Wanaume wengi ni wapenzi wa jinsia moja bila kujijua!

'Wapenzi wa jinsia moja' maana yake nini? Kama unakusudia kusema 'ushoga' nadhani sio sahihi. Ushoga ni zaidi ya platonic love....mtu anavutiwa kufanya ngono na mtu wa jinsia yake. Sasa kama kitendo cha kukaa bar pamoja ama kufurahiana mnapo ongea kwenye simu ni ushoga then urafiki ni nini? Ndoa zina 'mambo' mengi sana, hili la kununiana ni mojawapo tu....mkiwa wawili mpo kimya lakini mkiwa mbele ya watu ni vicheko, mabusu etc kama kawa....ubatili mtupu.
 
naomba niwasilishe mtazamo wangu wa masuala ya mahusiano na urafiki.....

unakuta mwanaume mtu mzima ana mpenzi/mke na wanaishi pamoja au hata mbali kidogo,jamaa kila kukicha ni ugomvi na mwenziwe..hana muda wa kukaa na mpenzi wake wakacheka na kufurahi plus kuongea mambo ya maana na mipango ya maisha.........akitoka ofisini ni straight wanameet na marafiki zao...wanapeana stories wanacheka wanafurahi mpaka basi....njoo nyumbani sasa..hakukaliki!!achilia mbali tangu ametoka nyumbani asubuhi hajaulizia kuna hali gani,,mama akipiga simu inajibiwa kwa hasira!!!akipiga mshkaji mwanaume mwenzie inapokelewa kwa furaha na vicheko...hizo ni dalili tosha kwamba wewe ni mpenz wa jinsia moja au unapenda wanaume wenzio kuliko wanawake basi tu hujapata exposure ya kutosha ungekuwa ushatusuliwa.....au pengine..who knows!!

wanaume wenye tabia hizi inabidi mbadilike........sisemi uckae na jamaa zako la hasha..ila familia/mke/mpenzi should come first always.....

na vice versa is truu kwa dada zetu..

Hiyo iliku left hand side,embu tupe RIGHT HAND SIDE tujue ukweli
 
Kwa kawaida hakuna Mwanaume ambaye anapenda maudhi nyumbani. Kama nikirudi home my wife akawa mkali bila sababu za msingi na kama attempt zote za kumrekebisha na kujadiliana HAYO matatizo kwa lengo la kuyamaliza likishindikana siwezi kamwe kukaa nyumbani. Ni bora nishinde kwa marafiki kuliko kuwahi kurudi nyumbani kukutana na ugomvi wa kipuuzi.

Kwa sehemu, kuna ukweli kuwa wadada (baadhi) huwa wana hulka ya kuanzisha ugomvi ambao ukiuchunguza kwa undani sana, hauna tija. Kwa hili wadada WENYE TABIA HIZI mjirekebishe!

Na kwa kusema hivi, hakuna uhusiano wa ugomvi moja na ni tafsiri batili sana, kufananisha urafiki wa namna na mapenzi ya jinsia moja. Please rekebisha mada yako!
 
Back
Top Bottom