Wanawake Misungwi Mwanza wawajengea waume zao nyumba bora

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Wanawake Misungwi Mwanza wawajengea waume zao nyumba bora

HIKI ni kitu ambacho hakijawahi kutokea hapa nchi baada ya wanawake kujiunga katika vikundi vidogo vya maendeleo na kuanza kuwajengea waume zao nyumba bora, ikilinganishwa na maeneo mengine ya Tanzania tulivyozoea kuona wanaume ndio wanaojenga nyumba.

Wanawake katika kata nne za Koromije, Mondo, Isenegeja na Mwaniko wilayani Misungwi mkoani Mwanza waliojiunga kwenye vikundi vidogo vya maendeleo wamefanikiwa kujenga nyumba bora na za kisasa zipatazo 45.

Vikundi hivyo, viliamua kuanza kutumia mavuno yao vizuri kwa kuanza kujenga nyumba hizo za kisasa ikilinganishwa na zamani ambako walikuwa wakitumia vibaya mavuno hayo.

Nyumba hizo zimejengwa baada ya kufanyika tathimini ya kwanza iliyohusisha shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za wanawake na watoto la Kivulini kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya ya Misungwi.

Baada ya kufanyika kwa tathimini hiyo ilibaini changamoto moja wapo kwenye wilaya hiyo, kuna mahusiano ya karibu kati ya ukatili wa watoto na matumizi mabaya ya rasilimali fedha zinazotokana na mavuno.

Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini mkoani Mwanza, akizungumza jana katika mkutano uliohusisha watendaji wa ngazi mbalimbali wilayani Misungwi ya kutekeleza kampeni ya kuhamisisha wananchi kujenga makazi bora, alisema vikundi hivyo vya akina mama wamekuja na mfumo na utaratibu wao wa kusaidiana vifaa vya ujenzi ambako walifanikiwa kujenga nyumba hizo.

"Kilichotufurahisha katika kampeni yetu ya kwanza ni kwamba vikundi hivi vilikuja kwa jitihada zao wenyewe, vimekuja na dhana ya kisukuma ya "wapo nyamaswa" maana yake ni tupa nyasi weka bati.

"Sasa hivi baada ya wizara kufanya tathimini wameona mbinu inayotumika ya wapo nyamaswa inaweza kutumika nchi nzima kuhamasisha ujenzi wa nyumba bora, husasani ni wao kwa wao ikiwa haihusishi pesa wao wenyewe mfumo wa kupeana vifaa na mbinu ya kujenga nyumba.

"Leo tumekutana hapa (Misungwi) kuifanya kampeni ya kiwilaya iweze kufikia kata zote kata 27, vijiji 114 na vitongoji 724 na kata hizo ambazo zimeanza kuna nyumba nzuri na za kisasa," alisema Yassin.

Yassin alitoa wito kwa mamlaka nyingine za mipango nyingine kuja kajifunza Misungwi namna gani ya kupanga na kuboresha makazi kwa kutumia mbinu za ujuzi wa wajasiliamali na Kivulini tupo tayari kushirikiana katika kuendesha kampeni hii hata ngazi ya kitaifa ili iweze kunufaisha watu wengi zaidi.

Katika hatua nyingine, Yassin alisema moja ya changamoto moja yapo inayochangia wanafunzi wengi kushindwa kujisomea na kufanya vizuri darasani ni kutokana watoto wengi wanatoka kwenye makazi duni.

Mwisho
 
Attachments

  • IMG_20200226_142158.jpg
    IMG_20200226_142158.jpg
    29.9 KB · Views: 1
  • IMG_20200226_142230.jpg
    IMG_20200226_142230.jpg
    27.6 KB · Views: 1
  • IMG_20200226_142310.jpg
    IMG_20200226_142310.jpg
    27.1 KB · Views: 1

Mbona hujapiga picha hizo nyumba au unaogopa kesi ya uhujumu uchumi
 
Back
Top Bottom