Wanawake acheni kulipa visasi, msishindane na mwanaume mtaumia

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
667
1,795
Miezi kadhaa imepita baada ya mke wa jirani yangu kumfumania mme wake akiwa na mchepuko lodge fulani hapa mjini

Baada ya fumanizi mke wa jamaa aliapa kuwa lazima atalipa kisasi mbele ya mme wake na kadamnasi na kweli baada ya miezi kadhaa mwanamke akapata naye mchepuko

Na ili kumkomoa mme wake akaamua kupata ujauzito wa mchepuko na juzi kaenda klinic kupima ujauzito na HIV bahati mbaya kagundulika ameambukizwa na pia ameambukizwa kaswende

Hata hivyo alilaumu kuwa aliyemwambukiza ni mme wake na kuzua taharuki ya familia lakini hata hivyo walienda wote kituo cha afya wakapime kwa pamoja

Mwanaume amechukua vipimo ameonekana hana maambukizi yoyote na mwanamke ameonekana kuwa ni positive

Kikao cha familia kilipokaa mwanamke aliamua kuwa wazi na kuanza kujilaumu kuwa kisasi kimemgharimu

Mwanaume alipoulizwa kwani tangu mke wako akufumanie hamkuwahi kukutana kimwili

Mwanaume akajibu" Sikuwahi kwa sababu mwanamke alikataa kunipa mapenzi na nikaacha, na alikuwa yupo bize anachat na mchepuko wake hata tukiwa tumelala sikufanya lolote niliamua kunyamaza niangalie kisasi chake kinavyofanya kazi "

Mwanamke alivyoulizwa kuhusu kuchepuka na kuambukizwa HIV alisema" Ilibidi afanye hivyo baada mme wake kuwa na tabia za kumcheat,kabla hatujazaa mtoto wa kwanza nilimkuta na binti mmoja akaniomba msamaha nikaacha,nimewahi kuona sms anazochat na wanawake mitandaoni ,niliumia sana nikavumilia ,miezi kaadhaa imepita nilimfumania gest ndipo niliamua na mimi kuchepuka "

Je ni halali kulipa visasi kwenye ndoa ?

Wanawake acheni visasi,vinaweza kukugarimu
 
Miezi kadhaa imepita baada ya mke wa jirani yangu kumfumania mme wake akiwa na mchepuko lodge fulani hapa mjini

Baada ya fumanizi mke wa jamaa aliapa kuwa lazima atalipa kisasi mbele ya mme wake na kadamnasi na kweli baada ya miezi kadhaa mwanamke akapata naye mchepuko
Mhh!
 
Mshahara wa dhambi ni mauti
 
Duh, Mke achepuke na mimba ya mchepuko juu!, bado utasema huyo ni mke?

Hao walishaachana ila walikuwa bado wanaishi kwenye Nyumba moja. Sikuhizi kuna Singo Mother wanaoishi na waume zao.
 
Miezi kadhaa imepita baada ya mke wa jirani yangu kumfumania mme wake akiwa na mchepuko lodge fulani hapa mjini

Baada ya fumanizi mke wa jamaa aliapa kuwa lazima atalipa kisasi mbele ya mme wake na kadamnasi na kweli baada ya miezi kadhaa mwanamke akapata naye mchepuko

Huwezi kumlipizia mume mchepukaji kwa wewe kuamua kuchepuka halafu ukapata faida yoyote au ukawa salama.
Pole kwake mwanamke mwenzangu maana Mungu amemlipa papo kwa papo wakati mwanaume anaugulia ndani kwa ndani

Ila mwisho siku yote hayo yaliyotokea mwanume ndio chanzo

"Muishi nao kwa akili"
 
Pole sana .. utazoea tu usijali.. na ungekuwa mwanaume alaf hiyo sentence ungeisema kulingana na uwanaume wako tungekushangaa sana kwa vile maliyamtu enjoy your life
Sawa mkuu asantee,Ila ndo hvyo uvumilivu Ni Jambo gumu Sana na wakati mwingine kulazimishwa kusamehe hata Kama unataka au hutaki Ni utasamehe uishi kwa amani au ubaki nalo rohoni upate jaka la roho
 
Back
Top Bottom