Wanaume wote wa JF someni hii,mmoja wenu ndo kafanya haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume wote wa JF someni hii,mmoja wenu ndo kafanya haya

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by makaburini, Dec 28, 2011.

 1. m

  makaburini Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanaume wa jf someni hii thread,na kwa sababu muhusika yupo humu basi ujumbe wake utakuwa umemfikia. Wiki ilopita kulikuwa na kauhaba ka mafuta ambako hakakuchukua siku nyingi, nikiwa njiani narudi kazini alinipigia simu dada mmoja ambaye tunafahamiana naye pamoja na mumewe akiniomba nimsaidie sababu gari lake halina mafuta, na yupo somewhere Morogoro road akiwa anatokea kazini na sheli za karibu hazikuwa na mafuta.

  Nikapitia kumnunulia sheli moja nilipata taarifa kuwa inauza mafuta na ndipo nilipompelekea sehemu alipo na kumkuta mwenye majonzi lakini alijitahidi kutabasamu baada ya kuniona na baada ya kumuwekea mafuta nilimuuliza mumewe aliko akajibu kwa unyonge yupo kazini!

  Nikamuuliza tena kwa nini usimwambie kwa kuwa hapa ni karibu na ofisini kwake dada machozi yakaaza kumtoka nikaamua nimuache aende!

  Baada ya siku chache nilimpigia kumuuliza akaniambia shemeji, naishi bila matumaini bora ya mgonjwa wa ukimwi! Akasema kuwa siku ile alimueleza mumewe tatizo hilo akamjibu" kwa hiyo.......unataka nikusaidiaje.....kwani mimi nauza mafuta ya gari???

  Kama uliweza kununua gari iweje ushindwe kulihudumia, kwanza mimi nina kazi zangu ofisini sina muda .........dada akaamua akate simu maana angeendelea kumsikiliza angemuumiza maana maneno yaliyokuwa yanatoka kwa mumewe wa ndoa ni makali.

  Najiuliza hivi sisi wanaume hawa wadada wa watu huwa tunawaoa ili kuwakomoa? Au hatujui maana ya ndoa? Au ni ushamba? Utoto? Au ni ukatili tu tunaamua kuwafanyia?

  alitaka amwambie nani amsaidie kama si mumewe? why jamani tunakuwa wakatili hivi?? aghhhhhhhhh

  Hebu wanaume wenye hekima jf tusaidiane kumshauri mwenzetu naona hajielewi na haelewi majukumu yake.
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Loh ndoa hii lazima
  1. Wamechokana
  2. Wakati wa tukio kulikuwa na jiugomvi
  3. Nyumba ndogo inahusika.

  Pole dada ila kuna wanaume wenye majibu ya kuumiza!
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mafuta tu ya gari?
  Au kuna jingine?

  Mafuta ya gari tu hayavunji ndoa.
   
 4. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Simply huyo mwanaume hapendi huyo mkewe atumie hilo gari. Kutokana na comment ya huyo bwana, yaelekea hilo gari ndio chanzo cha ugomvi wao.
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Na pengine lilinunuliwa pasipo makubaliano au idhini ya Mume kama wengine wanavyopenda
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo mengi hapo na sio ugomvi tuu wa mafuta
  Kuna kitu kingine kipo nyuma ya pazia na walishagombana sana
  hapo ugomvi wa mafuta ulikuw akikolezo tuu
  na inawezekana hata hilo gari huyo mume wa huyo dada hataki alitumie na limeleta mgogoro toka liliponunuliwa
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mwambie awe anapanda dala dala na hilo janaume ni lazima liwe na umeme na mwanamke ni gumegume..by khadija kopa
   
 8. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Ndoa....doa....ndoano...donoa...
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hao ndo wanaume
   
 10. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  precisely!!!
   
 11. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Mumewe ndie waubavu wake, sasa anapojibiwa vya kukatisha tamaa jamani ndo iweje na akasaidiwe na nani?? Mkuu yawezekana kuna kinagaubaga hapo kati kimefichwa, wao waseme tu ukweli!!! MJ1.....nakubaliana nawewe, yawezekana uloyataja yakahusu!!
   
 12. s

  sawabho JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Kuna mgogoro katika familia hiyo, sio rahisi mtu kumjibu hvyo Mrs wake kama wako katika good terms. Hatahivyo, umesikiliza upande mmoja, sio vizuri kutoa maamuzi kwa kusikiliza upande mmoja tu. Fanya mpango usikilize na upande wa pili yaana mwanaume ili kuona chanzo cha majibu mabaya.

  Huenda huyo Bi. Dada hakumshirkisha mumewe wakati wa kukunua hilo gari, labda mwanaume alishtukia gari nje kuuliza kulikoni, kajibiwa...................au Mwanaume alishirkishwa lakini kwa wakati huo kukawa na jukumu lingine la kufanya na hiyo pesa kama vile karo kwa watoto, kujenga nyumba, kulipia pango nk.....(ni mawazo yangu tu).

  Na, je huyo mwanaume yeye ana usafiri?
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,917
  Likes Received: 23,556
  Trophy Points: 280
  :juggle::photo:
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  KUna uwezekano kuwa kweli mumewe alimjibu hivyo... lakini pia kuna uwezekano pia kuwa unategwa wewe
   
 15. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kuna mambo ya kwenye ndoa ukiyasikia hata kutamani ndoa inakuwa vigumu sana. Hivi hata kama mmegombana ndio mwenzio anapokuwa na shida huwezi kumsaidia hata mawazo tu? Inawezekana kweli asingeweza kumsaidia labda yupo kazini lakini hata maneno ya kutia moyo kidogo hakuna?????? Khaaaaaaaaaa!!!!!
   
 16. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  upuuzi mtupu .yaani niishi kwa matumaini kisa wese? daladala zimeisha? je bajaji? je bodaboda? je punda? wanawake wengi wanaishia kujiuza kisa tu waonekane wanadrive
  mtu anakuwa na wanaume kibao kisa gari
  switi wa mafuta.
  honey wa service
  darling wa leseni
  angel wa insurance nk nk
  huyo jamaa yako yuko right kabisa ukinunua gari ujue na jinsi ya kulihudumia maana sio kitu cha muhimu sana hiyo ni luxury thing.kama huna huwezo achaaaaaaaaaaaaaa.
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mwanamke atakuwa kachuja tayari kwa mwanaume hapo hakuna jinsi ni kurenew tena penzi aanze utotoni kama mwanzo.
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huwa nakupendaga sana kwa kuwapaga mashosti ukweli
  hilo gari wakati anajinunulia mbona hakuombaga msaada si alijinunulia mwenyewe?
   
 19. s

  sawabho JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Sio kweli, ni huyo tu na baadhi ya wenzake ndo wanaume.
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Gari si alijinunulia na hakuomba msaada iweje mafuta aombe msaada?
   
Loading...