Wanawake 11 wateuliwa kuwa mawaziri Ufaransa kati ya mawaziri wote 22

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameteua baraza la mawaziri lenye usawa wa kijinsia kuambatana na ahadi ya mapema ambapo 11 kati ya mawaziri 22 ni wanawake.

Sylvie Goulard ndiye waziri mpya wa ulinzi huku bingwa wa olimpiki wa mchezo wa kupigana na panga Laura Flesseng, akiteuliwa kuwa waziri wa michezo.

Bruno Le Maire ameteuliwa kuwa waziri wa uchumi, Gérard Collomb waziri wa masuala ya ndani, huku naye François Bayrou ndiye waziri wa sheria.

Rais huyo mpya wa Ufaransa ana matumaini kuwa kikosi hicho kitazoa kura nyingi kwenye uchaguzi wa ubunge mwezi ujao.

Alitimiza ahadi yake ya kuwepo usawa kwenye baraza la mawaziri, lakini kati ya nafasi muhimu tano , ni moja ya tu ya ulinzi ilimuendea mwanamke.

Mawaziri wengine ni pamoja na Jean-Yves Le Driana, ambaye ameteuiliwa kuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni.

Wengine ni pamoja na:
  • Agnès Buzyn - Afya
  • Murielle Pénicaud - Kazi
  • Mounir Mahjoubi - Masuala ya dijitali
  • Françoise Nyssen - Utamaduni
  • Jean-Michel Blanquer - Elimu ya taiafa
  • Jacques Mézard - Kilimo na chakula
 
Wazungu ni watu ambao wakitoa promise lazima watatekeleza hata hiwe ni ahadi mbaya lakini najua bwana Emmanuel Macron ametekeleza ahadi ambayo mwenyewe hana imani nayo kutoka moyoni lakini kwa vile aliwapromise Wafaransa hana budi kutekeleza
 
Back
Top Bottom