaambia jeshi la Israeli kuwa yule mtu wanayemtaka atawapatia ifikapo kesho yake (akiwaambia wabaki nje ya mji, kichwa cha huyo mtu watatupiwa juu ya ukuta). Hapo sijaongelea story ya Ester na nyingine nyingi tu.

Jiulize, mtu akitaka kufanya uovu hapa TZ, wanawake wetu wako kwenye hali gani kuwa na uzalendo? Ushauri wangu ni kuwa tuwatumie ipasavyo kwa usalama na ustawi wa taifa letu huku tukizingatia uwezo wao wa kiasili.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
48,045
2,000
Anguko kubwa la wanaume wenye nguvu hutokea kwa njia ya mwanamke. Nabii Suleiman alimfuata mkewe kuabudu sanamu, kitendo kilichomchukiza sana Mungu.

Ingawa sacandal ya Monica Lewinsky haikumtoa madarakani Bill Clinton lakini ilimlaza macho kwa siku kadhaa na ili leta mtafaruku mkubwa kwenye ndoa yake.
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
54,585
2,000
Anguko kubwa la wanaume wenye nguvu hutokea kwa njia ya mwanamke. Nabii Suleiman alimfuata mkewe kuabudu sanamu, kitendo kilichomchukiza sana Mungu.

Ingawa sacandal ya Monica Lewinsky haikumtoa madarakani Bill Clinton lakini ilimlaza macho kwa siku kadhaa na ili lets mtafaruku mkubwa kwenye ndoa yake.
Grace Mugabe Na anguko la Robert Mugabe
 
Hizo zote za Nabii Suleiman, Grace Mugabe, Monica Lewinsky zinathibitisha nilichokiongelea kuwa bila juhudi za makusudi, wanawake wanaweza kuwa TOOL ya anguko la utawala au hata nchi (na hii huwa inahitaji mwanamke MMOJA tu, angalia mifano yote kwa maana hiyo wanaweza kuwa very efficient). Lakini mifano hiyo hiyo niliyoiorodhesha inaonyesha jinsi unavyoweza kumtumia mwanamke kwa mafaniko makubwa. Inategemea tu uko upande upi wa hiyo mifano (victim or victor).

Hata Sauli alimpa Daudi binti yake amuoe akitegemea atamtumia kumuangamiza Daudi.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
48,045
2,000
Hizo zote za Nabii Suleiman, Grace Mugabe, Monica Lewinsky zinathibitisha nilichokiongelea kuwa bila juhudi za makusudi, wanawake wanaweza kuwa TOOL ya anguko la utawala au hata nchi. Lakini mifano hiyo hiyo niliyoiorodhesha inaonyesha jinsi unavyoweza kumtumia mwanamke kwa mafaniko makubwa. Inategemea tu uko upande upi wa hiyo mifano (victim or victor).

Hata Sauli alimpa Daudi binti yake amuoe akitegemea atamtumia kumuangamiza Daudi.
Wakati wa WW II, wanawake walikuwa wanatafsiri mathematical coding language ya adui. Wakati wa Cold War, hati mkato ( shorthand) ilitumika sana kwenye mawasiliano na makatibu muhtasi wengi walikuwa wanawake.
 
Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,961
2,000
Wakati wa WW II, wanawake walikuwa wanatafsiri mathematical coding language ya adui. Wakati wa Cold War, hati mkato ( shorthand) ilitumika sana kwenye mawasiliano na makatibu muhtasi wengi walikuwa wanawake.

Na inawezekana huyo adui alikuwa anawatumia wanawake pia kuziandika hizo codes.
 
Betterhalf

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
2,832
2,000
Anguko kubwa la wanaume wenye nguvu hutokea kwa njia ya mwanamke. Nabii Suleiman alimfuata mkewe kuabudu sanamu, kitendo kilichomchukiza sana Mungu.

