Wanaume wa ukweli wanaojua majukumu yao na waletao mabadiliko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume wa ukweli wanaojua majukumu yao na waletao mabadiliko

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MKATA KIU, Mar 12, 2012.

 1. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,167
  Likes Received: 966
  Trophy Points: 280
  Wanaume wa ukweli waletao mabadiliko na wanaojua majukumuyao ( Career)
  Heshima kwenu Brothers and sisters na wadau wote wa jamiiforums
  Wekend hii Jumamosi nilikuwa Napata kinywaji na classmates,workmates na washkaji wengine huku tunacheki mpira Maeneo ya Break point Makumbusho, Kama mnavyojua Bar mnakutana na watu wengi msio juana kabla, but kinywaji na story za mpira zinawaunganisha na mnakuwa kama mmekuja pamoja
  Na mnajuana toka kitambo, Baada ya kupata drinks huku mpir aukielekea mwishoni jamaa yangu mmoja
  Alipigiwa simu na mke wake akimuomba hela ili achangie harusi ya shost wake so alimuuliza atoe ahadi ya bei gani, so kutokana na kelele za bar nakuona hawasikilizani vizuri jamaa ilibidi aweke loud speaker ili amsikie vizurihapo ndipo karibu wote meza ile tulisikia maongezi yao, Jamaa akaanza kumfokea wife
  Wake kwamba ana hela kwa nini anamsumbua wakati anajua maisha magumu, ikabidi yule dada(wife) akate simu, hii iligusa sana wadau nakusababisha jamaa mmoja kilaji kiliyekuwa kimeanza kuchanganya kuanza kuponda kuwa Wanaume wa siku hizi wamekuwa legelege especially kwenye career wanapenda kazi za kike ndo maana wana vipato vidogo na imesababisha hata wakose hela za emergence kumpa wife kama hizo ndogo alizoomba mkewe,
  akazidi kuponda kuwa Kazi ya jamaa ambaye ni Bank officer ni ya wavulana but Wanaume wanaojua majukumu na waletao mabadiliko kwenye familia zao wanapambana na umaskini kwa Career zisizo za kuvaa tai na huwezi sikia wakigombana na wake zao kisa kipato, akadai hizo kazi za kupendeza kufanga tai na kupulizia pafyumu nyingi Mwanaume wa ukweli Wanawaachia zifanywe na wake zao huku wanawapa mahitaji yote bila kuuliza mishahara yao as ziwasaidie kwa mambo yao madogomadogo kasha akaanza kulist kuwa Wanaume wa ukweli wapo
  1- Wanaume wa ukweli wapo Bandarini huko wanapangama container na other port operations like kukagua mizigo and so on as hukuhakuna hela ya mawazo na ni nadra kwa mdada kufanya hizo kazi maana ni akili plus ukakamavu

  2- Wengine wapo migodini wanasimamia operations mbali mbalizinazofanya wasivae tai wala suti mda wote wapo kwenye kadeti, reflectors na other operations dress code

  3- Wengine wameajiajiri kwenye garage zao zakuelewaka, japokuwa kaajiri mafundi but Mda mwingine anazama mzigoni kuhakikisha mabo yanakwenda sawa kama kuweka sawa magari na vitu vingi familia isipate shida, mda wote hela ndogo ndogo mama hakosi na bar wanakaa huku nyumba zikijengwa na magari yakinunuliwa

  4- Wanaume wengine Buildings contractor wapo site mda wote wanajenga nchi, na unakuta sometime wanapotea hata six months na wife halalamiki coz anajua mumewe ni Jembe na kaachiwa mahitaji yote bila tatizo na hata akiwashwa anapanda pipa anamfata husband site weekend then anarudi mjini anamuacha jamaa Site anafanaya kazi za kutengengeneza hela ya kuface majukumu

  5- Telecom installations Engineers , mida yote wapokwenye resi za kufunga na ku upgrade minara ya simu ili mimi na wewe tuchat na vi modem visome tuweze kuperuziinternet, yaani ni kusaka hela tu as one site iinstallation payment ni dolaelfu kadhaa na unakuta kidume na team yake kwa siku wanapiga kazi kusimamisha site hata 10 na zinasimama, huku wife yupo home kashapewa budget yake ya mwaka mzima kwenye account japokuwa anafanaya kazi nayeye na kidume kipo porini kinafanya kazi na wife alalamiki kijinga as he knows ameolewa na kidume

  6- Wengine wamejiajiri kwenye kampuni zao za clearing and forwarding, auditing firms na zinginevyo ambazo ni kusaka hela hakuna kucheka cheka,

  7- Wengine wanasambaza mbao na vifaa vya ujenzi,Vyakula, na vinginevyo ambavyo mvaa tai na mbeba blackberry aliyepanga sinza awezi kufanya as hajui zinatengeneza bei gani, mwisho wa siku akiombwa msaada na wife anaanza kulialia mara najenga, mara mshahara haujaingia and so on, akamalizia na military officers na wengineo kibao wanaotengeneza hela other than kuuza sura posta,

