Wanawake mnavotunyanyapaa kimapenzi.....kwa nini? (Muziki)

Kaizer

Platinum Member
Sep 16, 2008
25,324
17,844
Jamani leo ngoja tujibrekishe kidoogo, lakini tuumizevichwa kimuziki

Nimegundua nyimbi kibao zinazoelezea jinsi wanawake wanavotunyanyasa/sumbua kwenye mapenzi

Tukichukulia kwamba wanamuziki wanaimba mara nyingi mambo ya kweli yaliyopo kwenye jamii, hii inaonyesha kuna ukweli flani

Naomba tujadili hili kwa kupitia muziki hasa wa kwetu hapa (kiswahili) tukionyesha jinsi wanaume tunavolalama kwa sababu ya hawa wapenzi wetu.

Karibuni!


Mi mi naanza kama hivi

1.Georgina (Marijani Rajab na safari trippers?/dar international

" Ooh georgina,
Siku uliyoondoka uliniacha nalia na machozi,
Umekwenda kuishi mbali nami, Georgina wa mama
Sipati usingizi nikikumbuka tulivyoishi nawe Georgina,
Ooh Georgina

Umeondoka Georgina umeniachia MASIKITIKO,

Lini utarudi uniondoe wasi wasi......
georgina....nakonda kwa mawazo...nitakuja kufa...habari gani uliko"..

2.Lau Nafasi...(Kilwa jazz)
,,,,....huyu analalama jinsi anavonyanysika kwa penzi la Rosa..

Napenda nipate lau nafasi, nipate kusema nawe kidogo..aah mama...rohoni naumia
Hakika la kufanya badoo sijaliona!
nimeona leo bora nikuite huendakumbe roho yako ikadunda...ikaja siku ukanipoza roho mama...rohoni naumia!

3. Rosa (Western Jazz) (huu uchawi , mpewe nini mridhike?:sad:)
"Mapenzi yetu yamekuwa ni hasara Rosa
mganga aliyekupa dawa ni adui yangpenzi ulilotaka si penzi mwenzangu, eeh
dawa aliyokupa ni sumu mwenzangu eeh
hivyo ndivyo ulivyotaka toa roho yangu
nini ulichokosa kutaka kuniua rosa,
nilikuwa ninakupa mshahara wangu wote
hiyo haikutosha mpaka wataka kuniua rosa


eeh Rosa eeh Rosa mama!"

4. Shemeji Shemeji (mnavotuzunguka!) LOL:thinking:
"mpenzi wangu utaniponzaX3 kwa mambo unayoyafanya
.....mpenzi wanichonganisha mimi na yule ni rafiki,
wewe watupambanisha eeh mpenzi utaniumiza.....
kule ulisema yule kaka kumbe mafuta ulinipaka...pembeni huwa heka heka na vitanda kuvunjika......


shemeji shemeji huku wazima taa!x3
...ushemeji wa urongo miye sitaki, huyo ni shemeji yako mwazimia nini taa ...shemeji shemeji huku mwazima taaa mama..!"

5. Neema (DDC Mlimani Park...hapa hata siongezi neno...)
"Usipate tabuu neema, uliyoyafanya sio mageni hapa duniani eeh
Ikiwa ni kupendana aa mama wapo walipoendana kama watoto mapacha ooh
ikiwa ni mapenzi bibi wapo walippendana kama kumbi umbi. wanapendana sana ahata wakati wa kuitembea utawaona bibimbele bwana nyuma lakini sio ajabu hata pachan hutokea wakati wakakosa kuelewana tena kwa viapo oo nema sembuse mimi na wewe!

tafadhali yako nimeipokea kwa mikono miwili tena bila ya kinyongo moyonimwangu Neema
hata shemeji zako kitimtim na ngunde niliwatuma waje wakupe salamu zangu bibi

Ingawa roho iliuma ulipopnielezea kwamba yule bwana uliyezaa naye yupo!
kwa hiyo nisije humbani kwako wala kazini nisikufwate hata kusalimiana na mimi hutaki japo twafahamiana eeh!

chorus:

"Penzi maua.....penziupepo...sina neno mimi kwa kuwa najua hy nimmzazi mwenzio
Ipo siku nitakuja kwa wazazi wako nilete barua ya uchumba miyee nifunge ndoa na wewe"..