Ingawa sacandal ya Monica Lewinsky haikumtoa madarakani Bill Clinton lakini ilimlaza macho kwa siku kadhaa na ili lets mtafaruku mkubwa kwenye ndoa yake.
Nimekupenda buuureeeee
 
Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,961
2,000
Tatizo wanaume wa sasa hamtutumii kiuchumi.
Mko na sisi kwa ajili ya kutuchuna tu, mnadhani hayo mawazo ya akina Delilah wa Samson tutayapata wapi!

Haha! Hili nalo ni neno. Ningependa kupata fundisho kwenye hili, si mara ya kwanza kusikia hii kitu.
 
ndayilagije

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
7,476
2,000
With any successful man there is a strong woman behind. Wanawake wanalea,wanashauri,wanatulza,wanaleta amani ya moyo,wanafundisha. Sema tu sumu ya mwanamke ni mwanamke!
 
Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,961
2,000
With any successful man there is a strong woman behind. Wanawake wanalea,wanashauri,wanatulza,wanaleta amani ya moyo,wanafundisha. Sema tu sumu ya mwanamke ni mwanamke!

Ni kweli kabisa. Wengine bado hatujabahatika kupata wa type hizo.
 
Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,961
2,000
Pole mkuu,ujue nini!wanawake wengi wanatembea na majeraha mioyoni mwao,hivyo hujikuta hawawezi au hawataki tena kurelease potentials zilizo ndani yao.Kosa kubwa la kijamii.

Ni kweli kabisa, ila ni kosa kwao pia kwa sababu baadhi ya tabia wanazozionyesha kabla ni big turn off kwa mwanaume ambaye alikuwa anakaribia kufanya maamuzi magumu. Uko sahihi sana, ni majeraha (yanayopelekea kufanya mambo bila kufikiria athari zake) na defense mechanism kujilinda wasiumizwe tena. Ila kuna swali la toka enzi, 'what do women really want'?
 
ndayilagije

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
7,476
2,000
I believe that they want what they deserve! Kuheshimiwa utu wao,kushirikishwa,kushauriwa/kushauri,kusikilizwa,kupendwa na kutambuliwa pia. Ukitaka kujua ubaya wao waonyeshe kuwa wao ni dhaifu,nadhani wako extra emotional to any kind psychological torment Vinginevyo wako piece tu.
 
Mmh, it's that simple? Naamini mwanamke ana power sana, na ndiyo ilikuwa maudhui ya post yangu ya kwanza. Bahati mbaya mwanamke mwenyewe au jamii inaposuppress au kuimissuse hiyo power, jamii nzima inaathirika.
 
Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,578
2,000
Keynez,

Mkuu,
Umeandika jambo zuri sana.

Ila tatizo wanaume nao hasa hawa vijana wa kuanzia 1990s ukiwaangalia na kuwatathimini unaona kabisa nchi inatishio kubwa sana la kukosa watu wa kutengeneza nguzo imara kwa wasichana na wanawake imara kwa ajili ya taifa eti kuwa imara.

Mfano, huto tuvijana twa umri huo twingi tunajua kugonoka na mambo ya 0713 kila sekunde.

Hebu angalia ile generation ya akina Mhe. Anna Tibaijuka (Prof), Mhe. Asha Rose .Migiro (Dr.) , Mhe. Ndalichako (Prof) hao waliandaliwa na pande zote mbili yaani wazazi na sisi wanaume tiliokuwa tumewazunguka katika maeneo mengi ya maisha ya kila siku.

Sasa leo hii, tuvijana 90% kazi zao ni kuongelea kugonoka kutwa nzima, miziki mpya, kwenda kula bata Dubai na USA kukaa na Jay Zee n.k.n.k.

Hapo ni lazima, tuuone wanawake wanahamasishwa kufanya pet manual jobs ili wawe dhaifu kisha tuvijana tuibe pesa ya serikali au shirika binafsi badae wawashike kirahisi wanawake maana hawana financial freedoms.

Any way, Tanzania tunahitaji reshuffle ya sekta za dini, familia, shule/ mitaala na vyombo vya serikali.

Naomba niishie hapa kwa sasa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom