Wanawake ndio wajibu hapa: ungefanyaje Kama unakutana na kisirani hiki…………?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Hebu fikiria kwamba, umepika chakula kizuri sana na unaamini mumeo mpenzi wako akirudi kutoka kazini na kula chakula hicho atafurahi, hata kama hatakwambia, ‘asante.' Lakini mume huyo anaporudi anajizungusha na hatimaye anasema kwamba, hatakula chakula. Unapomuuliza sababu anasema tu kwamba, ameshiba. Unapomuuliza amekula wapi, anaweza kujibu kiungwana kwa uongo kwamba, amekula chakula cha mchana saa mbaya, au alikuwa na ‘pati' ndogo pale kazini au chochote.

Mwingine hakujibu kiungwana kwa kiwango hicho, bali atafoka na kutoa kashfa. ‘unataka kujua nimekula wapi ili iweje?' anaweza pia kukuambia, ‘unafikiri ni wewe peke yako unayejua kupika?' Kuna majibu mengine, ambayo ni mabaya zaidi na yenye kukwaza zaidi ya hayo. Hebu niambie kama ni wewe unakumbana na kisirani hiki ungefanyaje?
 
mimi akinijibu hivyo hapo kwenye blue.....naigeuza hiyo hotpot miguu juu....halafu panakesha siku hiyo.....
khaaaa.....
 
sitamuuliza tena juu ya chakula hata hivyo atakuwa ana matatizo huyo ninaamini hata humo ndani amani haitakuwepo sio upande wa chakula tu hata mambo flani.
 
Mwanaume mwenye akili timamu hawezi kumjib mkewe wa ndoa hivyo hivyo lbd kama alilazimishwa kumuoa.Ningekuwa mimi kama ndo mara yake ya kwanza sitomjibu, nitamvumilia nione mwisho wake utakuwa upi?
 
mmh hujib nn tena me nitamuona kapotea 2 na hapa ni mtakuja so atakuja 2.
ila sitajishaua tena kujitia best wife(sitamuuliza yan) naweka mezan akila haya akikataa haya. 2takula kiporo wenyewe asubuh teh.
 
Kwa vile na mfahamu alivyo na sio kawaida yake kuwa vile au kunijibu vile mkewe,
Nitamshukuru na kumwandalia kitanda tulale,
Kwani najua lzm kutakuwa na tatizo kubwa sana linalohitaji kuongelewa muda mwingine na sio wakati ule,
Kesho yake nitamtafutia mda mzuri na kumtaka tuliongelee swala hilo na nipate maelezo ya kutosha.
 
Sitamjibu badala yake naenda chumbani kulala hata hamu ya kula itaniishia na mimi pia, si kwa kususa ila ila kama ni muungwana ataona nimejisikia vibaya kutokana na majibu yake, the next day nitamuuliza, asije kuwa amehamishia hasira ya alikotoka, which is very wrong
 
mimi akinijibu hivyo hapo kwenye blue.....naigeuza hiyo hotpot miguu juu....halafu panakesha siku hiyo.....
khaaaa.....
Usifanye hivyo my dia, vuta subira huenda kuna yaliyomsibu huko atokako ingawa si vema kufanya hivyo, kama si kawaida yake hata wewe utashangaa, so vuta subira
 
Kwa vile na mfahamu alivyo na sio kawaida yake kuwa vile au kunijibu vile mkewe,
Nitamshukuru na kumwandalia kitanda tulale,
Kwani najua lzm kutakuwa na tatizo kubwa sana linalohitaji kuongelewa muda mwingine na sio wakati ule,
Kesho yake nitamtafutia mda mzuri na kumtaka tuliongelee swala hilo na nipate maelezo ya kutosha.

you will be a perfect wife..
To be honest Nimependa ulichojibu
 
Thx AD,unajua kwa vile majibu haye yanatia hasira na yeye ana hasira nikilianzasha hapo inaweza tokea vita ya tatu ya dunia,
Cha kufanya nikulivumilia ili tulale then kesho akiwa fresh ndio ahangaike mwenyewe kujieleza mpaka nimuelewe!

kwa kweli ukifikiri njia uliyosema hapo juu is "Excellent way to approach the problem"
dahhhh lakini kuna wengine hapa tuna madadi sjui hata yanatoka wapi "short temper"
tunaangukia conclusion wakati bado hapo hatuja sort out problem ... vizuri kuona watu kama wewe..
 
Back
Top Bottom