Wanaume wa Tanzania na romance | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume wa Tanzania na romance

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ashangedere, Sep 30, 2010.

 1. A

  Ashangedere Senior Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asalaam aleykum wanajamvi, kuna jambo huwa linanitatiza saaana kuhusu ndoa nyingi (si zote) za kitanzania.
  Hivi kuenda na mke wako kwenye sherehe na kukaa nae ni kinyume cha maadili yetu???
  Kumshika mke wako mkono mbele ya watu hata kama watoto wapo ni kinyume cha maadili yetu??? au ni kuwafundisha watoto wawapende na kuwathamini wenzi wao pindi wa kiwa wakubwa???
  Kumuweka mke wako mbele kuliko marafiki na ndugu mfano: Rafiki anakuambia muende somewhere kuhave fun ukimwambia uko busy na wife ni kinyume na maadili?? kuna jambo lingine linanishangaza saaaaana, siku ya harusi tunashikana mikono kanisani, tunakula keki moja tena twalishana na mdomo, tunadance ziro distance mbele ya umati lakini baada ya hapo yote yanakuwa KINYUME NA MAADILI, hapo kanisani kila mtu anakaa upande wake, kushikana mikono kushney,kwenye sherehe kama hamjuani no kudence no romance, no what, naombeni wanaume hapa jamvini mniambie why this is happening.... Je mnajua howmuch your wives wanapenda romance??? I can assure you women love romance more than anything else, we love displaying affection kwenye public japo kwa mipaka. Plz wanaume naombeni views zenu on this.
   
 2. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mie sisubirigi afanye, nikijickia kufanya nafanya vyovyote vile ninavyojickia bila kuvunja sheria, c wangu bwana bac nipo nae free na anatakiwa nae ajibu mapigo kama hataki kec....na kweli kwenye wedding mabusu kibao ngoja leo mpo kwenye cjui party ya ofc, yupo busy na colleagues, hapo hapo na mie ndio nabana.
   
 3. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  tatizo wanaume wa kitanzania eti ukiwa bize na wife washkaji wanakwambia mwanamke anakuendesha,anyway mi kama nataka unibebe unikumbatie unikiss anywhere u must do,thats the meaning of love,love has no limitation ch muhimu ni kuangalia tu mpo katika situation gani
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nafikiri ninavyofikiria hapa sijakosea
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,053
  Trophy Points: 280
  Jamani,
  wanawake wananiboa,
  wanataka kila kitu aanze mwanaume kufanya.
  Utafikiri wao ni vipofu, viziwi, viwete, na wana ulemavu wa namna zote
   
 6. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  sema baadhi...wengine tukijickia/ hamu ya kufanya hiki au kile, tunafanya!
   
 7. A

  Ashangedere Senior Member

  #7
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  baadhi ya wanawake wanaogopa kushushuliwa kwani unakuta walishajaribu sikumoja wakashushuliwa so wanakuwa wanyonge japo wanapenda na wanaogopa kuanzisha
   
 8. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  tatizo mnapenda sana show game, wakati sisi tupo very realistic kwa mambo mengi tu!
   
 9. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ukiona hivyo ujue hakupendi ulilazimisha kuolewa. Wanawake wengi wa tz wanatabia ya kulazimisha ndoa na mtu anaweza hata kubeba mimba ili mradi aolewe so kwa kufanya hivyo unakuwa umelazimisha ndoa na ndio maana mambo kama hayo yanatokea. Kama mtu alikuoa akiwa amedhamiria na sio kulazimishwa hawezi kukushushua matokeo yake atafurahia. Na sio hilo tu hata infidelity haiishi kwa sababu ya mambo kama hayo ya kulazimisha ndoa.
   
 10. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,442
  Likes Received: 2,015
  Trophy Points: 280
  hivi vitu ni tamaduni tu unajua tofauti yetu na wazungu ni kwamba wazungu wanaonyesha mapenzi kwa vitendo kabisa kama mtu kafurahi anaonyesha kwa vitendo ila sisi waafrika tuko tofauti kutokana na tamaduni zetu utakuta mtu anampenda sana mwenzi wake lakini kuonyesha wazi anaogopa kutokana na tamaduni zetu hata kwenye harusi utakuta MC ndio anawaongoza au padre na sheikh kuwa unaweza kufunua shela na kumbusu au mchum mchum mwaaa baada ya hapo inachobaki ni wivu tu na kuulizana mbona umechelewa ulipitia wapi au mbona nimekutumia msg hujajibu yaani mapenzi yetu yanaonekana kwa wivu wivu tu na si kwa vitendo

  na siku ukijifanya kubusu busu kwenye sherehe za kikazi au harusi (zakualikwa) mkitoka hapo kama sio gazeti la udaku kuwatoa front page basi ujue ndio itakuwa discussion kwa waalikwa wote

  mapenzi ya kiafrika na kibongo yana miundo mbinu yake tofauti na sinema na movie za Marichuy, tunayaweza wenyewe
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  vunja ukimya ....

  siku ukijiskia unataka maua ......mpigie simu umwambie leo usirudi home mpaka uje na maua! yanini kujikera kwa kutaka mwanamme afahamu ile inaitwa 'ilmu lghayb' (elimu iliyojificha) ya kusoma mawazo yako?
   
 12. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2010
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Hii sredi nimeipenda, mi siku moja nimeenda kwenye arusi nakutana na mshkaji yuko na waif wake hadi arusi inaisha hawajaongea, kama vile haitoshi ilipofika muda wa msosi waifu akazuga kwenda msalani, aliporudi akaunga foleni nyuma ya hubby wake kama mtu wa tatu, sikuipenda kabisa ile. Kama vipi si wangeacha kuja tu. Ila jamaa alikuwa anautafuta ukaribubila mafanikio.
   
 13. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  No time to weste.tupobusy na hela.
   
 14. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,442
  Likes Received: 2,015
  Trophy Points: 280
  ukiona hivyo ujue hiyo ndoa ni kongwe ina miaka zaidi ya mitano, ndoa kongwe zina visa sasa si bora hao walikaa pamoja kuna nyingine unasikia mtambulishaji anasema baba mdogo na mkewe popote mlipo tunaomba msimame unakuta baba mdogo anasimama mbele ya ukumbi na mkewe anasimama upande wa pili kabisa
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  haki ya nani Funzadume wewe hamnazo, nimecheka sana, ndoa zina mambo jamani, sasa walilazimishwa kwenda huko, ingekuwa mi ni bora nisiende kabisa.
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Let it be that way and it shouldn't change
   
 17. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2010
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Ila kiukweli jamani kushikana mikono kwenye harusi au mkusanyiko wa watu ni ujasiri, unless ni katika vipindi vya kutegana (initial stages za uhusiano). Nazionaga sana chuoni kwa wenzangu wa UDSM wanakumbuka njia flani ya Yombo kuelekea Hall 4 na Hall 3 ndio mambo hayo kwa sana. Malizeni chuo afu mkutane kwenye harusi au matukio mengine na wahusika, kwa bahati wawe walioana, unakuta kimyakimya kama sio wao. Izi mambo ni noma.
   
 18. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Halafu sijui kwanini mwingine ukimshika mkono anasema anaona aibu anakwambia sipendi tushikane mikono mbele za watu, halafu baadae huyo huyo anaanza kusema ohooo sijui u dont show me love and affectionate
   
 19. A

  Ashangedere Senior Member

  #19
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usiseme hivyo kuna wanaume wanasema ukimtaka mwanamke unamfanyia chochote lakini ukishamuweka ndani ndio baasi. hapo utakuta mama ulibembelezwa ile mbaya kuolewa uliobwa na kufanyiwa yoote, lakini sasa ukimwambia nataka uwe romantic anakuambia kwani wewe si wangu tu kwani lazima nikufanyie hivi na vile?? kwanza tumeshaoana kwani unataka nini tena?? wala sio kwamba mtu alilazimisha ndoa, lakini hata hiyo mnayosema ya kulazimisha ndoa mi hainiingii akilini mwanamke hawezi kukurupuka na kukulazimisha lazima muwe na mahusiano na mahusiano mwisho wake ni ndoa sijui kama kuna mwanamke alilazimisha kuolewa na mwanaume asie na uhusiano nae!! aonjae asali sharti achonge mzinga!!!
   
 20. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,442
  Likes Received: 2,015
  Trophy Points: 280
  Utakuta ndoa ni ya mtu wa karibu na mnatakiwa wote muwepo. Nyumba hizi zinaficha mengi sana kuna jamaa niliwahi kuwaona wametoana out wenyewe pale Girrafe Hotel sijui walikuja kusuluisha ugomvi basi walikaa pale hawakuongea mwanzo mwisho na baada ya m/mke kumaliza chakula akamwambia jamaa maliza haraka tuondoke jamaa akamwambia usini-force kula haraka kilichofuata yule dada akabeba funguo za gari akanyanyuka akamwambia utanikuta kwenye gari. Yule m/ume alikasirika halafu watu kibao waliona ile movie ilivyoenda baadae akaagiza mzinga wa konyagi kubwa akaunywa kama juice ulivyoisha akatoka kumfuata mwenza wake kwenye gari
   
Loading...