Kwa sasa ni hizo wadau ningeomba wengine hasa wa wenzi hizo tuongezee nyingine zenye ujumbe kama huo...kwamba jamani dada zetu wakati mwingine mnatunyanyapaa sana kwenye hii tasnia ya mapenzi
Mf..Edita wa DDC pia...

hapa najua kuna manguli wa hizi Oldies (wapi Balantanda) so tutakuwa na mjadala mzuri tu wa jisni wanamuziki walikuwa wanafikisha ujumbe wa kunyanyapaliwa kimapenzi kupitia tungo zao

(samahani bongo fleva siko deep kivile LOL si nasikia kuna mbagala....)

Karibuni!:israel::israel::israel:
 
Hommie aisee GEORGINA banaa we acha tu ingawa nilikuwa sijazaliwa wakati huo nina u-feel sana huu wimbo
 
mmmh jamani hata wewe swty?lol mbn nyie mmetunyanyasa sana tu jamani?umesikiliza siwema?mbn unanipa mateso ya moyoooooooooooooooooo?
 
apana.
enzi izo waimbaji wengi walikuwa ni wanaume so kila watakachoimba wataimba towards wanawake na ii haina maana kwamba wanawake ndo wana makorokocho
--kiukweli wanaume pia walikuwa na matatizo sema wanawake hawakupata chans ya kuimba saaaaaana km wanaume walivyofanya
--chek nyimbo za sasa wanaume wanavyoimbwa....mchek jide,na waimbaji wengne wa kike....rate inawazidia wanawake JUST BCOZ WAIMBAJI WA KIKE STILL NI WACHACHE..
----we jana uliniambiaje????na leo unafanyaje?
--twende kwa simu nkakuchambe kdg..
 
macho yanachekaaaaaaaaaaa,moyo unaliaaaaaaaaaaa macho yanacheka mie moyo unali-by shakila, Nyiwa peleka salamuuuuuu kwa yule wangu muhimuuuuuuuuuuuuuuuuuuu,umuelezeee hafahamm kwamba nnapata tabuuuuuuuuuuuu
 
3. Rosa (Western Jazz) (huu uchawi , mpewe nini mridhike?:sad:)
[/COLOR][/SIZE][/FONT][/B]"Mapenzi yetu yamekuwa ni hasara Rosa
mganga aliyekupa dawa ni adui yangpenzi ulilotaka si penzi mwenzangu, eeh
dawa aliyokupa ni sumu mwenzangu eeh
hivyo ndivyo ulivyotaka toa roho yangu
nini ulichokosa kutaka kuniua rosa,
nilikuwa ninakupa mshahara wangu wote
hiyo haikutosha mpaka wataka kuniua rosa


eeh Rosa eeh Rosa mama!"
[/COLOR][/FONT]Karibuni!:israel::israel::israel:
[/B]

Thank Mheshimiwa Kaizer haka ka wimbo katamu umenifanya niweke zilipendwa sasa nianze kupata kitu roho inapenda ..
Kesho sikukuu eti Asprini anafurahia
 
Tatizo kwa nchi yetu waimbaji wengi ni wanaume, kwa hiyo wanawakilisha mitazamo yao tu. Mfumedume in action
 
Jela ya Mapenzi! Haya sasa

"Ingekuwa wenye kugombania mapenzi wana jela ya peke yao mwenzangu,
labda hiyo ningheweza kugoimbania mapenzi
Lakini jela ya namna hiyo hapa duniani bado haijatokea
na mimi ndio siwezi kugombenia mapenzi!

Ikiwa, nitagombania mapenzi nikipelekwa kwa hakimu nikishindwa
ikiwa sina faini nikapelekwa gerezani
mateso ndio yatazini na wewe nitakukosa
Faida gani nitapata?


Kwa hiyo mwenzangu tangu leo ufahamu mimi mwenzio siwezi kugombania mapenzi!"
 
Clara ya marquees:

Clara ooh mamaa sikujua kama utanikataa eeeh, clara ooh mamaaaa...

