Wanaume watolewa hofu kutumika kidole kupima tezi dume

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,409
20,759
tezi+dume+pic.jpg

Dk Mwaiselage amesema baada ya upimaji huo majibu atakayoyapata mpimwaji itategemea kama ana dalili za tezi dume au hana, iwapo hana dalili atapewa ushauri arudi baada ya miaka miwili, na kama anazo zikionekana atakwenda katika vipimo vya ziada lakini havihusiani kidole kwani navyo pia vinahusisha damu.

Dar es Salaam. Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) imesema upimwaji wa saratani ya tezi dume kituoni hapo hufanyika kwa njia ya damu na si kwa kidole kama ilivyozoeleka.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Ijumaa kuhusu matembezi ya kuhamasisha uchunguzi wa mapema wa saratani ya matiti yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi asubuhi, mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo, Dk Julius Mwaiselage amesema kipimo hicho hutumika kwa vipindi vya hatua zote za uchunguzi.

Amesema huo ni mwongozo ambao umewekwa kupitia wizara ya afya na hospitali zote zinaufuata mwongozo .

“Upimaji huu unafanyika katika hatua za uchunguzi kupitia damu, mwanaume yule ambaye anatakiwa kufanyiwa uchunguzi huo anafika katika hospitali au kituo husika na anapimwa kwanza kwa kutumia damu kama ilivyo kwa HIV na Malaria,” amesema.

“Mpaka kufikia hatua za juu zaidi za vipimo ambavyo sasa itathibitika kwamba ni tezi dume, ataendelea na vipimo zaidi vikiwemo vya radiolojia, huu upotoshaji wa kwenye mitandao unalenga kutisha watu kutokana na maadili yetu tunashtuka, kwa hatua za juu ni suala la mgonjwa na daktari,” amesema.

Mwananchi
 
Labda awe daktari Mwanamke ndiyo nitakubali kupima lakini sio daktari mwanaume mwenzangu anitie kidole kwenye mk.undu wangu, mimi mwenyewe sijawahi kuuona mku.ndu wangu iweje nimwachie mwanaume mwenzangu aone mkun.du wangu
 
Upo sahihi ni vema kukataa maana laiti ukiruhusu daktari nae kama

ni mpenda sifa ....atakukagua kwa muda mreeefu kweli ...akishika

angle zote ...rinda lazima lisheki
 
mbona kule kwenye mambo yetu mkipelekewa ulimi down mnajiachia tu...
 
Hebu mkapimwe
sio kwa aina ile ya upimaji... yaani serious mzee mzima anainama halafu unaona njemba inavaa gloves then inajipaka lubricant! Hata kama unaroho ngumu lazima utatoka nduki mkuu. Hii ya kupima damu wanataka kumix watu tuu.
 
Bora maana upimaji wa dole haufai ni bora tezi lije tu kuliko kupigwa finga

Sasa ntaenda kupima
 
Hapo namimi nitapima, nilisha amua bora nife kuliko kunitoboa na kidole
 
sio kwa aina ile ya upimaji... yaani serious mzee mzima anainama halafu unaona njemba inavaa gloves then inajipaka lubricant! Hata kama unaroho ngumu lazima utatoka nduki mkuu. Hii ya kupima damu wanataka kumix watu tuu.
kwani ukipimwa unakufa
 
tezi+dume+pic.jpg

Dar es Salaam. Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) imesema upimwaji wa saratani ya tezi dume kituoni hapo hufanyika kwa njia ya damu na si kwa kidole kama ilivyozoeleka.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Ijumaa kuhusu matembezi ya kuhamasisha uchunguzi wa mapema wa saratani ya matiti yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi asubuhi, mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo, Dk Julius Mwaiselage amesema kipimo hicho hutumika kwa vipindi vya hatua zote za uchunguzi.

Amesema huo ni mwongozo ambao umewekwa kupitia wizara ya afya na hospitali zote zinaufuata mwongozo .

“Upimaji huu unafanyika katika hatua za uchunguzi kupitia damu, mwanaume yule ambaye anatakiwa kufanyiwa uchunguzi huo anafika katika hospitali au kituo husika na anapimwa kwanza kwa kutumia damu kama ilivyo kwa HIV na Malaria,” amesema.

Dk Mwaiselage amesema baada ya upimaji huo majibu atakayoyapata mpimwaji itategemea kama ana dalili za tezi dume au hana, iwapo hana dalili atapewa ushauri arudi baada ya miaka miwili, na kama anazo zikionekana atakwenda katika vipimo vya ziada lakini havihusiani kidole kwani navyo pia vinahusisha damu.

“Mpaka kufikia hatua za juu zaidi za vipimo ambavyo sasa itathibitika kwamba ni tezi dume, ataendelea na vipimo zaidi vikiwemo vya radiolojia, huu upotoshaji wa kwenye mitandao unalenga kutisha watu kutokana na maadili yetu tunashtuka, kwa hatua za juu ni suala la mgonjwa na daktari,” amesema.

-Mwananchi
 
Daaah - Daktari amenikatisha kiu yangu - nilikuwa nataka nikajitolee (ku-volunteer) hii kazi ya kupima watu kwa kidole. Niweze kuwapima watu wengi iwezekanavyo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom