Wanawake na suruali

mhalisi

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
1,181
320
Siku hizi umeingia utamaduni katika nchi yetu ambapo kina dada wengi wanapenda kuvaa suruali kuliko kuvaa sketi au magauni kama ilivyo utamaduni wetu. Ni kwasababu gani dada zetu siku hizi wameacha utamaduni wa kuvaa sketi na magauni badala yake wanavaa suruali?
 
Mabadiliko ya hali ya hewa (joto), usawa na wanaume, mishemishe (mfano dar (mbagala) kugombania daldala), kuonesha maumbile ili wanaume wavutike (kwa sababu sketi huwa haioneshi vizuri makalio, na siku hizi wanaume si wepesi kutongoza hivyo lazima kufanya vivutio) n.k
 
Siku hizi umeingia utamaduni katika nchi yetu ambapo kina dada wengi wanapenda kuvaa suruali kuliko kuvaa sketi au magauni kama ilivyo utamaduni wetu. Ni kwasababu gani dada zetu siku hizi wameacha utamaduni wa kuvaa sketi na magauni badala yake wanavaa suruali?

Utamaduni wa sisi waafrika ni kuvaa nguo za magome ya miti. First of all imekuaje tumetoka kwenye magome ya miti hadi kwenye nguo za pamba?
Sketi na magauni huvaliwa na wanawake wazee banaaa. Acha dada zetu wavae na wa-enjoy wanachotaka kuvaa.
 
Siku hizi umeingia utamaduni katika nchi yetu ambapo kina dada wengi wanapenda kuvaa suruali kuliko kuvaa sketi au magauni kama ilivyo utamaduni wetu. Ni kwasababu gani dada zetu siku hizi wameacha utamaduni wa kuvaa sketi na magauni badala yake wanavaa suruali?

Utamaduni wetu ni upi huo, na nani alikwambia suruali ni vazi la kiume? Mfano India, Pakistani na mpaka Uarabuni wanawake huvaa kama shati refu halafu na suruali (kwa kihindi inaitwa panjabi).

Halafu utamaduni wa tz kuanzia mwaka gani maana wazee wetu hapo zamani ilikuwa ni kaniki kuvaliwa kuanzia kifuani na kwenda mbele maana vitambaa vilikuwa ni shida sana enzi zile.

Acha tuvae bwana suruali ni safi sana utakimibia na kupanda milima bila ya hofu alimradi haikubani na kuonyesha maumbile yako.
 
Wengi wanaficha viguu vyao kama fito
Baadhi yao wana lengo la kuufahamisha umma kuwa wana matak.o makubwa.
 
sketi/magauni haswaa za kushonesha huvaliwa jumatatu, zile walizotoka nazo kanisani jumapili

jumanne na kuendelea mwendo mdundo suruali na vimini
 
Siku hizi umeingia utamaduni katika nchi yetu ambapo kina dada wengi wanapenda kuvaa suruali kuliko kuvaa sketi au magauni kama ilivyo utamaduni wetu. Ni kwasababu gani dada zetu siku hizi wameacha utamaduni wa kuvaa sketi na magauni badala yake wanavaa suruali?
<br />
<br />
Ka pepo ka ngono kanabeep hapo.
Kwa wale walio wakristo wanafahamu fika biblia inavyowakataka kutovaa mavazi yasiyo staha yanayowachora maumbile yao. Suruali ni vazi linalowachora kwa kuyafunua maumbile yao kwa kila mpita njia.
Hivyo kwa kufanya hivyo wameamua kumuasi Mungu wao peupe pee!!
.
 
Aaaaaaaaaah wapi bwana,siku hizi biashara waziwazi,wanawake hawawavai suruali bali socks tena siku zaja hawata vaa suruali tena bali watajichora mwili kwa mfano wa nguo kisha watatuambia utandawizi na maendeleo coz suruali si suruali ni jina tu na si kama tuzijuavyo.teteeni tu usawa coz najua mliwapenda walipoonesha maungo yao nje.Najua mnachukia bt 2fanyeje ukweli huu hampendi kuusikia?
 
Kwanza naomba nikueleweshe maana ya utamaduni.Utamaduni ni mfumo wa maisha ambao unajumuisha mawazo au matendo ambayo yanatokana na jamii husika.Kwa maelezo hayo, kwa vile uvaaji wa suruali hautokani na jamii yetu, sio utamaduni wetu.Infact nina wasiwasi kama ni utamaduni wa jamii yeyote duniani.Kwa nini ninasema hivyo,ninasema hivyo kwa sababu kwa jinsi maumbile ya mwanamke yalivyo(mwanamke ana makalio makubwa), si busara kuvaa suruali.Kwa sababu hiyo sidhani kama kuna jamii ambayo ingeruhusu wanawake wavae suruali kwa kuwa ingekuwa aibu kwa jamii husika.Upuuzi huu umeshamiri sana baada ya jamii nyingi kuharibika through what is called globalization.Ushenzi huu ambao infact ni mbinu ya kitapeli ya kuiba resources za developing countries na kufanikisha demonization or demon infestation of nations kwa kutumia mbinu mbali mbali ambazo ziko tayari in place, umesaidia sana kuharibu morals, ikiwa ni pamoja na kuvaa suruali.Demon infestation ambayo imefanywa makusudi,ndiyo inayofanya watu siku hizi wafanye mambo ya ajabu sana.The NWO inahusika moja kwa moja na jambo hili.
Siku hizi umeingia utamaduni katika nchi yetu ambapo kina dada wengi wanapenda kuvaa suruali kuliko kuvaa sketi au magauni kama ilivyo utamaduni wetu. Ni kwasababu gani dada zetu siku hizi wameacha utamaduni wa kuvaa sketi na magauni badala yake wanavaa suruali?
 
huo muda wa kuchunguza huyu kavaa suruali hajavaa gauni unaupata wapi? nani kasema magauni ni utamaduni wetu? muulize bibi yako, kama walivoiga kuvaa magauni ndivo hivo hivo wameiga kuvaa suruali.haina shida so long wanajisitiri,aisee yaonekana ww mkeo hatavaa suruali kama umeoa, acha mambo ya kizamani.
 
Siku hizi umeingia utamaduni katika nchi yetu ambapo kina dada wengi wanapenda kuvaa suruali kuliko kuvaa sketi au magauni kama ilivyo utamaduni wetu. Ni kwasababu gani dada zetu siku hizi wameacha utamaduni wa kuvaa sketi na magauni badala yake wanavaa suruali?
culture hubadilika kuendana na wakati. Hata hizo sketi na baadhi ya magauni zilikuwa sio asili yetu. Tukubaliane na mabadiliko ya maisha.
 
Back
Top Bottom