Wanaume wanapojiremba kupita kiasi ina maana gani?

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165
Siku hizi, kuna ugumu wakati mwingine, kujua kama mtu ni mwanamke au ni mwanaume. Vijana na hata watu wazima wengi wanaume hujipamba sana kwa kutumia vipodozi, ambavyo kwa kawaida, vimekuwa vikitumiwa na wanawake.

Kuna wanaume wanaopaka nyuso zao dawa za kung'arisha na kupambana kabisa na ndevu. Hawa ukiwatazama nyuso zao ni kama za wanawake, kwani mwanaume mwenye uso mororo sana huonekana kama mwanamke kwa kiasi cha kutosha. Kuna wanaume wanaovaa hereni, bila hata kujua wazivae kwa namna gani.

Uvaaji wa hereni kwa wanaume, ambapo inasemekana ulianzia kule Marekani, ulikuwa ukifanywa kwa sababu maalum na kwa namna maalum. Kwa mfano kuna waliokuwa, au wanaovaa ili kuonesha upendeleo wao kimapenzi (kwa mfano ushoga) na wengine kwa sababu mbalimbali.
Kwa kawaida mwanaume anapotoga sikio moja tu, hasa la upande wa kulia na kulivisha hereni, inamaanisha kwamba, mwanaume huyo ni shoga!

Kwabahati mbaya hapa kwetu kuna vijana ambao hutoga sikio moja la kulia na bado wanaamini kwamba, wako salama. Ukweli ni kwamba siku akikutana na raia wa Marekani wanaotafuta mashoga, hawatasita kumwita na kumtongoza. Ndio maana yake, kwani nyie mlidhani vipi?

Kwa kawaida wanaume wamekuwa wakikataa kuvaa mapambo na kujipodoa kama wanawake katika kuonesha kwamba, mwili wao hauhitaji vitu hivyo kwani ni mwili wa kazi hususan za nguvu na hivyo mapambo hayawezi kuwa na maana kwao. Ndio maana najiuliza kujipodoa na kujipamba huku kwa wanaume na kuvaa hereni na makorokoro mengine yanaashiria jambo gani?
 
Mimi wananiudhi sana wanaume wanaojipodoa, kuna vitu wanapaka siku kama Nape, sijui wanaita Calolite.
Mwanaume anatakiwa tu kuwa smart, kujipaka mafuta mazuri, pafym. sio mkorogo
 
Yaani hao wapo sana,siku hizi ndo mtindo wa wanaume wengi
labda wameona wanawake wanafaidi
umesahau rangi za kung'alisha midomo
al maarufu LIPSHINER
 
Kumbe siko mwenyewe ninae washaangaa!Jamani hii hali kwakweli inatisha yani kuna kamkaka pale mtaani wetu kamejichubua kana vaa hereni alafu miguu mweus the kanajiitakidume,kwakweli nakachikia hana nikimuona sipendi kumwangalia mara mbili,sasa nashindwa kuelewa ni kutafuta kupendeza au ni kutofahamu wakifanyacho!kwenye daladala unakuta mkaka lips zinag'aa yani kapika poda kanoga katuzidi mpaka wadada jamani,sijui kifuatacho miaka ijayo!
 
yaani utakuta sharo mwingine sijui kavaaa nusu **** naye anaonyeshakiuno sijui sh..ng*
mi kwa kwlei siwaelewi utakuta mt kajipodoa aaaaaaaa
 
tunakoenda ndiko siko kwani kila mmoja anaibuka na yake
 
Tatizo Umagharibi unatumaliza.
Tuna kasumba ya kuona kila kinachofanywa na ngozi nyeupe ni sahihi.
Tunaiga bila kutafakari. Kama Taifa Tunahitaji mabadiliko makubwa ya kimaadili.
 
kwa kweli hata mie nimekuwa nikijiuliza sana kwamba hawa wakaka wanaojipodoa kama madada wanamaana gani? Ni kutafuta uzur? Au ni mawakala wa tgo?.kiukweli sipendi kabsa tabia hii, nina mdogo wangu wa kiume alianza kujipodoa nikampiga stop na amenielewa nikaja kugundua alikuwa anaiga
 
Mimi wananiudhi sana wanaume wanaojipodoa, kuna vitu wanapaka siku kama Nape, sijui wanaita Calolite.
Mwanaume anatakiwa tu kuwa smart, kujipaka mafuta mazuri, pafym. sio mkorogo

Hivi hiyo ndio nini?? nasikia tu wasanii wanajisifia kwa kutumia hiyo kitu..
 
Yaani hao wapo sana,siku hizi ndo mtindo wa wanaume wengi
labda wameona wanawake wanafaidi
umesahau rangi za kung'alisha midomo
al maarufu LIPSHINER
Lipshiner ni ya Ke na lipcare ni ya Me. Watu wengi wakiona Me anatumia lipcare wanadhani anatumia lipshiner kwa sababu container zake zinafanana kidogo!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom