Wanawake: Mambo yanayopelekea mwanaume apoteze kujiamini, na kuamua kuvunja mahusiano

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,418
98,990
Kwenye mahusiano,Kuna wanawake wengi ambao wanaumia kwakua wanaume wao wamepoteza kujiamini.

Mwanaume anapopoteza kujiamini mara nyingi anakua na Gubu, anakasirika vitu vidogo vidogo, anakua na wivu sana kwani hujiona kama vile hatoshi hivyo kuogopa kusalitiwa au kuachwa. Hii humuumiza mwanaume ndani kwa ndani.

Kwa bahati mbaya nikuwa. Pia kuna wanawake wananyanyasika, kutukanywa na kuteswa na hawajui sababu, pia kuna wanaume wana hasira na visirani ila hawajui sababu, endelea kujua sababu.

(1) Mwanamke kusifia sifia mwanaume mwingine unapokua na mwanaume wako;

Anaweza kuwa ni Bosi wako, Kaka yako, rafiki yako, msanii kwenye TV au X wako, unapomsifia mwanaume mwingine ni kama unamkosoa mwanaume wako kuwa yeye hayuko vizuri.

Mwanamke ukimsifia mwanaume mwingine, labda ni mzuri, anafanya kazi vizuri na chochote kile hicho kitu hakitoki kwenye vichwa vya wanaume wengi. Anakua anawaza kila saa na mara nyingi huhisi kama uko naye kwakua tu huna mtu mwingine na humpendi.

Hivyo Dada kuwa makini, hata kama ni Baba yako, kwa mfano ukasema napenda jinsi Baba yangu anavyohangaika kutafuta pesa. Hivyo ni kama unamuambia mume wako, wewe ni mvivu kwanini usitafute pesa kama baba yangu, ni kama unamuambia ningepata mwanaume kama Baba yangu ningekuacha hivyo kuwa makini katika kusifia.

(2) Kumsimanga mwenzio au kuonyesha kutoridhishwa pale anaposhindwa kufanya vizuri tendo la ndoa;

Hakuna kitu kinawafanya wanaume wengi kupoteza kujiamini kama hiki.

Kwenye akili za wanaume wanaamini unatakiwa kwenda angalau mabao matatu kwa tendo na kuchukua angalau nusu saa kitandani kwa kila bao,

hii nadharia mara nyingi si kweli, maana wanawake wengi huridhika kitandani kuanzia dakika ya 7 mpaka 15.

Lakini mwanaume ambaye anajiona hamridhishi mke au anahisi ana maumbile madogo au hajui kusex vizuri.

Hii husababisha wengi kupoteza kujiamini na kila dakika wanahisi kusalitiwa.

Utajikuta keshaanza kujiingiza Kwenye kundi la wanywa al-kasusu, vumbi la Congo, Viagra, ugolo+Colgate, panado na coka, mchuzi wa pweza, waganga na madawa mengineyo ya Nguvu za kiume n.k

Hivyo mwanamke
Kama una mwanaume wa namna hii, kwanza penda kumsifia, usioneshe kujali sana kuhusu kuridhika na wakati mwingine furahia romance tu,

Acha kumuuliza uliza mara kwa mara kwanini hawezi kukufikisha kileleni,

Kiukweli kuniuliza uliza maswali Kama hayo Mara kwa Mara, haisaidii kitu. Zaidi zaidi inaharibu zaidi.

Cha kufanya mjenge vizur kisaikolojia, na Kama Kuna kitu unakijua kinaweza kumsaidia akuridhishe. Mfanyie kimya kimya.

Akija kustuka, performance imeongezeka na ukiona ameridhika na kufurahia Basi muweke wazi ulichomfanyia ili ajiskie amependwa na kujaliwa.

(3) Kama alishawahi kupenda Sana na kusalitiwa huko nyuma;

Wanaume ambao walishawahi kupenda sana huko nyuma na kusalitiwa wengi huingiwa na Hali ya kupoteza kujiamini. Wanaona kama walikosea sehemu ndiyo maana wakaachwa, wanaona kama hawajitoshelezi hivyo huwa na wivu, hasira na Gubu.

Ukimkosea kidogo hachelewi kukulinganisha na ex wake.
"Wanawake Wote ndo mlivyo"

Anakulinganisha na X walioachana, hii INAUMIZA sana maana anakua kama anakujumuisha na kukuadhibu kwa makosa ya X wake.

Kwa mwanaume hii si sawa, ukishaachana na mtu kubali kuwa ni kawaida na si kwakua una mapungufu hasa katika uwezo wako wa tendo la ndoa. Kwa mwanamke ongea naye taratibu, kama unaona kabisa anakuhukumu kwa makosa ya X wake muambie na mueleze kwa upole kuwa wewe si X wake hivyo anapaswa kuacha kukuhukumu kwa makosa yake.

(4) Kujipandisha mabega ikiwa umemzidi kipato mwanaume wako;

Hili nalo ni tatizo, Kisaikolojia wanaume wengi wanaamini kuwa wanapaswa kuwa juu katika kila kitu kinachohusu Maisha na mahusiano.

Ila kiukwei, ni Hapana,
si kila kitu, wakati mwingine hata huko kitandani wanawake hukaa juu,

ila ukweli nikuwa wanaume wengi unapoanza kupandisha mabega hupoteza kujiamini na wanahisi kudharauliwa kwa sababu ya umeonyesha jeuri ya kipato chako.

