Wanawake na hofu ya kusaidiwa na nyumba ndogo

Watu wenye mawazo kama yako huwa wanaingia kwenye ndoa kimtego mtego.
Pole sana kwani hakuna utakaloambiwa na mtua naefanya kazi za kufua ukaona ni jambo jema.
hivi na maana kazi ngumu/ ya kitumwa kuliko zote ni kufua na kupasi?
Mie mwenzio najiona kama heshima vile kufua nguo za mume wangu! Ila namuonea huruma na namuheshimu sana kwa kazi anazofanya. tukizipa majina majina mabaya kazi za mume wangu ni kama, mlinzi wetu, mtumwa wetu wa kazi ngumu hapa home, ndio dereva wetu, ndio huwa anaenda sokoni tena kwa ratiba yangu, anakula chakula anachokuta tumeamua kupika, ndio wa kupelekewa mashitaka, ndio ATM yetu nk nk
Lakini dada ushauri wa haraka
usiolewe na mtu ambaye huwezi kumuheshimu, yani ambaye unamdharau, utapata kichefuchefu maisha yote. Pia hakikisha nae anakuheshimu, la sivyo my dia ukimfulia anakuona mtumwa, na wewe kumfulia unaona ni utumwa.
All the best.

Ila kwa upendo wa KAWAIDA kabisa, kama hakuna dharura, ni mategemeo yake akute nguo safi, akute chakula, akute hali ya mapumziko nyumbani. Magemeo yangu nipate mahitaji yangu, kwa
 
all in all, kufanyiana kazi, au kusaidiana personal issues, hazina mahusiano kabisa na mtu kuamua kuwa na kidumu.
hayo ni maamuzi yanayotokana na ukosefu wa maarifa ya kupambana na challenges za utu uzima.
Watu wote wenye kutembea nje ni watu wenye weak personalities.
 
maisha ya siku hizi yanawaharibu sana wanawake katika maadili ya zamani ya kumuona mwanaume yupo juu yao na anahitaji kuheshimiwa na kumjali kama mtoto asiyekuwa. unakuta mwanamke anafanyakazi kama mwanaume au zaidi matokeo yake anarudi home late na kukuta mume amesharudi na kukosa huduma muhimu za mkewe, au la mke amerudi amechoka na mume akirudi hawezi kumuhudumia, mbaya zaidi wanawake siku hizi wanakuwa na kauli mbaya sana kwa waume zao kunapotokea kupishana maneno. wanaweke wa pembeni afanyi makosa hayo anakuwa makini kumjali na kumbembeleza mwanaume na kumfanya ajisikie mfalme. vitu vidogo sana vinamfanya mwanume amuone mwanamke anampenda na kumjali, asili ya muafrika ndio hiyo na ndio maana ndoa za wazazi wetu zamani zilidumu wakati wazungu wanaongoza kwa kuachana kwa sababu ya mfumo wao wa maisha ambao umeingia kwa madada zetu siku hizi
 
pamoja na mambo mengine yanayopelekea nyumba ndogo,ikiwemo tamaa zetu tu wanaume and alike,mitazamo kama hii kwa wadada ndio inapelekea ongezeko la nyumba ndogo.kwanini tu usiwe MWANAMKE?kujaribu kupingana na asili kama matokeo ya westernization na mazao ya makongamano kama lile la beijing,sterio-types tu za mtaani na kujaribu kuishi maisha ya kwenye tamthilia,hasa kwa dada zetu,yataendelea kuathiri sana ndoa na jamii zetu waafrika.yalianza huko kwa wazungu na sasa yanakuja kwa kasi kwenye jamii yetu!hebu tuwe waafrika kwa mambo yasiyotudhuru,tuna tamaduni na mila za kwetu jamani.elimu,kazi,kipato,historia ya familia,exposure etc. havikufanyi usiwe mwanamke au mwanaume!!

Well said my dear.

Pauline hivi ni nini maana ya mke mpendwa? tukiachana na lile tendo si ndio mambo kama hayo kumfulia, kumpikia n.k. Kama kweli mwanaume unampenda kutoka moyoni utajikuta unafanya hayo mambo bila hata kujiuliza labda siku moja moja ukichoka.

Hebu tuachane na ubeijing wadada Mume ili awe mume lazima awe na sauti ndani ya nyumba sio kwamba awe mnyanyasaji la hasha ila lazima aheshimiwe, kuna mambo afanye kwa kuamua mwenyewe kama hayo ya kufua, kupika n.k. Sio eti mtu unakaa na mume unaanza kabisa kumwambia "babu we siwezi kukufulia mie fua mwenyewe au pika mwenyewe", sasa huyo anakua mume tena au kitu gani ni bora nikae bila kuolewa kuliko kuolewa na mume ambae mimi ndio nina sauti haina haja sasa.

Raha ya mume ni yule akirudi nyumbani au akishinda nyumbani, nyumba nzima inatambua kwamba leo baba yupo sio kwa kumuogopa bali kuna heshima fulani lazima iwepo.
 
Maty, nadhani Pauline kama hajakusikia kwenye hili,
Mungu amuepushie mbali, na aendelee tu na ubeijing wake.........................
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom