Wanawake muwe wazi mnapotaka kutubwaga, sio kutuweka kama sub bila kujua nini cha kufanya, mnatutesa sana kisaikolojia, badilikeni na semeni ukweli

GONZZ EPACLEM

JF-Expert Member
Dec 3, 2016
312
239
Habari wana JF
Nimeamua kuupandisha sasa ujumbe wangu wa jana kama uzi rasimi ili kujaribu kusaka angalau kupata mamentor nguri kuliko wale akina espy na wenzake maana blahblah zao hazijanisaidia lolote lile.
Story iko kama ifuatavyo
Hapo miaka ya nyuma (2013) hivi niliwahi kumpenda manzi na ndio ilikuwa mara yanyangu ya kwanza kumpenda demu kwa dhati sio kwa papuchi ila ilikuwa ni kwa dhati kabisa tofauti MABAHARIA wanavyopenda maana kuna ka utofauti kati ya pendo la KIBAHARIA na la mtu aliyependa aweke ndani baadae, bahati mbaya mahusiano yalikuwa ya muda mrefu sana.
Ee bhana hawa viumbe wakati mwingime wanajua kucheza karata zao za maigizo dah! Nilihudumia nikijua nahudumia wife material bhna, ila kilichonikuta nina kijua mimi
Tokea 2015 nikaamua kuapa kama wewe hapo juu na nilifanikiwa pakubwa sana KUIKWAA LIKIZO NDEEFU ya kupenda toka 2015 hadi 2020 disemba 31 saa 6 usiku.
Kipindi hicho chote cha Likizo nilicheza kibaharia hatariiii + rough za kutosha tu kwa hawa viumbe, mwiko tu hamna kupenda, unapenda KiBAHARIA tu maisha yanaendelea bila MAJERUHI WALA MAUMIVU
emoji23.png

Asikwambie mtu bhana kupenda KIBAHARIA HAKUNA STRESS WALA NDUGU YAKE NA STRESS, safi mno.

Sasa 2021 imeingia bhana ohoooo!
hali ya miaka ya nyuma imenitokea sasa KUPENDA KUSIKO KAWAIDA kupenda OUT of KI-OCEAN yaani duh!
Nina mwezi mmoja na tulianza vizuri sana kwa january yote,
kimbembe kinachonitesa ni kuwa nimemuonesha upendo wangu wote kuanzia kwenye UNYAYO WA MGUU HADI KISOGONI kudadeeek, yaaan acha bhana kumpenda demu taabu sana,


Kila nikituma sms
mimi= mambo
yeye= p
mimi= kipenz wangu mbona huna furaha
yeye= niko normal
mimi= mbona mwanzo hukuwa hivi
yeye= sijui
mimi= aya bhana
yeye= p, baadae

Yaani akili yangu yote haifanyi kazi kabisa kwa sabab ya huyu mmanzi na nilikuwa na mpango wa KUMWEKA NDANI KABISA ila sasa naona LIKIZO INANIHUSU SINA UJANJA

Bandugu JF ina mamenta wazurii sana hebu nishaurini nimchinjie BAHARINI au niendeleee KUJILIZA LIZA kwa huyu mmanz!
binafsi niligeuka kuwa mentor wa wengi waliopatwa na majanga haya kipindi nikiwa LIKIZO maana NILIKOSA kazi ya KUFANYA LIKIZONI kwa party time tu lakini, sasa yamenikuta tena mimi mwenyewe na siwezi KUJIMENTOR mwenyewe maana sina taaluma ya umenta ijapo niliifanya ili kufariji wenzangu tu LIKIZONI
Sina raha, sipati chakula kwa utulivu, moyo una ruka ruka tu kama mahaarage yakiwa YANAKWEPA KUIVA KWA MAJI YA MOTO, imeathiri utendaji wa kazi zangu kabisa na nina fanya makosa mengi ninapo kuwa kazini, ila yote ni kwa sababu moyo umependa kupitiliza kwa huyu manzi,


Nawasihi jamani mamenta mnisaidie tu, kama ni kurudi UBAHARIANI NIMECHOKA na sipo tayari kurudi likizo hiyo tena, maana nimekuwa sasa 27+months sio haba, naomba mnipe ushauri NiFanyaje kwa hili

demu kabadilika kinoma na ukitaka kumpigia lazima uwe na roho ngumu maana jibu lake ni kuwa niko bize na mtoto wa ant labda nitafute baadae, ukimcheki hiyo baadae utasikia nataka nilale maana sijalala mchana kwa hiyo nataka kupmzika,

SEMA NINA UZOEFU NA UBAHARIA, dent akisema ivo si kweli utashangaa ukiiingia FB mesenger yupo online hata saa 7 usiku unamuona kabisa yupo online, au whatsaap unaona kabisa yupo online, wachaa wee moyo unavoruka ruka khaaaa,
Hii mambo iache tu inatesa sana,
karibuni sana kwa kunipa mawazo mbadala
 

Attachments

  • 1612670830821.gif
    1612670830821.gif
    42 bytes · Views: 2
  • IMG-20200919-WA0000.jpg
    IMG-20200919-WA0000.jpg
    29.6 KB · Views: 2
Kwani bado hujamla kimasikhara??kama bado mle kwanza dogo.nakama tayar ulipiga show gani mpaka alete izo mambo? La mwisho inavo onyesha nikama hajakupenda vile. Kete uliyo bakiwa nayo mtupie mahindi kuku 😂😂😂 I mean mpe hela
 
Pole sana, Hao viumbe mkuu we wache tu. Nishapitia sana kwenye hizo kesi na bado naendelea kukutana nazo
 
Wewe ulitegemea majibu gani ili ujue anakupenda? Inawezekana na yeye ameshapitiwa na mabaharia hadi amechoka. Itachukua muda kuanza kukuamini na kukuoenda kwa dhati.

Jipe muda
 
Subiri ukue kwanza..
Wanawake huwa hawajui nini wanataka
Wewe kama mwanaume ndo unatakiwa uwe kiongozi..umuongoze ajue mipango yako na plans zako kwake...

Sasa kama unaweza hata kuwekwa pending na hujui ...basi humfai..

Wanawake wanataka mtu wa kujua nini anataka hata kabla hajasema
 

sijui kwanini nimecheka
Ila mara ya mwisho kupata maumivu ya moyo hivyo nililia kama msibaaah jamani hayo maumivu hayana komando
Pole sana utavuka tu hapo japo inahitaji muda na ni bora uwe mkweli kama ulivyo jipe muda wa kuugulia maumivu,jichanganye na washkaji,jipe shughuli ya kukufanya busy mimi nilipiga sana mazoezi mpaka namaliza eda kitambi chote kushney
 
Back
Top Bottom