Wanaume wenzangu, kuwa na mpenzi mmoja ni hatari kuliko ugonjwa wa kisukari

Uhuru na Kazi, Kazi na Bata!

Tukiacha unafiki pembeni, wengi ni mashahidi katika hili.

Unapokuwa na 'mahusiano' mapya, kuna raha sana kimwili na kihisia. Kila wakati unatamani kuwa na mpenzi wako, japo kwa maongezi tu kwa njia ya simu ikiwa yuko mbali nawe.

Kila unachofanya unatamani kumshirikisha na kusikia maoni yake, hamu ya kuwa naye inakuwa katika kiwango cha juu sana kisichomithilika.

Hiki ndo pekee kipindi ambacho furaha yako ya mapenzi unapaswa kuipima, lakini cha ajabu baada ya muda haya yote husahaulika na kupotea kabisa!

Basi achana na porojo za kuvumilia kwamba hiyo ni kawaida, hakuna cha kawaida hapo. Ndiyo maana ukipata mpenzi mwingine ile furaha tele hukurejea tena.

Sisemi hii kwa lengo la kupotosha au kuhamasisha mtindo usiofaa, la hasha. Ni ukweli ambao upo hata nisipokwambia, mimi ndivyo ninavyojisikia.

Hata katika mahusiano yenye malengo madhubuti, mathalani kuelekea ndoani. Kipindi cha furaha kwa walio wengi ni kipindi cha uchumba tu, hapa kila mmoja anakuwa 'at their best'.

Baada ya hapo huko ndoani ni uvumilivu tu na kulea familia, ndiyo maana wajanja waliostukia huwa hawavuki hatua ya uchumba. Furaha ikiisha piga chini, pata mchumba mwingine kula raha mpya.

Note:
Linapokuja suala la familia itabidi uvumilie tu, lakini sio kweli kwamba utazipata raha kwa kiwango kile... labda mjifanyishe tu ili siku ziende.

Kupanga ni kuchagua, nimechagua FURAHA.

Unachozungumza broo Kina ukweli mimi nilishawahi kutumia hii kanuni siku nilipogundua mpenzi nilienae amenichoka na tunapoelekea muda wowote tunaachana

Nilichofanya nilitafuta mpenzi mpya hivyo kipindi penzi linavunjika upande wa kwanza moyo ulikuwa umeshahamia upande wa pili kwaiyo mpka siku demu wangu anabwaga manyanga hivyo kipindi ana sms amekaa amefikiria ameona bora tuachane mi nilimjiku “ok” bila maelezo

Baada ya mwezi kupita alianza kunisumbua kuniuliza maswali yasiyo na msingi akitaka kujua saivi natoka na Nani mara Ohoo ivi ulikuwa unanipendaga kweliii wewe au ulikuwa unanichezea ukimuuliza why unaniuliza maswali haya wakati ulishaniacha hajibu sms yako tena
 
Furaha ni kwa jinsia zote mkuu, kwanini umeona mashiko kwa vijana wa kiume tu... hata mabinti wanahitaji hicho kipindi cha kufurahi.
Mkuu kwema.nimeshindwa kabisa Ku digest hii hoja yako.
Though hujaoongelea sana watu walioko kwenye ndoa tayari,umesema kwamba kuna raha sana MTU anapokuwa na mahusianao mapya yana raha yake,.kuliko aliyonayo,
Una ushauri gani kwa wanawake walioolewa tayari kuhusu utamu Wa mahusiano mapya nje ya ndoa.
 
Back
Top Bottom