Wanaume Walio Uchi Wanapoisaka ‘Fimbo Ya Bahati’!

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,435
1-26.jpg






MAELFU ya wanaume waliokuwa nusu uchi na waliovalia vinguo vyeupe vinavyoanzia kiunoni, venye kuficha tupu zao kwa mbele na kuyaacha makalio wazi, hivi karibuni walishiriki tamasha maalum la kutafuta fimbo zilikuwa zimerushwa katika umati wa watu.


Wale waliopata fimbo zenye urefu wa sentimita 20, ambazo zinaitwa “shingi”, wanaaminika kuwa ndiyo wanaume wenye bahati zaidi mwaka huu (2019).




2-17.jpg
3-15.jpg






Maadhimisho haya yalikuwa ya 510 katika historia ya Japan ambapo maelfu ya washiriki huoga maji ya baridi katika mto Yoshii ili kutakaswa kabla hawajaanza kutafuta fimbo ya bahati. Mara baada ya kumaliza kuoga maji hayo baridi, taa huwasha.





4-12.jpg
5-11.jpg






Mkuu wa sehemu hiyo ya kuabudia husimama juu katika jukwaa la mita nne na kurusha fimbo hizo mbili katika mkusanyiko mkubwa wa watu. Watu wawili watakaoweza kuzipata fimbo hizo hutajwa kuwa washindi wenye bahati.





6-10.jpg
7-10.jpg






Tamasha la ‘Saidaiji-eye’ ni miongoni mwa matamasha makubwa katika tamaduni za Japan katika kalenda ya mwaka. Vilevile tamasha hili linafikiriwa kuwa linaleta mazao mazuri katika mwaka.
 
na sisi huku kibongo bongo wangerusha vipande vya vyuma ktk umati wa watu ili kwa mtu atakayeokota chuma, awe shujaa wa huu mwaka yaan aupite salama pasipo vyuma kukaza, kwa jinsi vyuma vinavyokazana ila yeye awe hodari mwaka 2019 aupite bila kuwa na kesi ya deni lolote..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom