Wanawake bwana tukifanya kazi muda mrefu na kuchelewa kurudi nyumbani mnalalama ila tukikaa nyumbani bila kutoka tena mnalalama

Ndivyo tulivyo yani hata na sie kuna muda unajiuliza kabisa hivi nataka nini sasa.....sijui hormones, sijui shetani, sijui upendo sijui hata tusingizie nini.

Mtusamehe bure tu.
Hahahaha kwa kwel hatujawahi kujua tunataka nini maana kuna saa na mimi natamani tu atoke😂😂ila sasa ifike saa mbili ajarudi lazima akute mnuno wa kutosha
 
Mwananmke kama anapenda ndoa yake anatakiwa kuwahi kurudi hata akichelewa aombe ruhusa..


Hii ni africa..
 
Anataka usafiri naye, kwahiyo yeye hana kazi za kufanya?

Ushauri wangu:
Sio vema mwanamme kushinda nyumbani, hata kutazama mpira kuna namna tuliyokubaliana.
 
Hapo umenena wapo kama upepo.
Ukishinda nyumbani Ili watoto wakuzoee maneno ukiwa mtu wa kutokaa nyumbani maneno unazulula tu
 
Mwanzo Mimi binafsi nilikuwa nafanya kazi na taasisi fulani ila badae mwaka 2017 ilifunga shughuli zake nchini Tanzania.

Nikapoteza kazi na nikawa muda mwingi nipo nyumbani napanga mipango ya kupata pesa nikiwa nyumbani muda mwingi .

Yaani kwa wiki nilikuwa natoka siku 4 siku tatu nipo nyumbani.

Lakini cha kushangaza wife alikuwa ananinunia akiniona nyumbani na ni kwangu mpaka nikawa nakosa amani Mimi sio mlevi wala mtu wa kujichanganya sana na mambo ya club au starehe zozote ingawa starehe yangu kubwa ni kuangalia Mpira ambao naangalia nikiwa nyumbani.

Alikuwa akinuna sana sana na nimesota kweli ila nakiri hatujawai kushindwa kupata basic needs

Sasa mwaka huu mwezi 4 nimepata tena shavu na nimekuwa busy sana kusafiri mikoa mbali mbali na kurudi usiku kwa kufanya vikao vingi na shughuli nyingi na kurudi nimechoka sana

Ila ananuna na kupiga simu kila muda na kuwa kero hata kwa mabosi wangu yaani anataka niwai nyumbani kitu ambacho ni kigumu kwangu.

Hataki nisafiri mwenyewe anataka nisafiri nikiwa naye safari ya kikazi duh!

Nimeshindwa kuelewa anataka nini nifanye ili niweze kumridhisha maana sielewi kabisa alikuwa anapenda nifanye kazi au anapenda nikae tu jobless.

Ananiweka njia panda.

Ndo walivyo hapo anahisi tayari una mchepuko.
 
Ni kawaida kabisa, alishazoea kuwa na wewe mida mwingi sasa haupo kama alivyozoea anakuwa nakaumis .. anashindwa kuongea romantically..
sasa anakuwa kama anakisirani ndio hicho wahi kurudi, mara tusafiri wote anakosa tu namna yakuwasilisha feelings zake...

Tenga muda wa shoo kali.. na pia mara moja moja uwe unampigia simj kama unaongea na demu unayemyongoza
 
Back
Top Bottom