Wanaume Wanaowasaidia Wake Zao Kazi za Nyumbani Ndoa Zao Hudumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume Wanaowasaidia Wake Zao Kazi za Nyumbani Ndoa Zao Hudumu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, May 22, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Wanaume Wanaowasaidia Wake Zao Kazi za Nyumbani Ndoa Zao Hudumu
  [​IMG]
  Utafiti umeonyesha kuwa wanaume wanaowasaidia wake zao kazi za nyumbani ndoa zao hudumu Friday, May 21, 2010 2:52 AM
  Wanaume ambao huwasaidia wake zao kazi mbalimbali za nyumbani kama vile kupika, kuosha vyombo na kuwaogesha watoto, ndoa zao hudumu muda mrefu kulinganisha na wale wanaosubiria kufanyiwa kila kitu na wake zao. Utafiti uliofanywa na watafiti wa chuo cha London School of Economics (LSE) cha Uingereza umeonyesha kuwa wanaume wanaowasaidia wake zao kazi za nyumbani ndoa zao hudumu muda mrefu kulinganisha na wanaume ambao hawependi kuwasaidia kazi za nyumbani wake zao.

  Utafiti huo ulisema kuwa ndoa ambazo mke na mume wote wanafanya kazi huwa katika hatari kubwa ya kuvunjika iwapo mume hamsaidii mkewe kazi za nyumbani.

  Utafiti huo uliopewa jina la "Men's Unpaid Work and Divorce" ulihusisha familia 3500 za Uingereza.

  Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuwa wanaume ambao waliwasaidia wake zao kazi za nyumbani kama vile kwenda sokoni, kuosha vyombo, kupika na kuwaangalia watoto ndoa zao zilionyesha kuwa imara zaidi.

  Hata hivyo utafiti huo ulisema kuwa ndoa za watu wa zamani zilidumu sana kwa kuwa mke alikuwa hafanyi kazi akijishughulisha na kazi za nyumbani pekee wakati mume alifanya kazi kutafuta chakula kwaajili ya familia.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Si ndo mwanzo wa kuitwa bushoke!
   
 3. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sio kweli ukimsaidia mke wako utakuwa Bushoke, kamanda Ndiba vipi bwana, huo ni ugentleman bana, we jaribu siku moja kuosha vyombo, uone penzi utakalo pewa na wife wako --lakini hii kama umeoa, am telling mtaishi vizuri sana kama mnasaidiana ndani ya nyumba
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nimefarijika sana na huo utafiti. Hizo zote nazifanya na nyingine nyingi tu! Na sasa navuta kwenda mwaka wa 10, sijaona dalili za kulimwa kibuti. Ngoja niendelee kufanya hako ka utafiti kwa tutaishia wapi.

  Huu utafiti una ukweli kwa kiwango kikubwa, ila wamesahau kuongeza kuwa na endapo mume huyo hatazungushi ki-hiace mitaani!
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hiyo ya Bushoke inahusishwa na uswahili. Sisi tuna-operate kisasa kabisa. Hakuna mzizi wala nini. Mwendo wa ratiba na kuangalia uzito wa kazi ulionao mwenzako. Mambo ya Bushoke hakuna katika hii issue!

  Kweli kabisa. Mwambie aniulize ili nimweleze, "from the Horse's mouth"! Hii kitu inapunguza stress kwa my wife na kumfanya apumue, tayari kwa dinner!
   
 6. JM Aristotle

  JM Aristotle Senior Member

  #6
  May 22, 2010
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli haya yote ni kweli...
  Shida ni kwamba, wengi tumelelewa katika hali ya "mfumo dume", na ndo maana wengine wanafikiri kumsaidia mke ni "ubushoke"
   
 7. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  .........Huu utafiti naukubali, ni kweli kabisa mwanaume akiwa anakusaidia kazi yaani penzi ndio linazidi maana anakupunguzia mzigo wa kazi nyingi za nyumbani ambao utakufanya uchoke.
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Inawezekana ila nadhani baadhi ya wanaume wanasumbuliwa na inferiority complexes! Anahisi ataonekana Bushoke akimsaidia mke wake wakati ofisini anawabebea wakubwa zake mafaili hadi chai!
   
 9. m

  muhanga JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  vitu vingine ni malezi zaidi
  binafsi huwa siwezi kumwambia mwanamke
  eti nitayarishie maji ya kuoga au niandalie chakula.....

  mimi nimezoea ukiwa na njaa unaingia jikoni na kujipakulia
  mwenyewe,na kuoga kama maji hakuna bafuni unakwenda
  mwenyewe kutafuta yalipo na kuoga....
  sijabadilika,nipo hivyo hivyo still
   
 11. m

  muhanga JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  congrats bro thats gentlemanly behaviour.:thumb:
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mimi sioni kama ni suala la kuwa gentleman au la. Ni suala la kuwa responsible. Utasubirije kuletewa maji bafuni wakati mtu unayetaka akuletee maji ana kazi nyingine na wewe uko tu uanaangalia movie? Au utamwambiaje mwenzako akuipakulie chakula wakati yuko anaogesha watoto au kuwatandikia kitanda? Ni upuuzi wa hali ya juu mwanamume kujaribu kumfanya mke wake kijakazi.
   
 13. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  for the first time kuona wanaume wanaongea lililo jema hivi!!(maana wako very few wenye mtizamo chanya juu ya mwanamke)
  kweli jamii yetu ya sasa inaanza kuamka na kuona mwanamke ni binadamu/mtu
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kweli, inawezekana ni mara yako ya kwanza.
  Aza
  [​IMG] Senior Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Join Date Tue Feb 2010
  Location uvungu
  Posts 153
  Thanks : 306
  Thanked 26 Times in 22 Posts
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Really?????????
   
 16. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Hongereni wakina baba munaoona umuhimu wa kuwasaidia wake zenu katika shughuli mbali mbali za nyumbani. Ni kweli kabisa nyumba inakuwa na furaha na upendo na watoto wote wanaona kufanya kazi ni jukumu lao kwa vile baba na mama nao wanasaidiana.

  Tatizo kubwa ninaloona ni mama mkwe au mawifi wakija hapo nyumbani na kuona mtoto/kaka yao anafanya kazi kusaidiana na mkewe - heeeee itakuwa nongwa na maneno tele tele.

  Ila mukiwa na msimamo basi mambo yanakuwa poa, lakini pagumu hapo hasa anapokuwepo mama mkwe nyumbani.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  ıuǝnɥɐ ǝʇɐdıu ɐʞɐdɯ ıɹıqnsɐʇıʞ ısɐq ɐʎuɐɟıʞnʞ ɐzǝʍoʇnʞ ɐɥɔ ısɐıʞ ɐʍɾuoƃɯ ıu ɐɯɐʞ ɐu ɐʍɾuoƃɯ ɐʍıʞıu ɐʇɐɥ ǝןıʞ ǝʇoɥɔoɥɔ ɐʍıʎuɐɟnʞ ıpuǝdıs ǝdʎʇ ǝɯɐs ǝɥʇ ɟo ɯɐ ı 'ssoq noʎ ɥʇıʍ ʎʇıɹɐןıɯıs ɹǝɥʇouɐ ¡ssoq noʎ ʞuɐɥʇ
   
Loading...