Wanawake, hivi kupika vizuri lazima mjaze mafuta kibao kwenye chakula?

lewis acid

Member
Mar 21, 2017
57
120
Jamani kuna jambo linanikera kwelikweli,

Kuna kasumba imeota mizizi kwa sasa, sijui niseme wanawake hawajui kupika au wanadhani wanaume tunapenda mafuta sana.

Hii tabia ya kumwaga mafuta kwenye chakula ni tabia ya hovyo mno, mtu unatoka mishe mishe una njaa unafika home unajisemea kimoyo chakula kije haraka nina njaa, hicho chakula kikiletwa ukitia mkono tu kama ni mboga basi mafuta yanang'aa yamewekwa kibao.

Hivi mnataka kukomoa mtu kupitia bajeti ya kununua mafuta au mnataka kukomoa mtu kiafya? Kwa nyie wanawake mnaoamini kwamba mapishi mazuri ni lazima mafuta yawe kibao mtatuua kwa magonjwa nawambia.

Takwimu za watu wenye pressure na kisukari zimeongezeka, fanyeni research ndogo tu mtaani kwenu mnapokaa mtakubaliana na mimi.

Upishi mbaya ni kuangamiza afya ya mwanaume na familia pia, kibaya zaidi ni kwamba baada ya muda mwanaume anaweza kubaki mwanaume jina tu. (Mnielewe vizuri hapa).

Hebu badilikeni.

UPDATES;
Naona mnatoa povu wanawake na baadhi ya wanaume, ila hili suala sio kwangu tu, watu wengi mnakula misosi ya hovyo siku hizi.

Mimi siishi kisiwani, nina marafiki, nina ndugu na jamaa, katika tour za mara moja moja nimebaini mapishi ya nyumbani kwangu na huko kwingine matumizi ya mafuta yamefanana.

Nyie mnao ni attack endeleeni ila ujumbe mmeupata, lengo mbadilike, mke wangu nimeshazungumza nae sasa nazungumza na nyinyi msiokua wake zangu, nyie ni shemeji zangu huu ujumbe uchukueni, mtatuua hata kama hampendi kuambiwa ukweli ndio nawambia sasa.

Povu ruksa.
 
Jamani kuna jambo linanikera kwelikweli.
Kuna kasumba imeota mizizi kwa sasa, sijui niseme wanawake hawajui kupika au wanadhani wanaume tunapenda mafuta sana.

Hii tabia ya kumwaga mafuta kwenye chakula ni tabia ya hovyo mno, mtu unatoka mishe mishe una njaa unafika home unajisemea kimoyo chakula kije haraka nina njaa, hicho chakula kikiletwa ukitia mkono tu kama ni mboga basi mafuta yanang'aa yamewekwa kibao.

Hivi mnataka kukomoa mtu kupitia bajeti ya kununua mafuta au mnataka kukomoa mtu kiafya?
, kwa nyie wanawake mnaoamini kwamba mapishi mazuri ni lazima mafuta yawe kibao mtatuua kwa magonjwa nawambia.

Takwimu za watu wenye pressure na kisukari zimeongezeka, fanyeni research ndogo tu mtaani kwenu mnapokaa mtakubaliana na mimi.

Upishi mbaya ni kuangamiza afya ya mwanaume na familia pia, kibaya zaidi ni kwamba baada ya muda mwanaume anaweza kubaki mwanaume jina tu. (Mnielewe vizuri hapa).

Hebu badilikeni

Ni kweli kabisa....wanawake wengi wanajisifu wanajua kupika lakini wanachofanya ni kurundika mafuta kwenye mboga.....mimi nilikishaa chaga kula nyumbani...nakula mara chache sana...hata hivyo mke wangu huwa haingii jikoni kabisa....nilishamshindwaga ..yeye na wadogo zake wote ni hivyohivyo...hapa nawasema mahouse girls
 
ni kweli wengi wanahis kumwaga mafuta ndo upishi !lahasha !jana nimeshangaa mtu kwenye thread ya upish wa supu anasema weka mafuta !dah yaan supu ya nyama au samak unatupia mafuta ya nn tena? HAIPENDEZI !mfundishe

kuna wanawake Hawafundishiki....siyo kwamba hawajui
 
Ni kweli kabisa....wanawake wengi wanajisifu wanajua kupika lakini wanachofanya ni kurundika mafuta kwenye mboga.....mimi nilikishaa chaga kula nyumbani...nakula mara chache sana...hata hivyo mke wangu huwa haingii jikoni kabisa....nilishamshindwaga ..yeye na wadogo zake wote ni hivyohivyo...hapa nawasema mahouse girls
Mbona maelezo meeeengi! Eti unajisifu umeacha kula nyumbani!
 
Huwa nawaambia mkipika unaweka nazi usiweke mafuta au mafuta yawe kidogo sana kwa mbali, asilimia kubwa ya mogonjwa ya moyo ni kula mafuta mengi sana yenye cholestrol
 
Usi generalize. Kuna nyumba nyingine hawatumii mafuta kabisa. Mimi najua wadada wa kazi ndio hupenda kujaza mafuta especially kama kuna mafuta ujazo wa lta 5 na kuendelea ndan. Mpe hela ya koroboi moja kama atajaza. Pambana na mademu zako
 
Ha ha mkuu si uingie jikoni upike ha ha

Pole kiukweli Chakula kikijaa mafuta kinakera hadi kinakifu haraka.....ongea na bibie ajifunze mapishi...siku hizi binti akiwa hajui kupika ni ujinga wake mwenyewe....aingie youtube / group za FB za mapishi ajifunze.
 
Tena Yale mamwanamke manene manene ndo yanapenda kupika na Mafuta meengi! Yanajifanya yamepika chakula cha gharama, yanakuwaga yananuka kuanzia mdomoni mpaka kila sehemu! mpaka roho imenichafuka khaa!
 
Back
Top Bottom