Wanaume wanazama Pangoni na Wanawake Wana bounce kama Mawimbi

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,508
6,479
Habar Wana Jf.

Kabla sijaanza haya maudhui ngoja nimalizie kiporo katika Uzi wangu uliopita.

Je zawadi ina pata point ngapi Kwa wanawake? Ukweli ni kwamba Kwa kila zawadi anayopewa mwanamke iwe kubwa au mdogo basi ujue zote zinapata point moja,ukimpa gari utapata moja na atayetoa Maua ridi atapa point moja. Kwahiyo bro usije ukajiona umemaliza Kwa kumpa mwanamke gari then ukakunja nne kana kwamba hapo mwanamke wako hachomoi tena! No kama unafikir hivyo basi ujue huwajui hawa viumbe.

Ndio maana si ajabu unakuta Mzee umehonga ndinga hlf kuna bwege mmoja huwa anatoa Toa chocolate halafu anakula mzigo kiulaini, wewe umetoa ndinga moja umepata point moja,na mwenzio kapeleka chocolate mara Saba kapata point Saba,hapo Nani mshindi? Najoa unatoa macho kama hunielewi hivi,endelea tu kutonielewa Ila utakuja kunielewa baadae.

Kwahiyo inashauriwa badala ya kufokasi katika kutoa mazawadi makubwakubwa ni Bora ukatoa zawadi ndogo ndogo mara nyingi zaidi ili upewe thamani na mwanamke wako.

Je mwanamke akikwambia baadhi ya matatizo yake anatarajia nini? Ni Kawaida wanawake kupenda kushare changamoto zao mbali mbali kwasababu mwanamke ili apate nafuu na kifua chake kiwe chepesi basi ni muhimu kwake kutoa Yale yaliyo Moyoni yasikilizwe na mtu mwingine au watu wengine, kwahiyo mwanamke akija home kwako wewe mwanaume,labda anakueleza changamoto zake za kazini,anachotaka kutoka kwako ni wewe kumsikiliza Tu basi labda kama yeye mwenyewe stake msaada kutoka kwako,kitendo cha wewe kutoa solution kwa kusema Kwa mfano ''kama kazi yenyewe inakupa shida si uache Tu kazi'' hapo ujue unafeli bro! Hataki solution toka kwako Bali anataka umsikilize Tu,na ukifanikiwa kumsikiliza Tu basi anapata faraja Sana.

Haya chukua pop con,kama mnywaji wa kahawa weka mambo Sawa tuishi na mada ya Leo!

Wanawake mtambue kuwa wanaume wanapokuwa wamevurugwa na mambo yao au kuwa na mambo ambayo yanawashughulisha huhitaji kuingia ndani ya cave/Pangoni ili wapate kutulia na kufikiria namna ya kutatua changamoto zao,haimaanishi wanaenda Pangoni kiuhalisia Ila wanahitaji kuwa pekee Yao Kwa kipindi Fulani, kwahiyo mwanamke ukiona Hali kama hii,usipaniki na kutaka kumuuliza boy wako ''mbona hupigi Stori na Mimi tena, mbona unaonekana kama haupo kawaida nini tatizo'' na mambo kama hayo,San Sana mwanaume atakwambia nipo Sawa mke wangu wala usijali, so akishakwambia hivyo basi usiendelee kumgasi gasi mpe nafasi atatue changamoto zake akimaliza atarudi katika Hali yake ya kawaid,hapo sasa ukimuona yupo normal waeza muuliza nini lilikuwa tatizo,akiwa willing kukwambia Sawa asipotaka usipanic,jua ndio hulka za wanaume zilivyo, lakini wanawake wengi Kwa kutojua hili huanza kuwa wasumbufu na kutoa maneno kibao,'' naona hunipendi mbona huniambii nini kinakusumbua''? Mwanamke tambua kuwa mwanaume si Sawa na mwanamke katika kudili na mambo yake,wakati nyinyi mnapenda kushare mambo yenu basi wanaume hawako hivyo.

Wanaume nanyi tambueni kuwa Kwa kipindi Fulani Fulani huenda ikawa hata Kwa mwezi mara moja,mwanamke huwa ana bounce kama Mawimbi sometime anakuwa high na sometime low. Anapokuwa high ina maana anakuwa ktk full mood kila kitu kinaenda Sawa,mawasiliano mazuri,maelewano fresh na vitu kama hivyo. Na kinyume chake anapokuwa low basi ujue anakuwa hayupo katika mood nzuri,utamkuta kisirani kingi,huenda mawasiliano yasiwe mazuri na vitu kama hivyo, sio kwamba wanafanya makusudi ni asili Yao kutokana na maumbile Yao,na wakati mwingine anaenda sambamba na mzungo WA vipindi vyao vya kila mwezi,kwahiyo wanaume mkiona mazingira kama haya msipaniki Sana mjue kuwa ndio maumbile Yao na ndio walivyo,lkn muhimu ujue kutofautisha chuya na mchele,sio anakuletea jeuri kwakuwa kapata bwana mpya au ana michepuko anamtia kiburi halafu wewe ukawa bwege Tu kila siku dharau nyingi na kisirani au matusi juu hlf unadhani yupo low,no! Uwe Makini kumsoma je hapa ni mood swing au naibiwa?

Haya ni mambo ambayo watu wameyafanyia utafiti Kwa sample kubwa ya watu na kupata data hizi,ebu tafuta Kitabu Man are from Mars and Women from Venus, utakuja kunishukuri baadae kina madini Sana na ukikisoma sometime unaona kabisa kama mwandishi anaongea na wewe coz kuna mambo anakugusa kabisa kuhusiana na Maisha ya kimapenzi,kuna watu ndoa zao zilikuwa zinakufa lkn baada ya kusoma Hiki Kitabu na kujifunza wapi wanakosea na wapi PA kurekebisha wamejikuta ndoa zina nawiri na kustawi upya.

Ni hayo Tu.
 
Back
Top Bottom