Wanaume wasiokuwa na hela wana lawama na gubu sana kwenye mahusiano

GRAMAA

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,155
3,399
Kama wewe mdada ulishawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi au kwenye ndoa kabisa na mwanaume asiye na hela nadhani utakubariana na mimi kwamba watu hawa wanalawama na gubu sana.

Kibaya zaidi mwanamke awe na hela alafu mwanaume asiwe na hela hapo lazima mwanamke uwe na moyo wa chuma vinginevyo utakonda.

Mwanamke asifanye kosa kwa bahati mbaya utasikia njemba inasema, "Najua unakiburi kwakuwa mimi sina hela ndiyo maana huniheshimu sawa haina shida ila kumbuka hela zinatafutwa ipo siku na mimi nitapata tu". " pia nashukuru kwa dharau zako na ninajua pia unanisimangia chakula chako"

Kosa si kosa mwanaume atasusa kula siku nzima, atasusa kuoga na kununa juu. Masikini mke atakuwa na kazi ya ziada ya kulibembeleza jitu zima lile na likaoge.

Mwanaume asiye na hela kununa na kususa susa hovyo ndani ya nyumba kwake ni kawaida tu. Na uhisi muda wote anadharauliwa tu.

Ikatokea mmegombana basi yeye ataingiza hata na mambo yasiyokuwepo na yasiyo husiana na ugomvi huo kabisa. Utasikia "Najua unanisimangia chakula chako, najua kiburi chako kinatoka wapi na pia najua dharau zoote hizi zinakuja kwakuwa umeniona mimi sina kazi, sawa nashukuru mama ila Mungu ndiye mtoa riziki. Ipo siku na mimi nitapata tu"

Wanaume tutafute hela ili tuondokane na mambo ya lawama na gubu za ajabu.
 
At the end you have only yourself. Love and care others bu usisahau kujipenda na kujijali mwenyewe coz watu wanaopenda na kujali wengine wao hua hawarudishiwi yale wanayoyafanya.
 
Unaweza kua sahihi,ila mwanamke akapata hela dharau hakosi mkuu,sema mapungufu ya ki binadamu pia yapo.

macson
 
MAGALLAH R,

Uko sahihi ila ktk nyumba/mahusiano kunakua na mambo mengi ana , automatically wanamke % nyingi duniani hawawez kuvumilia mume asie na pesa na hali yeye anazo ,hvyo vimasimango huwa vipo sana ,japo wanawake wengine hufanya hvyo ili kummotivate mwanaume aongeze bidii kutafuta pesa,na #wanawake mkumbuke kuwa kila mja na Rizki yake hvyo huwezi kumforce akatafute pesa nyingi ili aonekane ana pesa coz anaweza kwenda kuiba,kudhulumu au kufanya lolote baya ili akuridhishe lkn mwisho wa siku fedha aliyonayo sio halali yake,

Point to note:
Kuwe na muda wa kuvumiliana .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom