Wanawake mkiamua, wanaume wote kwisha habari yetu!!!!!!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
Ndiyo, si mliamua tu kulea mimba zetu-mngeamua kuzitoa nani angewazuia.

Eeeeeeee! Hata tukiwaudhi mnatupikia chakula na kukitenga mezani, tukirudi home tunakula, mkiamua kuweka sumu si wote tutakwisha.

Isitoshe hata, mkisalitiwa bado mnaendelea kutoa 'huduma' baada ya kutusamehe kwa dhati-kama mngeamua kulipa kisasi si wanaume wengi tungekuwa tuna lea watoto wasio wetu.

Umeona eeee! Mnakaa na wanaume wengi na kuwatunzia siri zao za ujambazi na maovu mengine ya duniani-unadhani mwanaume gani angetamba kama nyinyi mkiamua kutoa hizo siri!

Bisha sasa! Kwamba kina mwanaume aliyefanikiwa maishani kwa kiasi kikubwa basi ni nyie wanawake ndiyo mmechangia hayo maendeleo yao.

Ushagundua? Kwamba mwanaume hata awe na mali vipi kwamba kama hajaoa hapati heshima sawa na mwanaume aliyeoa ikimaanisha kwamba mwanamke ndiye anakamilisha heshima ya mwanaume.

Aiseee! Kumbe wa norway waliwatumia wanawake kuwalaghai wanaume wa kikoloni kufanya nao mapenzi then wakawa wanawawekea sumu mpaka wakamaliza kizazi cha wanaume wabaya wa kikoloni, na ndiyo maana ukimpiga mwanamke kama ni mgeni serikali inakukatia tiketi ya ndege na kuku deport immediately-serikali inawaheshimu sana ladies.

Kumbeeee! Mwanaume ukitaka alianzishe against you hata kama ni kimbaumbau we mtukanie mamake, ndo utamjua yeye ni nani-kwamba binadamu wote tunawapenda sana mama zetu zaidi kuliko madingi

Duuuuuuuuuuuu! Aisee mbele ya mwanamke yaani mwanaume hata awe jasiri vipi anaweza kutoa siri zake zote-Kumbukia stori ya Samson na Delilah.

Mazeeeeeee! Kuna mijanaume imeshawahi kuahirisha safari kisa eti ni kwa sababu ya demu tu-big up sana wanawake!

Jamani mengine ongezeeni, hayo ni yangu machache kwa leo!
 
u tell me loh!

Uzi kama huu mlitakiwa muushadadie japo kwa kusema "Hallo hallooo............" lakini mko kimya matokeo yake mnawaacha baadhi ya wanaume wanauvunja vunja, na kumfanya Ndyoko aonekane kama vile anawa-tweza.
 
Hebu fafanua hapa, vinginevyo Nitake radhi, maana baada ya kusoma hapa nimeanza kuhisi kizunguzungu!

Wewe pata tu kizunguzungu, wala huntishi, kwani ni mara ngapi nimeona nyuzi zako zimekaa kimazoea!? leo umeacha kufikiri kimazoea na umetoka nje ya box na ndio maana umeweka huu uzi uliosheheni hekima........... lol
 
Na ni MAUA kama WARIDI uyaonapo uhai ukujia tena. Bila sisi wanawake wanaume mngeuana ovyo, maana ni kwa kupitia sauti zetu za upole na mioyo yetu ya huruma AMANI inakuwepo duniani. Ni kwasababu ya wanawake , wanaume wanaitafuta hiyo pesa. Nguvu aliyonayo mwanamke ni kubwa kuliko MISULI ya mwanaume imejifumbata huioni kwa macho.Japo wanatuita viumbe dhaifu lakini wanakili moyoni POWER kubwa tuliyo pewa.Nashukuru Mungu kwa kuzaliwa nilivyo
 
Kwani nani amekuambia kulea familia ni hisani?Hilo ni jukumu lake,hata kumhudumia mumewe sio hisani ile ni majukumu yake,huo ndio ukweli wa mambo!
 
Wewe pata tu kizunguzungu, wala huntishi, kwani ni mara ngapi nimeona nyuzi zako zimekaa kimazoea!? leo umeacha kufikiri kimazoea na umetoka nje ya box na ndio maana umeweka huu uzi uliosheheni hekima........... lol

I salute you bro.........raha ya 'utoto' ni kwamba yuo are always surrounded by adults from whom you learn alot!...........
 
Back
Top Bottom