Wanaume wa Kibongo, utasa na kuelekea mwaka 2014

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
701064668.jpg

Katika uzi wake wa "Dar hakuna mwanamke wa kuoa, mnaohitaji kuoa, mkaoe mikoani" Mshua's amedai kuwa "wanawake wa Dar hawana sifa za kuolewa na kuishi katika maisha ya ndoa hadi kufa na kuzikana". Hayo ni kwa mujibu wa uzoefu wake wa kushuhudia na kusimuliwa na watu mbalimbali juu ya familia zikifarakana kutokana na kuoa mwanamke aidha aliyezaliwa na kukulia Dar au kuishi miaka mingi na hatimaye kuwa na tabia za wanawake wa Dar. Ili kuondokana na tatizo hilo ameshauri kuwa kama mwanaume anataka kuishi na mwanamke kwa muda mrefu basi ni bora akaoe mkoani, japokuwa hakutoa ushauri wanawake wa Dar wakatafute wapi wanaume wa kuwaoa.

Baadhi yetu tulishajadili suala kama hili lakini kwa utani na kutokuwa serious katika thread mbalimbali. Mfano ni ule uzi wa mariantonia aliyedai kuwa "Huko dar kila duka la dawa baridi (small pharmacy) lazima ukute wanauza dawa za kuongeza NGUVU ZA KIUME na kukuza uume wakati wanapenda kuwatusi wanawake mchina,mchina,mchina,…. Umemchukuwa [mwanaume] kuwa mgeni wako usiku na bila aibu anakula chips, hata kuku robo hawezi kumaliza.."

Kapwani
nae akasema "sasa nimejua kwanini asilimia 60% watoto ndani ya ndoa sio wa mume ...nadhani wanawake waligundua siku nyingi ila wakaamua wasiseme!....Unajua mfumo dume unasaidia sana kuficha abouts za kina baba na kina mama nao wako clever/stupid... they know how to deal with these kind of problems...having children with other men hahaaaaaaa." Michelle akashauri "serikali ichukue jukumu la kupiga marufuku mashine za DNA, manake asilimia kubwa ya wanaume wenye watoto wamerutubishiwa na wenzao wenye uwezo....huu utafiti uwe siri aisee....Dar itachimbika!"

Watu wengi wanalichukulia hili tatizo kimzaha mzaha, lakini ni tatizo sugu na linaloendelea kuwaathiri wanaume wengi. Lakini wapo watu wengi wamejaribu kutoa mifano hai. Kwa mfano, kwenye uzi wake wa "Wanaume Wagumba", The Boss alisema kuwa kuna watu wawili tofauti anawajua na inasemekana hao watu ni wagumba lakini "licha ya kuoa mda mrefu hawakufanikiwa kupata watoto". Akadai kuwa hata hivyo "wake zao walikuja kuzaa watoto....na inaonekana ni watoto wa nje....au watoto wenye baba wengine....." Sasa hapo akabaki na "maswali kibao ya kujiuliza.... kwa nini wanaume wengi hawataki kwenda hospitali kupimwa"wakati "inasemekana asilimia 90 ya matatizo ya ugumba yana tiba"?

Suala la wanaume wengi wa Kibongo kutokuwa au kupungikiwa na nguvu za kiume ni nyeti sana hasa kwa wale wanaume wa Dar na miji mingine na inabidi walichukulie suala hili kwa uzito unaostahili hasa wakielekea katika mwaka 2014. Mengi yameshaandikwa humu JF lakini katika huu uzi wangu wa kufungia mwaka 2013, nitayaunganisha mengi ya yaliyokwishasemwa hapa ili katika kuelekea mwaka 2014 wanaume tuaanze angalao kulichukulia kwa uzito hili tatizo na kupima afya zetu mara kwa mara. Inabidi ifike mahali tukubali kuwa wakati mwingine mfume dume unatufanya kuwa vipofu na viziwi hasa katika masuala ambayo tunayaona ni nyeti sana kwetu.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wanaume wa Kitanzania wenye mbegu za uzazi zisizorutubisha hivyo kutoweza kurutubisha yai la mwanamke na kusababisha mimba. Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen toleo la Jumamosi Julai 17,2010 zaidi ya asilimia 35 ya wanaume waliofanya vipimo vya rutuba za mbegu za uzazi wamegundulika kuwa hawana.

