BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,825
- 287,845
Wanaume wengi wasingiziwa watoto
Faraja Mgwabati
Daily News; Sunday,April 20, 2008 @00:01
MATUMIZI ya kipimo cha kupima chembechembe asili za urithi katika mwili wa binadamu (DNA), yamegundua kuwapo kwa udanganyifu mkubwa wa wazazi wanawake kuwasingizia wanaume watoto wasio wao, imefahamika.
Uchunguzi uliofanywa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) umeonyesha kuwa katika kipindi cha 2006/2007, kesi 209 zilipokewa na ofisa huyo na kupimwa DNA zilionyesha kuwa kati ya wanaume 98, sawa na asilimia 47 au nusu ya waliofika hapo walisingiziwa kuwa baba.
Katika uchunguzi huo wanaume 111, sawa na asilimia 53 ambao walikuwa wakikataa kwamba watoto siyo wao waliumbuka baada ya vipimo vya damu kubaini watoto hao ni wao.
Mkemia Mkuu wa Serikali Dk. Ernest Mashimba aliiambia HabariLeo mwishoni mwa wiki kuwa hata hivyo kumekuwa na mabadiliko katika idadi ya wanaume wanaokuta watoto si wao ikilinganishwa na mwaka uliopita ambao wanaume 150 kati ya 250 waliopimwa ili kuhakiki ubaba wao kubainika kwamba walikuwa wakisingiziwa baba wa watoto.
Mashimba alisema katika mwaka huo (2005/2006) wanaume 100 ambao walikuwa wakikataa watoto waligundua kwamba ni wao baada ya kipimo hicho. Alisema hivi sasa kuna mwamko mkubwa miongoni mwa wazazi kupima DNA na imesaidia wazazi kuweza kufahamu kama watoto wanaowalea ni wa kwao au la.
Ni changamoto kubwa wakati mwingine tunapokea wazazi wenye miaka 70 na watoto wenye miaka 40, inabidi uwape ushauri nasaha kabla ya kupima ili wasigombane, alisema Mashimba.
Alisema wazazi wanaotaka kupima DNA wanashauriwa kupitia mahakamani au Ofisi za Ustawi wa Jamii ili ofisi yake iweze kutoa majibu ya vipimo kwa taasisi hizo badala ya kuwapa wazazi wenyewe.
Mashimba alisema mtambo huo wa DNA pia umesaidia kuweza kugundua majambazi na kuwaachia huru watu ambao walishukiwa kuwa majambazi. Kwa 2006/2007 watu 24 walipimwa kati yake 15 walionekana hawana hatia.
Alisema gharama ya kupima sampuli za mtoto na mzazi mmoja ni Sh 200,000, na matokeo ya DNA hizo hutolewa ndani ya wiki mbili ili kutoa nafasi kwa mashine hiyo kukusanya sampuli zisizopungua 96 kabla ya kupima.
Hata hivyo Mashimba alisema pamoja na mtambo huo kusaidia wazazi na polisi kugundua wahalifu, kuna changamoto ya kutengeneza sheria ambazo zitasaidia kutoa mwongozo wa DNA.
Mfano alisema kuwapo kwa miongozo itakayofuatwa ya uchunguzi wa DNA bila kuathiri haki na usiri wa wahusika, kudhibiti uchunguzi holela wa DNA na kuepusha utumiaji mbaya wa matokeo ya DNA.