Wanawake na maswali magumu kwa wapenzi wao…! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake na maswali magumu kwa wapenzi wao…!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 13, 2012.

  1. Mtambuzi

    Mtambuzi Platinum Member

    #1
    Oct 13, 2012
    Joined: Oct 29, 2008
    Messages: 8,795
    Likes Received: 1,247
    Trophy Points: 280
    [​IMG]

    Wanawake ni watu wenye utambuzi wa hali ya juu sana kwenye swala zima la mapenzi. Unaweza kusema neno moja tu na kupitia neno hilo wakajua kwa usahihi kabisa kwamba wewe ni mtu wa aina gani. Kuna jambo moja ambalo huwa wanaume hawalijui. Ni kwamba pale unapomdanganya mwanamke wakati unapomtongoza na ukampata, si kwamba umempata kwa sababu ya uongo wako, bali ni kwa sababu mwanamke huyo amekupenda, vinginevyo wala usingempata.

    Hapa sizungumzii yale mapenzi ya kimaslahi, yaani mwanamke anampenda mwanaume kwa kuangalia rasilimali anazomiliki. Nazungumzia mapenzi ya dhati, mapenzi yanayounganisha mioyo ya wapendanao. Mapenzi ya watu wanaozungumza lugha moja, wanaokamilishana, wanaopendana bila masharti. Hayo ndio ninayoyazungumzia.

    Hivyo basi wanaume wanatakiwa wawe makini sana na kauli zao pale wanapokuwa na wenzi wao. Hapa nazungumzia wapenzi wapya wanaoanza kuwa na mitoko kwa ajili ya kufahamiana.Hapa chini nitataja baadhi ya maswali ya mitego wanayouliza wanawake kwa nia ya kujua aina ya mwanaume anayetoka naye:


    1.Unauonaje uhusiano wetu?
    Kama jibu lako la haraka haraka litakuwa ni kutarajia kufunga ndoa na kuzaa watoto nk…… Unaweza kumpoteza huyu mwandani wako, kwani kwake yeye atakuona kama unataka kumgeuza mashine ya kutotolea watoto na si vinginevyo. Jibu kama, "nina furaha sana kuwa nawe na sioni kama kuna jambo litakalotutengenisha kati yangu na wewe, huwa najisikia fahari kuwa karibu nawe na nina mararajio makubwa juu yako iwapo mambo yataenda vizuri…" kauli hii inapopenya katika masikio ya mwanamke inamfanya ajisikie fahari sana na ajione kama vile amelamba dume.


    2.Ninaonekanaje na nguo hizi nilizovaa?

    Mwanamke anapouliza swali la aina hii, anatarajia mwanaume atoe maoni yake si kwa vazi alilovaa kiujumla bali pia anataka kujua maoni ya mwanaume juu kitu fulani kuhusu vazi hilo. Wanawake wangependa kusikia kuhusu rangi ya vazi hilo kama limeendana na ngozi yake ya mwili au aina ya mtindo alioshona kama unamfanya awe na mwonekano gani kulingana na umbo lake.. Je vazi hilo limem-shape vyema nk. Kama ukipatia namna ya kumsifia kulingana na jinsi alivyopendeza lakini bila kutia chumvi utakuwa katika nafasi nzuri ya kudumisha uhusiano. Wanawake ni wajanja sana, iwapo utamsifia kwa kutia chumvi atakusitukia na kukuoana mzushi..

    3.Je hutojali iwapo nikikuomba unisaidie?

    Jibu kwa swali hilo ni "Sitojali." Na haraka sana unatoa msaada hata kama hujapenda kutoa msaada huo, wanawake wanapoomba msaada kwa wapenzi wao hawataraji jibu la hapana au vijisababu vya kutaka kuhalalisha kutotoa msaada. Kwa kawaida wanaume ni waungwana sana wanapoombwa msaada na si kwa mpenzi wake tu, bali mwanamke yeyote yule. Kwa kawaida mwanaume anakuwa mwepesi kutoa msaada, hata kama sio wa moja kwa moja, lakini hata mawazo yatakayosaidia kupatikana suluhu ya kile mwanamke alichotaka kusaidiwa. Mwanamke atashangaa sana kusikia jibu la hapana kutoka kwa mpenzi wake na jibu hilo litamfanya amuone mpenzi wake kama mtu asiyejali...


    4.Je unawaonaje marafiki zangu?
    Kuna msemo mmoja unasema, "unaweza kumjua mtu kutokana na marafiki zake waliomzunguka." Mwanamke anapouliza swali kama hilo hawatarajii jibu moja tu. Kwa mfano jibu kama, "ni wazuri," au "ni wachakaramu sana." Jibu hilo haliwezi kumridhisha mwanamke hata kidogo. Iwapo utawaponda marafiki zake hilo litakuwa ni kosa kubwa, kwani kama utawakosoa kama vile wana tabia zisizofaa, basi atahisi kuwa na yeye umemweka kwenye kundi la wanawake wenye tabia zisizofaa…. Kwa hiyo mwanamke anapokuuliza kama unawaonaje marafiki zake anatarajia ueleze kwa undani jinsi unavyowaona hao marafiki zake, kwa kufanya hivyo atajua kwamba unampenda na kumjali. Sifa za ziada kuhusu huyo mpenzi wako na mmoja wa marafiki zake zinaweza kumfanya mpenzi wako ajisikie vizuri. "Wewe na lara 1 mnavutia sana mkiwa pamoja, maana kila nikiwakuta mko pamoja mnakuwa ni watu wenye furaha wakati wote, huku mkitaniana na kluongea kwa bashasha. Inaonyesha ni kiasi gani mnapendana sana na mnaosaidiana kwa hali na mali…." Unaweza kutoa maoni ya aina hiyo.

    5.Vipi, mwishoni mwa juma hili utakuwa na shughuli gani?
    Iwe una shughuli au huna, wanawake huwa hawapendi kuwekwa roho juu, linapokuja swala la miadi. Iwapo utamwahidi kuwa mtakuwa na mtoko, basi hakikisha kweli mnatoka na kwa muda mliopanga. Utafanya kosa kubwa iwapo utamwahidi mpenzi wako kwamba mtatoka halafu usitokee….. swala la miadi huwa linapewa uzito mkubwa na wanawake. Iwapo mwanaume atakuwa na kauli kama, "nitaangalia," au "labda tutapanga kuwa na mtoko juma lijalo." Kauli za namna hii huwa wanawake hawazipend. Ni vyema mwanaume akawa na uhakika wa kile anachomwahidi mpenzi wake, kama hana uhakika na ratiba yake ni vyema asiahidi. Kama yuko bize yuko bize tu, ya nini kubahatisha. Wanawake wengi huwa hawapendi tabia ya kukurupushwa.

    6.Je mpenzi wako wa zamani alikuwaje?
    Hili ni swali la mtego kwa sababu kama utamzungumzia mpenzi wako wa zamani kwa namna ya kuonyesha kuwa unam-miss, basi mpenzi wako wa sasa atakuona kama vile bado unampenda mpenzi wako wa zamani, kama utamzungumzia kwa namna ya kuonyesha chuki kupita kiasi dhidi yake, mpenzi wako wa sasa pia atakuona kama vile bado unampenda mpenzi wako wa zamani na unajutia mkitendo cha kuachana naye. Jaribu kutoonyesha hisia za aina yoyote kuhusu huyo mpenzi wako. Zungumzia sifa za jumla za huyo mwenzi wako wa zamani, unaweza kusema kwa mfano "alikuwa ni mtu wa kujichanganya. Pia alikuwa ni mtu mwenye bidii sana tulipokuwa chuoni." Zungumzia sifa za kile alichokuwa anakimudu zaidi na si kutoa maoni……

    7.Je unadhani wazazi wako wananionaje?
    Mwanamke yeyote unapompeleka kwa wazazi wako, anakuwa na hisia kwamba yeye sio wa kwanza kupelekwa hapo nyumbani kwa wazazi wako. Yeye atachukulia kama hiyo ni moja ya mchakato wa kufanyiwa tathmini na wazazi wako, ikiwa ni mwendelezo wa wapenzi wako wa zamani uliokwishawapeleka hapo. Anajua kwamba wazazi wako watakuwa wanajaribu kumlinganisha na wapenzi wako wa zamani uliowahi kuwapeleka hapo. Hatopenda kusikia sifa za jumla kutoka kwa wazazi wako, kwa mfano sifa kama, "ni mzuri," au "anakufaa." Zitamfanya aone dhahiri kama wazazi wako hawakumchunguza vya kutosha na kuona sifa zake nyingine. Binafsi atadhani kwamba hakupewa uzito unaostahili kuwafunika wapenzi wako wa zamani uliowapeleka hapo kwa wazazi wako. Iwapo wazazi wako watazungumzia sifa za mpenzi wako za ndani kabisa, basi mweleze usimfiche. "mama yangu amekusifu sana anasema una utaalam mkubwa wa mapishi." Au "Baba yangu amevutiwa sana na uwezo wako wa kujua siasa, hususan wakati ule mlipokuwa mkijadili kuhusu mabadiliko ya katiba." Unaweza kumwambia……

