TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,513
- 11,274
Jamani hii nimeikuta kwenye Blog ya Dina Marios wa Clouds Fm.
Mwisho wa kunukuu.
Chanzo Dina Marios Blog
Kwa mtazamo wangu nadhani ni vyema wanawake wakamfahamu mapema mwanaume kabla ya kukubali kufunga naye pingu za maisha manake tendo la ndoa ni haki ya kila mwanandoa ati!
Kuna dada mmoja ameolewa mwaka jana tena mke wa pili harusi ya kiislamu tumemchangia vizuri jamani kuanzia kitchen party,send off,harusi...sasa juzijuzi nikakutana nae nikawa namuuliza habari za maisha ya ndoa maana nikitambo hatujaonana,akaniambia alishaachana na yule mwanaume(mumewe),nikamuuliza kwanini ndio akaanza kunipa mchapo kama ifuatavyo.
Yeye katika maisha ya uchumba na bwana walikuwa hawajawahi kufanya tendo la ndoa,alikutana nae akawa anampa mahitaji yake muhimu lakini hakuwahi kumuomba tendo la ngono hata siku moja shost akashukuru mungu kwamba ni wanaume wachache utakutana nao katika maisha haya mkawa wapenzi na asikuombe naniliu..sasa baada ya mwaka kupita bwana akamwambia anataka kumuoa lakini mke wa pili.Mwanadashosti akaona si mbaya bahati ilioje akakubali kuolewa ndio na sisi tukashereheka....sasa wakiwa ndoani akawa anaona mbona bwana haniombi unyumba jamani!!!ikabidi yeye aanzishe michezo ili hatimae mchezo kamili uchezwe, baadae anakuja kugundua jamaa jogoo hawiki wala hasimami kujitutumua kuwika.
Akaendelea kuniambia kuwa alivumilia lakini kiukweli alishindwa akajikuta anaanzisha mahusiano na kijana mwingine akahakikisha yule mume anajua ili ampe talaka na kweli alijua na talaka akapewa ndoa ilidumu miezi 10 tu.Nikampa pole sana na tukaendelea na story zingine
Sasa nauliza tufanyeje?tukubali kuonja kwanza ili tujue kabisa mwanaume anaekuoa jogoo wake anawika na ngoma yake inakesha si ya kitoto au tuendelee na ule msemo wa kusubiri mpaka ndoa?
Mwisho wa kunukuu.
Chanzo Dina Marios Blog
Kwa mtazamo wangu nadhani ni vyema wanawake wakamfahamu mapema mwanaume kabla ya kukubali kufunga naye pingu za maisha manake tendo la ndoa ni haki ya kila mwanandoa ati!