  So jamaa baada ya kuongea sana akamaliziana kumpa jamaa laki moja akampe mkewe achangie sherehe as atamdhalilisha,ataonekana anajitenga au anakaa kama hana mume wakati anae, na akadai Matatizoya ndoa nyingi yanaanzia kwenyemapato na matumizi na kuepusha hili mwanaume waukweli unapaswa upigane kwa kutengeneza kipato tofauti na mke wako as majukumuyako ya kiume ni mengi zaidi ya mkeo,

  Mwanaume wa ukweli anafanya vitu vingi kwa mara moja like kulipa ada, wife anapendeza, nyumba zinajengwa, gari zinabadilishwa bila kusingizia kitu, na emergency ikitokea kwa ndugu wanasaidiwa bila kinyongo, sio mda wote umefunga tai blazameni, mda wote kiyoyozi kwenye Opa au Gx 100 ya mkopo huku unasubiri mshahara laki kadhaa mwisho wa mwezi, hayo mambo waachie wanawake mambo ya milliom 1 kwa mwezi,mwanaume fanya biashara, au jiajiri kwenye sector your best at and make more money, usiwaze kupendeza pendeza na kumsabishia mkeo na watoto manung”uniko daily,,,, au mda wote kubishana mpira wakati haujasimama kimaisha use ur weekendto raise your income after work as a Man,, Anadai inamuuma sana kukuta dume linasoma SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE AND SO ON ,

  AKAMALIZIA KUWA WANAUME WA UKWELI UWASIKII WAKIGOMA WAONGEZEWE MISHAHARA WALA NINI AS HAWATEGEMEI MISHAHARA THAN MAKING MORE MONEY THROUGH SELF EMPLOYMENT AND WORKING HARD AND THEIR KIDS AND FAMILYHAS BETTER FUTURE while their wives works on those banks and so on, Na sio vizuri kukaa Bar huku familia haina furaha au Amani na kujisifia na kigari chako cha mkopo huku unasubiri mwisho wa mwezi kama mdada,, unatakiwa unakaa bar huku nyumbani wanacheki dstv, ada zimeshalipwa na hela umeaacha za kutosha na investment unaweka as Mwanaume wa ukweli unaejua majukumu yako

  Jamani kusema kweli nilijisikia vibaya nikaingia kwenye ki spacio changu na kuelekea nilipopanga sinza as sipo kwenye kuleta mabadiliko zaidi ya njaa tu, nikasepa huku naitazama Ford Rangers aliyokuja nayo, bila kujua aliyoendelea kuongea, Nimekumbuka now nimeona tu share if he was truth or what, but baada ya kuiliza uliza leo ofisini nikajibiwa jamaa Amejiajiri na ni Telecom subcontractor wa Tigo, ndo aliyefunga 3g internet ya tigo kanda ya kaskazini na team yake, na pia ndio wenye tenda ya ku upgrade the whole country so jamaa mara nyingi anashinda porini ndo maana mkali

  So wadau tujadiliane if his words are truth?
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  aisee....kiboko hii...
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  hebu nieleweshe
  mie bia huwa zinanitetemesha meno
  nakuwa sioni
  nashindwa kusoma

   
 4. Ishina

  Ishina Senior Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna baadhi ya mambo ambayo nakubaliana nayo (ya kujituma zaidi na kuongeza kipato cha familia) na mambo mengine si-ungi mkono. Kwa ujumla bandiko lako limekaa ki-mfumo dume zaidi, unatoa picha kwamba wanawake ni viumbe dhaifu, tegemezi na wasiojiweza (labda kama wata-wezeshwa na wa sisi wanaume). Nadhani, unge-Generalized kuwa mwanaume na mwanamke wote kwa ujumla wao wasiwe lege-lege, washirikiane na wapambane katika kuongeza pato la familia.

  Kwa ujumla hakuna kazi au courses ambazo ni maalum kwa ajili Wanawake tu, na zingine za wanaume tu! Kuna wanawake Ma-engineers na kila siku wapo site wanapiga kazi, Ma-Dkt, Builiding Contractors wapo busy kwenye ujenzi, wapo wanachacharika bandarini, madereva na makonda wa daladala na etc. :angry:
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Nina matatizo lukuki na bandiko hili. Nataka kusema ni mambo ya mazungumzo ya kilevi tu. Lakini mie siku zote huamini ulevi si excuse, kwamba mtu akikutukana halafu akasema alikutukana kwa sababu alilewa tu, ujue huyo kila siku anataka kukutukana anakuonea haya tu, na siku aliyolewa ndiyo kaondoa hiyo haya. Kwa hiyo watu wanapolewa ndipo wanapata uwezo wa kusema kile wanachofikiri na kutenda kile wanachotaka kufanya kila siku.

  Lakini pia kwa mujibu wa maelezo sioni kama watu walikuwa wamelewa, ila wanakunywa. Kwa hiyo hili linaongeza uzito kwamba "walipoteza nishai na kuongea yaliyomo kumoyo, pasipo kupotoshwa na pombe".

  1. Watu hawathamini faragha. kwa mujibu wa maelezo ya hapo juu, mume anamuweka mkewe kwenye speakerphone kujadili jambo la finances za nyumba bila hata kumuarifu mkewe kwamba anamuweka katika speakerphone.(mfumodume)

  2. Watu hawathamini haiba, hata ya kusetiri unyumba kwa muonekano tu. Mtu sio tu anamuweka mkewe kwenye speakerphone kwenye baa, bali pia anamfokea mbele ya watu baki ambao ndio kwanza kakutana nao baa.(mfumodume)

  3. Fikra potofu kwamba kazi fulani ni za wanaume na nyingine ni za wanawake (mfumodume)

  Pia inaonekana kama

  4. Mke ni tegemezi sana kwa mume (mfumodume). Mke ngangali hata mume mwenyewe hawezi kumfokea kizembe hivyo kwenye simu.

  5. Tuna habari za kujitutumua hata pale inapoonekana bajeti haziruhusu. Mpaka mtu baki anajiingiza kutoa hela kuonyesha tu kujitutumua.

  6. Tunajiingiza sana katika mambo ya watu wengine. Mtu anamwambia mkewe hawana hela wewe mtu wa pembeni unajitia kutoa fedha. Akikugeuka na kusema unajipendekeza kwa ajenda binafsi ya kuvuruga nyumba yake utasemaje?

  7. Huyo jamaa naye kama alipokea hizo fedha anye anatiliwa shaka uwezo wake wa kufikiri.

  8. Inaonekana huyo mpuuzi aliyetoa hiyo laki ana uelewa mdogo sana wa uchumi kwa kukandia watu wanaodai ongezeko la mshahara. Au ni watu fulani masikini akipata ****** hulia mbwata, new money basi anataka kila mtu amjue ana hela.

  9. Wewe mtoa mada kujisikia vibaya kwa sababu mkalamba fulani anamwaga hela ya kupiga polish viatu , au ya kumpa bartender a keep the champagne chilled unajionyesha ulivyo na low point ya kujisikia unyonge.

  10. Hiyo concept nzima ya "wanaume wa kweli" katika hiyo context ya hapo juu ni upuuzi mtupu. na huyo jamaa huenda ana upungufu fulani, hawezi kuji establish kama mwanamme wa kuheshimika bila kutumia mteremko wa spectacles kama hizi kujiridhisha kwamba na yeye "mwanamme wa kweli". Nishakutana nazo sana types kama hizi, hasa Mahenge kwenye machimbo huko, mtu anapata hela anaishia kutapanya aonekane anazo, mwezi mmoja anarudi chimboni.
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  :scared:
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  nimesoma kuanzia namba 1 mpaka 7.....huko kwingine soma wewe unieleweshe.....

   
 8. s

  sonny Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Binadamu hatulingani kwa kipato,unaposema mwanaume wa ukweli hasitegemee mshahara nakuwa nakuona kama usiekuwa na dila kwsbb kuna wengne wamesomea kazi ambazo hazina kufanya mishe nyngne tofauti na kazi yake,mf:madaktari,masektari,tv opetrators na wngne wengi wanakuwa busy sana na kazi kiasi kwamba muda wa ktoka kwenda kufanay other busnes inakuwa ngumu,so labda useme jamaa amekosea kumdis mkewe hvyo na pengne labda pombe ilikuwa ishachukua nafasi,so mwanaume wa ukweli ni yule anae jali familia yake iwe kwa mshahara au mishe zingne lakini sio kupondea watu wanao vaa tai!asante
   
 9. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  khaaa kumbe kuna wanaume na nanihiii eeeh?
   
 10. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  ni kweli kabisa.

  tena baadhi y akazi legelege za kupigwa viyoyozi kutwa zimechangia hawa baadhi ya wanaume 'kuharibika'.........

  wanaume lazima wapige mishe ufikie ile financial freedom sio unakaa kaa tu kizembe zembe utal.iwa mjini apa
   
 11. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kumbe ulikuwa haujui Smile?Wao kazi yao kubwa kufungia suruali kwenye makalio yaani mlegezo basi..eeeeh teteh
   
 12. d

  dav22 JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  du noma......
   
 13. kande kavu

  kande kavu JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aisee mwambie huyo jamaa yako wa tigo aache kunifuata fuata. Jamaa kanichana kinoma, kesho naacha hii kazi yangu ya kuchomekea mpaka leso. Mweeee!
   
 14. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  samar pliz
   
Loading...