Kwa mwanaume
Unapaswa kujua kua nafasi yako kama mwanaume kamwe haiwezi kuchukuliwa kwa pesa, kama ukijiamini, ukatekeleza majukumu yako kulingana na uwezo wako basi huna haja ya kuhofia.

Kwa mwanamke,
Punguza amri, kufoka foka, mheshimu, nyenyekea lakini usijidhalilishe na jifunze namna ya kuongea kwa hekima na mwanaume wako Kama mwanamke.

(5) Mwanamke kufanya na mawasiliano mara kwa mara na X wake;

Aisee Ni ngumu sana mwanaume kuvumilia hili, anaweza kukuambia anakuamini na hajali ila moyoni mwake anajali.
Wanaume wanajilinganisha, na kama ukiwa karibu na X wako basi kuna wakati utajisahau na kumtaja hivyo mwanaume atakua na wivu na hasira.

kwa mwanamke
kama hufanyi kazi na x wako, kama hakuna kitu cha kukulazimisha kuonana au kuwasiliana na X wako basi achana naye kabisa na mfute kabisa kwenye maisha yako.
Acha kabisa kumzungumzia, hata kama tayar ameshakufa,
Narudia tena, hata kama amekufa au amefiwa usiende kabisa kwenye msiba wake kwani akili za wanaume wengi haziwezi kulibeba hili katika Hali ya kawaida.

(6) Kuwa na marafiki wengi wakiume;

Kuna kale kamsemo wanawake wanasema "mimi siwezi kuwa na marafiki wanawake, wengi ni wambea Sana",

ila ukweli ni kuwa kila mwanaume anapenda kuwa na rafiki mwanamke, anayeongea naye, anachart naye akiwa na matatizo yake anamuambia.
Lakini UKWELI NI KWAMBA hakuna URAFIKI WA MWANAMKE NA MWANAUME, Ipo siku TU shetani Lazima Atafanya kazi yake.

Nakwambia,
hakuna mwanaume anapenda mwanamke ambaye kila dakika yuko na wanaume.

Kwa maana hiyo,
kuwa na marafiki wa kiume lakini kuwa na mipaka yako Kama mwanamke wa mtu.

Hata kama mwanaume wako anakuruhusu kutoka nao usifanye hivyo ANAKUPIMA.

Narudia tena,
Ni suala la muda tu utaharibu mahusiano yako, kitatokea kitu kidogo kitatibua kila kitu.
Hivyo punguza marafiki wanaume na kama unakua na wanawake acha kuwapa umbea wako mwingi.

(7) Mwana mke Unapofanya mambo yako kwa siri siri sana;

Kama mwanaume hakufichi mambo yake basi ukimficha yako jua kuwa akijua mahusiano hayatofika mbali.

Unapokuwa unafanya vitu vyako na marafiki zako, ndugu zako au mwenyewe mwenyewe mwanaume wako anapoteza kujiamini, haamini kama Ni kweli unampenda au uko siriasi na yeye.

Huamini, Kuna mtu Wako mbadala unaemwamini zaidi yake unamwambiia Siri zako. Yeye Hana maana.

Mfano:
Uko kwenye ndoa au uchumba, ila unajenga kimya kimya wakati mwanaume wako yeye kila Jambo anakushirikisha.

unatuma matumizi kwenu kisirisiri wakati mwanaume wako yeye akituma hukuambia,

unachukua mkopo benki bila kumuambia mwanaume wako, benki wanapokuja kudai ndo Siri hujulikana.

Unaaga unakwenda kwenu, Unaomba nauli, anakuuliza kuna Nini unamjibu "Ni matatizo ya kifamilia". Unaishia hapo tu.
Ni matatizo gani ayo ya kifamilia yasiopaswa kumshirikisha wenzi Wako.


Vyote hivo huua hisia na mahusiano taratibu.

Kama mwanaume wako sio mchoyo Wala mbinafsi anakushirikisha mambo yake, ni Vema na wewe mshirikishe ya kwako kwa moyo mmoja ili muwe kitu kimoja.

Ni hayo TU kwa leo,

Wadau KARIBUNI kweye mjadala na ninyi muongeze, mkosoe au MCHANGIE ya kwenu.

Alamsiki
 
Dah ni kweli ulichokisema ila hiyo no 3 wanaume mbadilike bana aliyekutenda alishapita why uhisi kama utatendwa na huyu pia, why uwe na mashaka mashaka?
Kabisa,
Ndo maana Kuna some gals hawapendi kabisa kudate na wanaume waliotoka kutendwa Sana Uko walikotoka.

Yaan ukimwambia TU,
"Nakupenda usije niumiza, uko Nilikotoka nimeshatendwa Sana"

Utaona Anakwambia,
"TUtasumbuana TU, mi sipendi wanaume wa type iyo"
 
Kabisa,
Ndo maana Kuna some gals hawapendi kabisa kudate na wanaume waliotoka kutendwa Sana Uko walikotoka.

Yaan ukimwambia TU,
"Nakupenda usije niumiza, uko Nilikotoka nimeshatendwa Sana"

Utaona Anakwambia,
"TUtasumbuana TU, mi sipendi wanaume wa type iyo"
Ikitokea umemkwaza kidogo anahisi yale yale tu aliyopitia huko nyuma🤷‍♂️ ila mengine kweli wadada tunazingua hasa hapo kumfananisha your man na watu wengine, kimaendeleo, hata muonekano tu, mi nna katabia nikiona mkaka mrefuu huwa nasema kabisa "wow mkaka fulani mrefu huyo 😉" naimagine babe mfupii si atanuna sana ila ntajirekebisha 😀
 
Back
Top Bottom