    8.Je unawaza nini?
    Wakati mwanamke anapokuwa kimya, ni kwa sababu anawaza kuhusu jambo fulani muhimu. Inaweza kuwa ni namna gani anaweza kusuluhisha ugomvi wake na mmoja wa rafiki zake au ni namna gani anaweza kuendeleza kipaji chake. Iwapo utakuwa unawaza jambo fulani, kiasi cha kukufanya kuwa kimya kwa muda wakati mko pamoja, halafu akakuuliza swali kama hilo na wewe ukamjibu kwamba, unawaza namna ya kurekebisha bomba la maji la chooni lililovunjika. Jibu kama hili litamfanya mwanamke akuone kama vile umechoka kampani yake. Yaani pamoja na kuwa naye karibu lakini unawaza vitu vidogo kama hivyo! Hii kwake yeye atadhani kama hujali uwepo wake. Iwapo utajikuta uko kwenye mawazo mazito ukiwa na mpenzi wako, kisha akakuuliza swali kama hilo, unaweza kumjibu tu kwa kifupi, "Siwazi kitu mpenzi, nina furaha kuwa nawe karibu." Unaweza kumalizia kwa busu moja matata… hapo utakuwa umemaliza.

    9.Je ilikuwaje mpaka ukanipenda?
    Swali hili ni gumu sana tofauti na jinsi wanaume wengi wanavyodhani. Hakuna mwanaume anayeweza kumuelezea mwanamke sababu ya kumpenda kwa namna ambavyo yeye (Mwanamke) angependa kuelezewa…. Lakini ili uweze kuepuka mtego huo, unaweza kumjibu kwa kumwambia hivi… "Tangu nikufahamu umenifanya nijiamini, unanifanya nijihisi niko salama na umenifanya nijione napendwa…." Majibu ya aina hii, yatamvutia mwanamke yeyote…

    10.Je ulimpendea nini mpenzi wako wa zamani?
    Kama jibu lako litakuwa, "sijui." Mpenzi wako atakuwa hakuelewi, atadhani hata yeye hujui umempendea nini. Jaribu kumweleza yale ambayo yalikuvutia kwa mpenzi wako wa zamani lakini usitie chumvi, lakini ni nyema ukazungumzia zaidi sababu za kuachana kwenu, kwa mfano unaweza kumwambia kwamba, mpenzi wako alikuwa hapendi ujiendeleze kielimu au ulipopanda cheo hakufurahi akihisi utakuwa unatumia muda mwingi kazini wakati si kweli……… Jibu hilo litamfanya ajue msimamo wako linapokuja swala la kuendeleza kipaji chako….


    [​IMG]
    Kesho nawajia na mada hii: Mwanamke: Unaweza kuwa mtabiri jinsi mwenzi wako atakavyokuwa baada ya miaka kumi…
     
  2. promiseme

    promiseme JF-Expert Member

    #2
    Oct 13, 2012
    Joined: Mar 15, 2010
    Messages: 2,715
    Likes Received: 30
    Trophy Points: 135
    Mie unko bado nnae Yule Yule wazamani kaniganda Kama ruba na nnampenda sijui kanifanyaje.....
     
  3. Root

    Root JF-Expert Member

    #3
    Oct 13, 2012
    Joined: Jan 23, 2012
    Messages: 26,116
    Likes Received: 12,825
    Trophy Points: 280
    Darasa zuri sana aisee sema wengine ndio wale watu wasio na maneno mengi hata maswali huwa hayana majibu marefu ingawa si majibu mepesi kama ya viongozi wa tz

    Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
     
  4. gfsonwin

    gfsonwin JF-Expert Member

    #4
    Oct 13, 2012
    Joined: Apr 12, 2012
    Messages: 16,943
    Likes Received: 1,817
    Trophy Points: 280
    Mtambuzi kuna jambo nimejiuliza sana akilini mwangu toka jana usiku, nilikuwa nausoma uzi wa Kaunga, nikaenda nikapitia nyuzi za@darkcity, AshaDii, boss, Mwanajamii one SnowBall Eiyer na wengine kisha nikaona uzi mwingine wa Superman na nyuzi ambazo wewe umetoa na nyingine kibao tu nikajiuliza hivi kweli haya mafunzo kunawatu wanayapata in reality? je michango ya wenzetu huwa tunaifanyia kazi? je tunatoka hatua moja kwenda nyingine in terms of relationships? je kiukweli humu MMU tupo ili kudumisha mahusiano yetu?

    kiukweli kama shule humu MMU IPO tena hii ni zaid ya ile ya chuo ila sasa kazi kwa sisi tunaojifunza.
     
    Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
  5. snowhite

    snowhite JF-Expert Member

    #5
    Oct 13, 2012
    Joined: Aug 2, 2012
    Messages: 14,174
    Likes Received: 2,136
    Trophy Points: 280
    HAPA PA KUTOA MAJIBU MAREFU HAPA NDO UTAKAPOFANYA WENZIO WAKUVAMIE
    sipati picha mwanaume umemuuliza ''unaionaje nguo yangu" ye aanze kujibu ni ''ni nzuri imekukaa vizuri kwa kweli hata hapa nyuma fundi amepatia sana kuweka hiyo zipu upande huu,halafu na hii material ya kitamba nayo imekushape poa sana mke wangu''
    wengi huishia kusema ''umependeza'' labda akiongeza atasema 'umependeza sana''
    wanaume na majibu marefu mh!sijui laba nimeweka kiujumla sana hebu tujuzeni!
     
  6. Mtambuzi

    Mtambuzi Platinum Member

    #6
    Oct 13, 2012
    Joined: Oct 29, 2008
    Messages: 8,795
    Likes Received: 1,247
    Trophy Points: 280
    Ndio maana nawafundisha namna ya kujibu, au wajue ninyi mnatarajia majibu ya aina gani.......
     
  7. snowhite

    snowhite JF-Expert Member

    #7
    Oct 13, 2012
    Joined: Aug 2, 2012
    Messages: 14,174
    Likes Received: 2,136
    Trophy Points: 280
    asavali !manake mi si unajua napenda majibu marefu!siyo mambo ya ''its ok" au ''haina shida''
    AHSANTE MWAYA!kababy kameamkaje lakini?mamake ako poa?
     
  8. Mtambuzi

    Mtambuzi Platinum Member

    #8
    Oct 13, 2012
    Joined: Oct 29, 2008
    Messages: 8,795
    Likes Received: 1,247
    Trophy Points: 280
    Dada gfsonwin, kusema kweli hata mimi nilikuwa najiuliza maswali kama hayo, lakini hivi karibuni nimegundua kwamba watu huwa wanasoma sana thread mbalimbali zinazoelimisha juu ya mahusiano, huwa naona wadau humu JF wakitoa reference ya post fulani inapotokea mtu anaweka post akiuliza kitu...
    Ni mara nyingi huwa naona wadau wakishauri kwa kusema, "Tafuta uzi wa Kaunga, aliwahi kuzungumzia jambo hilo." hiyo inadhihirisha kwamba wadau wanafuatilia mada zinatowekwa hapa........
     
    Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
  9. Purple

    Purple JF-Expert Member

    #9
    Oct 13, 2012
    Joined: Feb 9, 2012
    Messages: 2,031
    Likes Received: 228
    Trophy Points: 160
    Afadhali umebaelezea baelewe!
     
  10. Mtambuzi

    Mtambuzi Platinum Member

    #10
    Oct 13, 2012
    Joined: Oct 29, 2008
    Messages: 8,795
    Likes Received: 1,247
    Trophy Points: 280
    ndugu yangu kababy shida, kanalia mbaya mida ya usiku... lakini si unajua sie wakongwe, tunakomaa nako tu mpaka ngoma droo, saa hizi kamelala..
    Ila huyu dogo aliyeletewa mdogo wake, jealousy ile mbaya, kanuna na hampendi mdogo wake.... watoto bana, imagine ana miaka mitano, lakini mweh....... kaaazi kweli kweli
     
  11. snowhite

    snowhite JF-Expert Member

    #11
    Oct 13, 2012
    Joined: Aug 2, 2012
    Messages: 14,174
    Likes Received: 2,136
    Trophy Points: 280
    yaah watto wanasumbua sana usiku,nafkiri ni sababu maziwa yanakuwa hayaanza kutoka vizuri!so anapata shida kuvuta hivyo hashibi.
    hyo kubwa lao tototundu mwambie awe mpole tu!ndo kashakua hivo!
     
  12. gfsonwin

    gfsonwin JF-Expert Member

    #12
    Oct 13, 2012
    Joined: Apr 12, 2012
    Messages: 16,943
    Likes Received: 1,817
    Trophy Points: 280
    yaani hadi utakoma tena usilogwe ukamuacha na mtoto mbona atamtohoa majicho? but angalia try not to replace his love aisee......... tena kwakua huyu mdogo hajui muda kala basi yeye apewe mapenzi na huku akielimishwa sana juu ya kumpenda mdogo wake na nini nafasi ya mdogo wake kwake na uhitaj wa mdogo wake. usimkaripie but muelimishe kiupole and this time wewe baba uwe nae karibu na muda mwingi mnunulie zawadi mbili kisha mpe mwambie moja yake na moja ya mdogo wake ila yeye ndo ampelekee mdogo wake siku nyingine muulize tumnunulie nini mtoto na wewe unataka nini.......ataelewa tu muda mfupi
     
  13. Mtambuzi

    Mtambuzi Platinum Member

    #13
    Oct 13, 2012
    Joined: Oct 29, 2008
    Messages: 8,795
    Likes Received: 1,247
    Trophy Points: 280
    Shule nzuri sana hii, yaani huwezi kuamini alilia baada ya kumona mdogo wake, na kusema tumtoe hapo ndani.....
     
  14. HorsePower

    HorsePower JF-Expert Member

    #14
    Oct 13, 2012
    Joined: Aug 22, 2008
    Messages: 3,617
    Likes Received: 37
    Trophy Points: 145
     
  15. Jodoki Kalimilo

    Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

    #15
    Oct 13, 2012
    Joined: Feb 12, 2012
    Messages: 8,611
    Likes Received: 2,040
    Trophy Points: 280
    Received
     
  16. UncleUber

    UncleUber JF-Expert Member

    #16
    Oct 13, 2012
    Joined: Apr 25, 2011
    Messages: 4,943
    Likes Received: 98
    Trophy Points: 145
    Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
  17. lara 1

    lara 1 JF-Expert Member

    #17
    Oct 13, 2012
    Joined: Jun 10, 2012
    Messages: 15,444
    Likes Received: 10,121
    Trophy Points: 280
    Hahahaaaaaaa! Mama Ngina KWISHA HABARI YAKE!!!! Yaani mwanaume mpeku peku weye!!!! Khaaaaa! Nimetafuta ulipokosea wala sijapaona!!! Namna hii ni DANGEROUS!!!! Ole wake yule MCHAGA AWE KAPITIA HII THREAD ALAFU AWE AMECREMISHA HAYO MAJIBU!!!!! Nitamtoa RACE, MARATHON NA RELAY KWA MPIGO!!!!!!! Nishayacrem hayo majibu, nikimuuliza cha kwanza nikaona anafuata itikadi zako analo!!! ILA SWALA MSAADA HUSUSANI KUTUSAIDIA KIPESA UNGEONGEZA MSISITIZO NA KU BOLD KABISAAAA! ILI WAELEWE ZAIDI!!! LOL!
     
  18. Mtambuzi

    Mtambuzi Platinum Member

    #18
    Oct 13, 2012
    Joined: Oct 29, 2008
    Messages: 8,795
    Likes Received: 1,247
    Trophy Points: 280
    lara 1 hapo kwenye bold ushaanza majungu.... Una maana gani?
    Unajua nitakuto............................................vugaaaaa

    [​IMG]
     
    Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
  19. BADILI TABIA

    BADILI TABIA JF-Expert Member

    #19
    Oct 13, 2012
    Joined: Jun 13, 2011
    Messages: 30,865
    Likes Received: 6,216
    Trophy Points: 280
    Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
  20. elba10

    elba10 Member

    #20
    Oct 13, 2012
    Joined: Sep 27, 2011
    Messages: 11
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    bhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaas
     
Loading...