Mara nyingi lawama za kukosa mtoto katika familia zimekuwa zikielekezwa kwa mwanamke kutokana na wanaume wengi kutokuwa na ujasiri wa kujitokeza kupima rutuba zao. Mazingira ya kazi, mtindo wa maisha na hata kukaa kwa muda mrefu kwenye chumba chenye mvuke ni baadhi ya sababu zinazodaiwa kuchangia wanaume kupungikwa rutuba za mbegu za uzazi.

Katika jiji la Dar pekee, inaaminika kuwa ni asilimia 24.9 tuu ya wanaume wa Dar walio na mbegu za uzazi zenye rutuba, hivyo, wenye uwezo wa kurutubisha yai la mwanamke na hivyo basi, mimba kutokea. Utafiti huo umefanywa na Idara ya Jinikolojia ya Hospitali ya Taifa Ya Muhimbili. Zaidi pitia uzi wa NGULI https://www.jamiiforums.com/habari-...-wanaume-wa-dar-wenye-mbegu-zenye-rutuba.html

Of course, wapo ambao hawakubaliana na huo utafiti hasa wanaume, jambo ambalo siyo la kushangaza kabisa. Utafiti unasema wastani wa asilimia 30 hadi 35 ya wanaume walioenda kufanya check up Muhimbili kati ya mwaka 2010-2011 kwa ajili ya vipimo vya ugumba wamejulikana hawana nguvu za kiume. Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za Kitengo cha Masuala ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake cha hospitali hiyo. Of course, wanaoenda Muhimbili kutibiwa sio wale wanaoishi Dar tuu.

Lakini kuna utafiti mwingine uliofanyika na Dk Yahaya Kapona wa Muhimbili wakati alipokuwa katika Hospitali ya Tumaini, Upanga, Dar es Salaam mwaka 2003 ambapo ulibainisha kuwa asilimia 24.9 tuu ya wanaume wanaoishi Dar walikuwa na nguvu za kiume zenye uwezo wa kuzalisha kwa asilimia 100. Akiohojiwa mwaka 2011, Dk Kapona alisema kuwa utafiti huo ni wa muda mrefu na hali inaweza kuwa imebadilika lakini akasisitiza kuwa katika utafiti wake huo unaoitwa: "Utasa kwa wanaume Dar es Salaam," ulibaini kuwa hata wanaume wanaobahatika kuzalisha, mbegu zao si imara kwa asilimia 100.

Kuhusu mikoa mingine kuna utafiti ulifanyika Moshi mwaka 2006 na Dk G. Marseng ulioitwa: "Utasa katika jamii na kliniki ya misingi ya sampuli ya wanandoa katika Wilaya ya Moshi." Utafiti huo ambao ulifanyika kwa wanandoa 269, ulibaini kuwa asilimia 30 ya wanaume walikuwa wanakabiliwa na matatizo ya ugumba. Overall, tukubali tusikubali hili ni tatizo kwa nchi nzima, lakini no doubt that Dar inaongoza na sababu zinajulikana. Sababu mojawapo inayotajwa mara kwa mara ni uvaaji wa nguo za ndani zinazobana.

Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dk Cyril Massawe, wanaume wanaoishi maeneo ya joto hapa nchini hususan Dar es Salaam, wanapaswa kutumia nguo za ndani zilizotengenezwa kwa pamba halisi ili kutunza uwezo wa manii kiuzalishaji. Anadai "Mpaka sasa [wana]pokea kesi nyingi kama hizo, idadi kubwa ya wanaume wanaokosa sifa za kuzalisha inazidi kuongezeka na ndiyo maana watu wanaotafuta watoto hivi sasa ni wengi".

