Wanaume wenzangu, umewahi kupigana kwa ajili ya Mwanamke na bado ukaishia kutoswa?

Lizarazu

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
6,334
7,868
Habarini za jumamosi wana MMU?

Katika maisha ya kimahusiano wanaume tumekuwa tukifanya mambo mengi sana kwa ajili ya wanawake tuwapendao ikiwemo kupigana na mwanaume mwenzio na chanzo ikiwa ni yeye.

Na mara nyingi huwa tunafanya hivi pasipo kushurutishwa na mtu yeyote, bali huwa tunasukumwa tu na ego zetu za kiume hili kutaka kumuhakikishia tu kwamba wewe ni kidume haswa(zagamba).

Bahati mbaya unaweza ukapigana mpaka ukatolewa jicho ukiamini kwamba unapigania penzi lakini yeye kwa upande wake asishtuke kabisa na akakuacha mchana kweupeee!! Ukabaki unajilaumu tu na kuonekana mjinga.

HIKI NI KISA CHANGU KILICHOTOKEA MIAKA KADHAA ILIYOPITA.

Nilipokuwa form one kuna mtoto mmoja wa kihaya mashalah alikujaga second-selection na mimi ndio nilikuwa mtu wa kwanza kumzoea pale shuleni kwa maana nyingine mimi ndie nilikuwa mwenyeji wake.

Yule mtoto kiukweli alitokea kunielewa sana na hata mimi mwenyewe pia nilimwelewa vilivyo na mwisho wa siku nilimtongoza lakini hakunipa jibu.

Sasa wakati bado nipo nasubiri jibu, akatokea jamaa mmoja wa Form-three akamtongoza na ndani ya muda mfupi tu yeye akakubaliwa akaanza na kumla kabisa na mbaya zaidi demu akaanza kunipotezea mimi, kiukweli niliumia sana na nikatokea kumchukia yule jamaa.

Nakumbuka ilikuwa ni siku ya Ijumaa siku hiyo sikwenda shuleni na madaftari nilienda kwa kazi moja tu, kumshikisha adabu mtu ambaye nilimuona kama ameninyang'anya demu wangu....

Yule demu nakumbuka mara nyingi muda wa kutoka shule alikuwa anaongozana na mshikaji, sasa mimi siku hiyo niliwavizia sehemu ambayo wako wenyewe wawili tu njia nzima na bahati nzuri ikawa hivyo kweli.

Nilipowafikia nikawasimamisha yule demu akanipuuza, lakini jamaa yake akasimama tena kwa kujiamini kabisa halafu akaanza kunipiga beat eti nisimzoee kabisa demu wake, nami sikukaa kimya nikaanza kumjibu...jamaa alivyojiroga si akanikwida kisa tu yeye ni mrefu basi acha iwe varangati hapo!

Nakumbuka yule jamaa nilimpiga kabari moja matata hadi akaanza kupiga kelele za kuomba msaada na hapo ni baada ya kuwa ameshaning'ata lakini akaona simwachii maana nilikuwa nna hasira nae vibaya mno.

Jumatatu iliyofuata nilikutana na yule demu wake ambaye ndio alikuwa chanzo cha ugomvi, alinitukana sana akisema kwamba eti nilitaka kumuua mtoto wa watu(bwana yake) bila kosa lolote na kamwe hawezi kuwa na mimi, baada ya hapo hatukuwahi kuongea tena mpaka ana hama shule form-two.

Niliumia sana kumkosa yule demu maana mbali tu na kupigana kwa ajili yake pia mimi ndio nilikuwaga namfundisha, alikujaga kuanza shule hajui chochote hata pre-form one alikuwa hajasoma, nilijitoa Sana kwa yule binti wakati yule jamaa mwingine aliyempata alitumia status ya "u-form three tu.

Kwangu Mimi hiki ni kisa ambacho nakikumbuka kwa ukaribu, unaweza na wewe uka-share kisa chako hapa!

Je umewahi kupigana kwa ajili ya mwanamke na bado mwanamke huyo ukamkosa!??

Karibu.
 
Miaka kidogo imepita sikupigana Ila nilipigwa na vijana mtaani..

Nyumba niliyohamia nilitokea kuzoeana na jirani yangu alikuwa mrembo haswa,kila nikirudi kwenye mihangaiko akiniona ananichangamkia lakini sikuwa na uhusiano nae

Kuna siku nimeshuka kwenye bodaboda niingie ghetto namuona jirani anatoka dukani akanichangamkia Kama kawaida tukawa tunaongozana taratibu...
Dk 2 mbele nikashangaa nimechotwa mtama niko juu juu kimo cha ndama ile nimetua chini tu jamaa mwingine kanipa teke la mgongo nikasota kwa kalio Kama hatua 3-4 mbele,nikamaliziwa na Kofi zito nikawa mwekundu kama nyanya..
Kumbe bhana jirani wale wahuni walikuwa wanamkubali lakini alikuwa hawataki so wakaamua wapoze machungu kwa kunipa kipigo maana walikuwa wanasema "haiwezekani mgeni tu anahamia mtaa huu anatuzibia rizki"
 
mi jana tu nimetoka kumkuta demu wangu yuko na mzee flani bar na nilikua najipitia zangu nile moja baridi nikapaki gari pembeni ya gari yake nikaenda kaunta nikaagiza bia zangu mbili badae jamaa alivyoondoka nikabeba mzigo wangu nikaenda kuuchakata japo nilikua na hasira kwa mbali ila siku mmaindi wala nini na nime take advantage kuwa na mimi ntakua nazichakata pisi mpya asilete wivu tu maisha ya kupigania mwanamke yameishapitwa na wakati japo alikua anasisitiza nisimlipizie
 
Dizaini ya mleta mada ndiyo mashabiki wa Chadema wako hivyo wote

Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app
Watu Kama wewe shuleni walimu wenu wala hata huwa hawapati shida kwenye kusahihisha mitihani yenu.

Mwalimu anasoma mistari miwili tu Kisha anabaini hili jinga limeenda OP tayari anapiga mstari tu kwisha habari.

Nina uhakika kabisa hujasoma mada umekimbilia kutoa comment tu.

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Dah!!! Sitaki hata kukumbuka aisee,maana nilichapwa na waya wa kufuri za baiskeli na demu akanikana hapohapo kuwa hanijui masela wakamchukua akaenda kuliwa,enzi hizo tunatoka mziki kijijini huko mida ya tisatisa hivi usiku,dah!!
Duuh pole Sana mazee!! Ila naamini hicho kisa kilikufunza Kama Mimi changu kilivyonifunza.

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Miaka kidogo imepita sikupigana Ila nilipigwa na vijana mtaani..

Nyumba niliyohamia nilitokea kuzoeana na jirani yangu alikuwa mrembo haswa,kila nikirudi kwenye mihangaiko akiniona ananichangamkia lakini sikuwa na uhusiano nae

Kuna siku nimeshuka kwenye bodaboda niingie ghetto namuona jirani anatoka dukani akanichangamkia Kama kawaida tukawa tunaongozana taratibu...
Dk 2 mbele nikashangaa nimechotwa mtama niko juu juu kimo cha ndama ile nimetua chini tu jamaa mwingine kanipa teke la mgongo nikasota kwa kalio Kama hatua 3-4 mbele,nikamaliziwa na Kofi zito nikawa mwekundu kama nyanya..
Kumbe bhana jirani wale wahuni walikuwa wanamkubali lakini alikuwa hawataki so wakaamua wapoze machungu kwa kunipa kipigo maana walikuwa wanasema "haiwezekani mgeni tu anahamia mtaa huu anatuzibia rizki"
Noma Sana mzee!! Kisa chako kimenikumbusha jamaa yangu mmoja tuliendanae kwenye graduation ya A-LEVEL Ngaza girls, jamaa alikuwa ni mtalaamu wa kucheza dancel music,yaani alikuwa akianza kucheza hivi watu wanasimama wanabaki wanamuangalia yeye tu.

Basi Kuna demu mmoja alikuwa anacheza na mchizi wake, si akavutiwa na huyo jamaa yangu jinsi alivyokuwa anayarudi...alichokifanya yule demu akamuacha mchizi wake halafu akaja kucheza na jamaa yangu, Basi acha jamaa abambie! alibambia halafu demu kama ghafla akatokea kumuelewa hivi.

Baadae tukaona yule mchizi wake na yule demu amepotea sisi hatukujali..mwana akaendelea kubambia tu.

Kumbe bwana yule jamaa alipotoka mle ndani kwenye disco, akaenda kutusubiria huku nje akiwa na wapambe wake Kama 15 hivi.

Ile tunatoka tu nje hatuna habari yoyote Kama Kuna majangiri yanatusubiria huku nje kutupa kichapo, wakamdaka jamaa yangu aliyekuwa anacheza na demu wao.... Aisee walimlaza chini wakamchalaza stiki Kama mtoto mdogo!

Ila wanaume kuna muda huwa tuna ufala mwingi sana... Angalia Kama huyo yaani alikuja kutufanyia fujo sisi wakati demu wake mwenyewe ndio alitufuata.

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Kwa uwingi wa Wanawake uliopo tena wakiwa wanazidiana kwa Uzuri, ukiona Mwanaume anapigana kwa ajili ya Mwanamke jua Uchizi unamwita.
Mara nyingi wanaume tunafanya hivi vitu sababu ya scarcity mentality.

Kama umeu-train ubongo wako kuwa na aboundant mentality kamwe huwezi kupigania mwanamke au kuteseka kwa namna yoyote ile kisa mwanamke

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Habarini za jumamosi wana MMU?

Katika maisha ya kimahusiano wanaume tumekuwa tukifanya mambo mengi sana kwa ajili ya wanawake tuwapendao ikiwemo kupigana na mwanaume mwenzio na chanzo ikiwa ni yeye.

Na mara nyingi huwa tunafanya hivi pasipo kushurutishwa na mtu yeyote, bali huwa tunasukumwa tu na ego zetu za kiume hili kutaka kumuhakikishia tu kwamba wewe ni kidume haswa(zagamba).

Bahati mbaya unaweza ukapigana mpaka ukatolewa jicho ukiamini kwamba unapigania penzi lakini yeye kwa upande wake asishtuke kabisa na akakuacha mchana kweupeee!! Ukabaki unajilaumu tu na kuonekana mjinga.

HIKI NI KISA CHANGU KILICHOTOKEA MIAKA KADHAA ILIYOPITA.

Nilipokuwa form one kuna mtoto mmoja wa kihaya mashalah alikujaga second-selection na mimi ndio nilikuwa mtu wa kwanza kumzoea pale shuleni kwa maana nyingine mimi ndie nilikuwa mwenyeji wake.

Yule mtoto kiukweli alitokea kunielewa sana na hata mimi mwenyewe pia nilimwelewa vilivyo na mwisho wa siku nilimtongoza lakini hakunipa jibu.

Sasa wakati bado nipo nasubiri jibu, akatokea jamaa mmoja wa Form-three akamtongoza na ndani ya muda mfupi tu yeye akakubaliwa akaanza na kumla kabisa na mbaya zaidi demu akaanza kunipotezea mimi, kiukweli niliumia sana na nikatokea kumchukia yule jamaa.

Nakumbuka ilikuwa ni siku ya Ijumaa siku hiyo sikwenda shuleni na madaftari nilienda kwa kazi moja tu, kumshikisha adabu mtu ambaye nilimuona kama ameninyang'anya demu wangu....

Yule demu nakumbuka mara nyingi muda wa kutoka shule alikuwa anaongozana na mshikaji, sasa mimi siku hiyo niliwavizia sehemu ambayo wako wenyewe wawili tu njia nzima na bahati nzuri ikawa hivyo kweli.

Nilipowafikia nikawasimamisha yule demu akanipuuza, lakini jamaa yake akasimama tena kwa kujiamini kabisa halafu akaanza kunipiga beat eti nisimzoee kabisa demu wake, nami sikukaa kimya nikaanza kumjibu...jamaa alivyojiroga si akanikwida kisa tu yeye ni mrefu basi acha iwe varangati hapo!

Nakumbuka yule jamaa nilimpiga kabari moja matata hadi akaanza kupiga kelele za kuomba msaada na hapo ni baada ya kuwa ameshaning'ata lakini akaona simwachii maana nilikuwa nna hasira nae vibaya mno.

Jumatatu iliyofuata nilikutana na yule demu wake ambaye ndio alikuwa chanzo cha ugomvi, alinitukana sana akisema kwamba eti nilitaka kumuua mtoto wa watu(bwana yake) bila kosa lolote na kamwe hawezi kuwa na mimi, baada ya hapo hatukuwahi kuongea tena mpaka ana hama shule form-two.

Niliumia sana kumkosa yule demu maana mbali tu na kupigana kwa ajili yake pia mimi ndio nilikuwaga namfundisha, alikujaga kuanza shule hajui chochote hata pre-form one alikuwa hajasoma, nilijitoa Sana kwa yule binti wakati yule jamaa mwingine aliyempata alitumia status ya "u-form three tu.

Kwangu Mimi hiki ni kisa ambacho nakikumbuka kwa ukaribu, unaweza na wewe uka-share kisa chako hapa!

Je umewahi kupigana kwa ajili ya mwanamke na bado mwanamke huyo ukamkosa!??

Karibu.

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
Mapenzi kama hayo sijui upigane na mwaname mwenzako kwa mwanamke ni tabia za kibongo kule kwetu mwanamke akisaliti tu unampa nyekundu, unavumila kwa muda unampa fursa mwanamke mwengine.,
 
Hujawai kupenda kama hujawai kulia
Tukubali tukatae, mapenzi yanaweza kukupelekea kufanya jambo ambalo hukutegemea kufanya.

Waliopigana kisa mwanamke, siwezi kuwalaumu ni msukumo wa mapenzi ulipelekea kufanya hivyo.

Umeongea pointi kubwa mno tena ya kufungia mwaka.
 
Back
Top Bottom