Wanawake Barani Afrika watakiwa kuchangamkia Fursa za Uongozi

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Wanawake katika nchi za Afrika Mashariki wametakiwa kujiamini na kuchangamikia fursa za uongozi katika ngazi mbalimbali ili kuleta usawa, suala litakaloondoa dhana iliyojengeka kwamba baadhi ya vyadhfa ni Kwa ajili ya wanaume pekee.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote wakati akifungua kongamano la mtandao wa wanawake barani afrika la maendeleo na mawasiliano (Femnet) lililoandaliwa na Kituo cha Usuluhishi {Crisis Resolving Centre} linalofanyika jijini Arusha.

Mhandisi Mlote,alisema kuwa idadi ya wanawake duniani ni kubwa na hivyo haoni sababu ya wanawake kubaki Nyuma katika suala la uongozi ambapo aliwakaribisha katika jumuiya ya Afrika mashariki kuchangamikia fursa za uongozi na kuleta usawa kwa wanaume.

"Wanawake popote pale walipo wajione kama wao ni viongozi na uongozi wao isiishie kwenye familia zao bali wajitokeze kuonyesha uwezo wao katika kuongoza na sisi wanaume tuwape nafasi maana mwanamke ukimpa uongozi hana longolongo"alisema Mlote.

Kwa upande wake, Mhandisi Pamela Maasai ambaye ni mbunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA)alisema kuwa wanawake wengi barani afrika wamekuwa wakisita kugombea nafasi za uongozi Kutokana na athari za mfumo dume uliojengeka miongoni mwa Jamii.

Alisema baadhi ya wanaume ni kikwazo katika kutoa ushirikiano Kwa wanawake pindi wanapotaka kugombea nafasi za uongozi wakiamini kwamba mwanamke ni kiumbe dhaifu hawezi kumwongoza mwanaume jambo ambalo limepitwa na wakati.

Pamela ambaye ni msemaji wa umoja wa wanawake katika bunge la EALA,aliwashauri wanawake kutumia fursa za uongozi kuonyesha uwezo wao ili kujenga mazingira ya kuaminila.

"Wanawake tuache woga tujiamini na tugombee nafasi mbalimbali za uongozi hasa katika nyaja za siasa na tulipata tionyeshe uwezo wetu "alisema

Naye Rose Mjilo kutoka shirika la mimutie women kutoka jamii ya kifugaji wilayani Ngorongoro, alisema changamoto ya mfumo dume Kwa Jamii ya kimasai bado ni kubwa hivyo elimu zaidi inahitajika ili kuikwamua jamii hiyo kuachama na dhana hiyo.

Alisema jamii ya kimasai bado inaendekeza mfumo dume wa Uongozi Kwa wanawake na kutolea mfano kuwa hivi karibuni alijitosa kugombea mchakato wa kupitishwa kuwa mgombea ubunge katika jimbo la ngorongoro akiwa mwanamke pekee lakini wanaume walimbeza na kujikuta akikosa hata kura Moja.

Naye mbunge wa Afrika Mashariki kutoka Nchini Rwanda Fatuma Ndangiza, alisema usawa wa kijinsia sio suala la wanawake pekee bali ni suala la jamii kwa kuwa changamoto kubwa ni tamaduni zetu hivyo jitihada zaidi zinahitajika katika mshikamano ili kuondoa dhana ya mfumo dume.

Ends....

IMG-20211119-WA0015.jpg
IMG-20211119-WA0018.jpg
IMG-20211119-WA0019.jpg
IMG-20211119-WA0017.jpg
 
Back
Top Bottom