Wanaume Waliooana Malawi Waachiwa Huru Baada ya Wafadhili Kupiga Mkwara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume Waliooana Malawi Waachiwa Huru Baada ya Wafadhili Kupiga Mkwara

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, May 30, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Steven Monjeza kulia na mkewe Tiwonge Chimbalanga
  Wanaume wawili waliooana nchini Malawi ambao walitupwa jela miaka 14 wiki iliyopita kwa kuvunja sheria na kukiuka maadili ya kiafrika wameachiwa huru baada ya Malawi kuelemewa na shinikizo kubwa la mataifa wafadhili. Baada ya shinikizo kubwa toka nchi za magharibi, serikali ya Malawi imerudi nyuma katika harakati zake za kupambana na tabia ya ushoga na usagaji kwa kuwaachia huru wanaume wawili waliooana ambao walitupwa jela miaka 14 hivi karibuni.

  Steven Monjeza, 26, na "Mkewe" Tiwonge Chimbalanga, 20, walitupwa jela miaka 14 wiki iliyopita baada ya kufunga ndoa na kufanya sherehe iliyohudhuriwa na watu 500.

  Mataifa ya magharibi yakidai yanatetea haki za binadamu yalipinga kufungwa kwa Monjeza na mwenzake yakisema kuwa Monjeza na mwenzake hawajafanya kosa lolote zaidi ya kupendana kama wanavyopendana watu wengine.

  Serikali ya Uingereza ililaani hukumu iliyotolewa dhidi ya Monjeza na mwenzake ikisema kuwa Malawi imekiuka misingi ya haki za binadamu.

  Uingereza ambayo ndiyo mfadhili mkubwa wa Malawi, ilisema kuwa inajadili upya msaada wa paundi milioni 80 ambao Malawi hupewa kila mwaka.

  Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika, akiongea na waandishi wa habari leo akiwa pamoja na katibu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, aliagiza Monjeza na mkewe waachiwe huru mara moja.

  "Hawa vijana wamefanya kosa dhidi ya utamaduni wetu, dini yetu na sheria zetu lakini hata hivyo nikiwa kama mkuu wa nchi nimewapa msamaha na ninaagiza waachiwe huru bila masharti yoyote", alisema rais Bingu wa Mutharika.

  Naye katibu wa Umoja wa Mataifa ambaye alikuwepo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika ikulu, alimpongeza rais Bingu wa Mutharika kwa uamuzi wake wa kishujaa wa kulinda haki za binadamu na kuwaachia huru mashoga hao wawili.


  Hizi sheria za Kiafrika ni Pesa tu ukiwa na pesa sheria inakuwa ni yako hakuna wa kuogopwa Kasheshe kweli.
   
 2. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nilisema hawajafanya kosa, sasa mnaona???? haki imetendeka!!! Tangu lini Afrika ikawa na Uhuru wakati wanategemea MISAADA??????? TEHE TEHE TEHE....eti nini??....."miaka 14 ndani na kazi ngumu!"
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Karibuni uraiani mhh namuona mke kavaa khanga mweeehhh!!!
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Maria Roza
  umemjuaje kuwa huyo ndio bwabwa
   
 5. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mhh sura zao hata hazijifichi:rolleyez:
   
 6. F

  Fernandes Rodri JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2010
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 407
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Uchumi ndio unatawala kila kitu ,Hata kwako kama huna kitu mwenzi wako anakuona **** :painkiller:
   
 7. P

  Paul S.S Verified User

  #7
  May 31, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu imekufurahisha sana hii, ukweli ni kuwa kosa walifanya kwa mujibu wa sheria za malawi, na haki ilitendeka kwa mujibu wa sheria za malawi. sema umasikini wa nchi zetu ndio unaofanya watu wa magharibi kutumia pesa zao kutu lazimisha kuamini kila chakwao basi ni sahihi, nashindwa kupata picha inakuwaje unashabikia namnahii ninyi ndio wale mnaoamini na kupractice kila kinacho fanywa na magharibi
   
 8. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  dawa ni kuwatumia majasusi wawaue.
  sipendi kabisa tabia hizi za ajabu ambazo hata ng'ombe hawafanyi
   
 9. P

  Paul S.S Verified User

  #9
  May 31, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Swali ni kuwa je wataachiwa waendelee na maujinga yao ya harusi, maana wameachiwa bila masharti yoyote
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Tizama vizuri!

   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ndiyo uzuri wa kuiamini qurani kwenye kesi kama hizi, naona hawa watakuwa wametengenea eti jamani?
  qurani imeruhusu waume wakiendeana kinyume na maumbile, waadhibiwe kisha wakitubia waachiwe huru,

  hata hivyo nchi nyingi sana duniani watu wanafanya ufirauni, kwa kuwa sheria za Mungu aliyehai watu wamezikinai na kuzifuata sheria za miungu mfu, mfano huko Yemeni, Oman, Komoro, Marekani hata hapa kwetu Tanzania ni aibu
   
 12. crome20

  crome20 JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 831
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Yule ''mwanamke'' angechunguzwa kitaalamu kujua kama homones alizonazo zinaweza kuwa zimemsukuma kufanya hivyo au ni upumbavu tu wa kuiga. Na kama ni hivyo wafungwe tu na Malawi imetia doa Afrika kwa kushindwa kutekeleza sheria walizijitungia wenyewe.Je hiyo sheria ina haja ya kuwepo kwenye vitabu vyao??
   