Wazuri ni wengi nimekuchagua wewee
Miaka mingi tumeishi mimi na wee...
Nimevumilia yote ooh mamaa...
Clara eeeh nimekukosea nini maama

Clara ooh mamaa sikujua kama uanikataa eeeh
Clara ooh mamaaaaa :smile:
 
Mie nitazungumzia suala zima la mziki wa taarab (note: sio modern taarab wala Tarabu)

kwenye nyimbo hizi haijalishi kama imeimbwa na mwanamme au mwanamke, ujumbe unachukuliwa kumhusu yoyote anaehusika nao na labda ndio maana kwenye tasnia ya muziki huo hakuna kutaja jina la mhusika.

kwa wanaojua taarab utasikia nyimbo kama

"
na kamba umeikaza, pumzi zimenipaa
macho yanaona kiza, na sasa nishapumbaa
nimebaki kujikaza, nagonja dakika na saa

umenionjesha raha ya mtu anaependa, na mara ukanirusha na kunifanyia inda
nakuomba sawazisha, mwenzio mimi nateseka, mwenzio mimi naumia"

na hapo yeyote yule mwanamke au mwanamme anaenda kutunza akimaanisha kuwa ujumbe wako umenigusa na mi niko katika hali kama yako
 
Tatizo kwa nchi yetu waimbaji wengi ni wanaume, kwa hiyo wanawakilisha mitazamo yao tu. Mfumedume in action

Well..Gaijin, naweza kukubaliana na fact kwamba waimbaji wa kike walikuwa wachache, lakini pia waliwakilishwa na waimbaji wa kiume wakiuvaa uhusika wa kike

Mfani wimbo wa "makumbele" wa Ochestra Marquis Original, unawakilisha vyema dhana hii

Hillo la mfumo dume..silikubali 'hata kidogo;:nono::nono:
 
V.I.P Jery Nashon Dudumizi& Vijana Jazz

"Ahera hakuendeki,Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikooo,ahera hakuendeki Dunia haikaliki nimepatwa na mfadhaikoooo"

"Si maji wala Soda vitakavyozima kiu yangu,ila ni wewe Viaipiii(VIP),si maji wala Soda vitakavyozima kiu yanguuu,iila ni weweeeee,viaipiiii
"Ukinikubali viaipii,mimi niko tayari,kubadili dini,ukinikubaliii viaipii mimi niko tayariiii,kubadili dini,hata kama wazazi wangu hawapendi,nitafanyafanya mipando niwe na wewe smbamba(sambamba) nitafanyafanya mipango niwe nawee sambambaaa"
 
apana.
enzi izo waimbaji wengi walikuwa ni wanaume so kila watakachoimba wataimba towards wanawake na ii haina maana kwamba wanawake ndo wana makorokocho
--kiukweli wanaume pia walikuwa na matatizo sema wanawake hawakupata chans ya kuimba saaaaaana km wanaume walivyofanya
--chek nyimbo za sasa wanaume wanavyoimbwa....mchek jide,na waimbaji wengne wa kike....rate inawazidia wanawake JUST BCOZ WAIMBAJI WA KIKE STILL NI WACHACHE..
----we jana uliniambiaje????na leo unafanyaje?
--twende kwa simu nkakuchambe kdg..

mmmh haya bana :typing::A S 13:
 
Salama by Jabali la Muziki

Wapi salama, salama nakuomba
salama nakwita mamaa
umenipa machozi, machozi yasiyokwisha
nifanyeje mwana mamaa

nikilala naota sura yakoo
nikitembea nasikia waniitaa
nageuka sikuoni mwana mamaa
nauliza uko wapi mwana mamaa
 
apana.
enzi izo waimbaji wengi walikuwa ni wanaume so kila watakachoimba wataimba towards wanawake na ii haina maana kwamba wanawake ndo wana makorokocho
--kiukweli wanaume pia walikuwa na matatizo sema wanawake hawakupata chans ya kuimba saaaaaana km wanaume walivyofanya
--chek nyimbo za sasa wanaume wanavyoimbwa....mchek jide,na waimbaji wengne wa kike....rate inawazidia wanawake JUST BCOZ WAIMBAJI WA KIKE STILL NI WACHACHE..
----we jana uliniambiaje????na leo unafanyaje?
--twende kwa simu nkakuchambe kdg..

Subiri "kukuche" manake bado usiku hapa....:tape::tape:
 
Kaizer nadhani mie na wewe tunalingana umri mika yetu ileeeeeeeeeeeee ya 1950 na 60
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom