Wanawake hesabu zao ni kujumlisha tu za kutoa kwao hamnaga

Mr mgeni

JF-Expert Member
Apr 27, 2014
1,222
803
Mke wangu ni mfanyabiashara nikichukua kitu dukani nisipolipa ananiandika kwenye daftari haoni hata aibu.

Nikitoka kazini lazima anikumbushe deni namnukuu" samahani mume wangu nakudai sh.----, ila nimekukumbusha tu samahani lakini"

Hivi nanyi ambao wake zenu ni wachumi wanawafanyia kama huyu wangu? Na nyie wakina dada jamani kwanini mnakua hivyo unamdai mme wako hadi anakosa raha.
 
Tulipoambiwa tutakula kwa jasho ulielewa nini mkuu? Sie hatuwasaidii kuzaa kwa uchungu.
Tupambane tu na kuhudumia.

Asipokukumbusha kulipa duka litakufa utarudi kuleta uzi wanawake bure kabisa hawawezi chochote.
 
Wife wangu ni mfanyabiashara nikichukua kitu dukani nisipo lipa ananiandika kwenye daftari haoni hata aibu!?nikitoka kazini lazima anikumbushe deni namnukuu"samahani mme wangu nakudai sh.----,ila nimekukumbusha tu samahani lakini"
Hivi nanyi ambao wake zenu ni wachumi wanawafanyia kama huyu wangu?
Na nyie wakina Dada jamani kwanini mnakua hivyo unamdai mme wako hadi anakosa raha.
Anadai kistaarabu sana Mkuu, kama mimi nalipa bila tatizo. Na ni spirit nzuri kwa uhai wa biashara!
 
Wife wangu ni mfanyabiashara nikichukua kitu dukani nisipo lipa ananiandika kwenye daftari haoni hata aibu!?nikitoka kazini lazima anikumbushe deni namnukuu"samahani mme wangu nakudai sh.----,ila nimekukumbusha tu samahani lakini"
Hivi nanyi ambao wake zenu ni wachumi wanawafanyia kama huyu wangu?
Na nyie wakina Dada jamani kwanini mnakua hivyo unamdai mme wako hadi anakosa raha.
Kama vipi na wewe olewa tu upate raha za kuwa mke wa mtu.
 
Mtoa mada inaana hujui kuwa bandubandu humaliza gogo??

Unachotaka ni kufilisi duka sasa .
 
Back
Top Bottom