 13. K

  Kekuye Senior Member

  #13
  May 31, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili swala la 'haki za binadamu' ninaona linaelekea kuzifanya nchi za dunia ya tatu kutawaliwa na mataifa bepari hata kuingilia sheria za nchi husika. Bila kuwa na mipaka na kuisimamia kulingana na sheria za nchi husika sidhani kama tutafika mbali. Kweli mambo mengine pamoja na kuwa yanachukuliwa kama ni haki za binadamu yanatutoa utu na kwa desturi za nchi zinazoendelea hayakubaliki.
   
 14. k

  kaiya Member

  #14
  May 31, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Spin as usual, hivi malawi inaongozwa na sheria za qurani!!
   
 15. P

  Percival JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Sheria ya Qurani ? - wangeisha kula mawe hao hata Ban ki Moon angefika hawapo tena. Ngojeni mpaka wote mfanywe mashoga hao wamagharibi hata mapadri wanaruhusiwa kuwa mashoga - mwisho wa dunia umefika - Walivyokuja kwanza wazungu ni kueneza dini, kisha ukafuatia ukoloni na sasa ni kampeni ya kuwafanya waafrika mashoga au hawapewi ugali - My GOD FORBID
   
 16. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #16
  Jun 1, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama kweli dunia inalelekea pabaya, tuombe Mungu atuonyeshe Kweli ili kwayo tuwe huru.
   
 17. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,018
  Trophy Points: 280
  Asisingiziwe mungu hapa hili lakwenu na liko ndani ya uwezo wenu, maendeleo yamewashinda kuiga sasa watoto wenu wanaamua kuwa michicha hivi hivi. Manake ulaya mabwabwa yako na franga lakini wajomba pichani manake kama hawatoki kwetu mbagala labda kwa mtogole.

  Ukiangalia mwenendo wa maisha ya sasa na mijadala mingi ya wabongo basi kuna kila dalili tutawapata wengi hapa bongo hivi punde. Ukiona watu wanapoteza muda mwingi kujadili watu binafsi na maisha yao basi hujue hormoni za kiume zinawapungua wanaume.
   
 18. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hebu tupe kwanza research yako umeifanyaje kwanza
   
 19. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yaaani hapa sijaelewa tunapata fundisho gani katika hili kuwa haya mambo hayana tatizo tena baada hawa majamaa kuonyesha njia
  na sijajua sasa hawa wametenganishwa au ndio sasa mahaba yaanza ?
   
 20. g

  gutierez JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 1,254
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  ndio tatizo la nchi zetu za kiafrika nyingi,zinapenda siasa kutekeleza shida,sasa kama wao waliona ndio sheria yao mbona wameshindwa kutekeleza,sababu utasikia umaskini,ndio tatizo letu,tunapanga kitu tukipigiwa mkwara hatupewi misaada tayari tunalegeza,mimi nawasifu waarabu hawayumbishwi mtu akiamua anaamua kweli bora afe maskini lakini katimiza lengo lake,afrika sisi bado sana siasa nyingi ndio mana tutaendelea kuwa chini ya wenzetu nyanja zote kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni hatuwezi kujiongoza wenyewe kifikra,kiuchumi,kiutamaduni na kisiasa sababu kubwa ni umaskini na pia ubinafsi uliwepo ktk viongozi wetu,viongozi wetu wengi bado giza tu wana elimu za kushika kalamu tu na kuthamini mwenye pesa ila kujiamulia maamuzi yao binafsi na kuweza kuvumbua mawazo yao kiasi yakajenga nguvu bado hatuna,ndio unakuta ktk kesi hii wakiulizwa kwanini wanapinga ndoa ya jinsia 1 wameshindwa kujitetea kwa hoja pointi zao kiasi kuwaona hata magharibi wakubaliane nao,wao wataongelea sana kidini na kimila sasa hiyo sio point ya kuridhisha mana Malawi kuna dini za aina nyingi wapagani,wakristu na waislamu kwahiyo inakuwa haileti mana wakiingiza ktk udini,ukienda kitamaduni wengine sasa hawafuati watu wanazaliwa hospitali wengi wao siku hizi tofauti na enzi zile wanazaliwa majumbani na wakunga wa kienyeji,wito wangu viongozi wa nchi zetu za dunia ya tatu wanapokuwa wanawasilisha sheria zao ktk mahakama ya kimataifa wawe na sababu za kutosha na za msingi kutetea hoja zao la sivyo itakuwa hauna point kumridhisha upande wa pili ukubaliane na wewe,ukiwa na pointi watakuelewa mana wanakuambia hekima ni bora kuliko dhahabu na fedha watakunyonga ila haki yako watakupa,zaidi ya hapo tutazidi kuwa wanasiasa vitendo hakuna na kuwa watumwa wa pesa na mali tu kutokana na umaskini wetu!
   
Loading...