Majs
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 229
- 485
WANAUME 20 walio kwenye ndoa katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa wamevunja ukimya wakidai kupigwa na kutelekezwa na wenzi wao, imebainika.
Mkuu wa Dawati la Polisi la Jinsia na Watoto Sumbawanga, Koplo Germana Mfwomi alilieleza gazeti hili kuwepo kwa hali hiyo, mbali na kubainishwa kwenye uzinduzi wa mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia Manispaa ya Sumbawanga mkoa wa Rukwa uliofanyika jana mjini hapa.Inasemekana kuwa wanaume 15 wamevunja ukimya mbele ya dawati la polisi la jinsia na watoto Sumbawanga huku watano wakikiri mbele ya maofisa wa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Sumbawanga.
Akifafanua, Germana alidai wanaume watatu ndio waliokwenda kwa hiyari yao wenyewe na kulalamika mbele ya dawati la polisi la jinsia na watoto mjini Sumbawanga kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na wenza wao wa ndoa ikiwa ni pamoja na kupigwa mara kwa mara na wametelekezwa na wake zao.
Ofisa Ustawi wa Jamii, Manispaa ya Sumbawanga , Herry Sanga alieleza kuwa wanaume watano wenye umri zaidi ya miaka 30 wamekiri kupigwa na wenza wao wa ndoa huku akisisitiza kuwa idadi hiyo inaweza kuwa kubwa kwa kuwa wengi wao wanaona aibu kuvunja ukimya .
Mkurugenzi wa mradi huo, Mchungaji wa Kanisa la Moravian, Peter Kawageme alisema kuwa mradi huo utatekelezwa katika kata zote 19 zilizopo katika Manispaa ya Sumbawanga ambapo katika awamu ya kwanza utatekelezwa katika kata kumi kwa kipindi cha miezi sita kwa gharama ya zaidi ya Sh milioni 60.