EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,303
Polisi wilayani Same imewakamata wanawake 38 kwa tuhuma za kukeketa wasichana wadogo. Wanawake hao walikamatwa juzi Jumapili wakati wakicheza dansi ya kitamaduni ya kuzunguka nyumba iliyokuwa na wasichana 21 wenye umri kati ya miaka 3 na 15 ambao tayari walikuwa wameshakeketwa.
Akiongea na vyombo vya habari, Meya wa wilaya ya Same, Mh. Herman Kapufi, alisema kuwa aliwafahamisha polisi mara tuu baada ya kusikia habari hizo za ukeketaji. Kapufi amesema baadhi ya wasichana hao bado walikuwa wanavuja damu sehemu zao za siri huku majeraha ya engine yakiendelea kupona.
Tanzania imepiga marufuku ukeketaji tokea mwaka 1998 ambapo mtu anayekutwa hatiani kwa kosa la ukeketaji anaweza kuhukumiwa hadi kifungo cha miaka 15. Hata hivyo, ukeketaji bado unafanywa kwenye baadhi ya jamii. Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 15 ya wanawake na wasichana wamekeketwa huku vinembe vyao vikiwa vimekatwa na kuondolewa kabisa kwenye sehemu zao za siri.
Mara nyingi ukeketaji huo hufanywa kwa kutumia kisu, wembe au kitu kingine chenye nja kali bila ganzi au taratibu zozote za kiafya. Baadhi ya wasichana hupoteza maisha yao kutokana na majereha makubwa yatokanayo na ukeketaji. Pia kuna jamii nyingine ambazo zinawatenga wanawake ambao hawajakeketwa.
Baadhi ya watafiti wa mambo wanadai kuwa baadhi ya watu wanaamini kuwa mwanamke aliyekeketwa anakuwa mwaminifu zaidi kwa mume wake.
Habari kwa hisani ya AFP