Wapo watakaouliza au waliowahi kuuliza mwanaume wa Dar ni mwanaume gani? Whether or not huyo mwanaume ni Mmasai aliyehamia Dar miaka 20 iliyopita, hakuondoi ukweli wa kuwepo kwa tatizo. Tatizo la wanaume wagumba ni kubwa sana lakini taifa letu huwa haliangalii matatizo ya kijamii kama haya, ukizingatia bado ni taifa la mfumo dume. Tafiti zinadai nusu ya matatizo ya ugumba yanasababishwa na wanaume. Hata hivyo, wakati idadi ya wanawake wanaonenda kuwaona gynaecologists imeongezeka, wanaume wengi hawaangaiki hata pale madaktari wanapowashauri wake zao wawalete hosipitali. Hii inakuwa ngumu sana kwa gynaecologists kutatua hili tatizo. Matokeo yake mwanamke anaenda kuzaa na mwanaume mwingine, huku mumewe akidhani ni mtoto wake kwa sababu tuu huwa anamwaga shahawa kila anapojahimiana na mkewe.

Ni muhimu kwa pande zote kupimwa. Wanaume wengi wanaona aibu, lakini ni rahisi kupata matibabu kama tatizo likigunduliwa mapema. Bahati mbaya jamii yetu inaamini kuwa mwanaume anayetoa shahawa anaweza kumpa mwanamke yoyote mimba. Hii sio kweli. Kama alivyosema SHIEKA, "Mimi ninayo mifano kama mitano hivi ya wanaume kuwa mbogo kabisa kwenda kupimwa. Mmoja kati ya hao ninaowafahamu alitoa sababu. Alisema hivi: "Wanawake ndiyo wenye matatizo ya kuzaa sie wanaume hayo matatizo yatatoka wapi? Kitandani natimiza wajibu wangu; napanda mbegu na kila kitu. Mianawake mingi bwana haizai…Kwa mtu mwelewa utaona wazi kwamba baadhi ya wanaume wakiona jogoo lao linawika na kuweza kuliingiza kwa mwanamke, basi lazima ana uwezo wa kuzaa. Science ya sperm counts na mambo kama hayo hawajui. Kwa hiyo mtu kama huyu ukimwambia akapime hospitali atakutukana matusi ya kuli wa bandarini."

Pia watafiti wanadai wanaume wanachanganya kati ya erectile dysfunction and infertility. The fact that a man's penis doesn't function while in sterility, doesn't mean such man cannot ejaculate. Lakini tatizo wanaume wengi hawaendi kupima afya zao ili wafundishwe kwa udani haya mambo. Mwulize mwanaume yoyote hata hao walioshauri kwenda kuoa mkoani, lini walienda kupima afya zao kwa ujumla? I mean general check up na sio lazima uwe unaumwa. Mtu anajahimiana na mwanamke anatoa shahawa basi anadhani anaweza kumpa mwanamke ujauzito.

Hakuna mwanaume, hata wale ambao hawana hili tatizo wanaweza kudhibitisha moja kwa moja kuwa mtoto ni wao, lakini wanawake wenye watoto wana siri nyingi sana. Labda, ndiyo maana Ofisi ya Mkemia Mkuu ilisema hivi karibuni kuwa asilimia 48.3 ya waliojitekeza kupima DNA ili kubaini uhalali wa watoto wao walikuta kuwa hawakuwa wazazi halisi wa hao watoto. Hii haiwezi kuwakilisha population yote ya Tanzania, lakini inaweza kuwa indication kuwa kuna uwezekano wa wanaume wengi "kusingiziwa" watoto au kulea watoto wasio wa kwao.

Kwa hiyo basi katika kuelekea mwaka 2014, wanaume tuachane na dhana potofu. Kama unatoa shahawa unapongonoka haina maana kuwa lazima utakuwa na uwezo wa kumpa mwanamke mimba. Kama huwezi kuzaa na mwanamke wa Dar basi hutaweza kuzaa na mwanamke wa mkoani pia. Tusikwepe tatizo, bali tulikubali, tulikabili na kulitatua. Katika kuelekea mwaka 2014, ni muhimu sana kupima afya zetu hasa katika miaka hii ambapo asilimia 50 ya wagonjwa wanaotibiwa Muhimbili, kitengo cha Fiziotherapia, wanaumwa magonjwa yasiyoambukiza, yakiwemo yale ya uchakavu wa viungo. Magonjwa yasiyoambukiza yameshika kasi na yanapoteza uhai wa watu wengi kutokana na kushindwa kutambua njia za kuzuia magonjwa hayo yasiwatokee. Tupime afya zetu. Ni ushauri tuu.

Nawatakia heri ya mwaka mpya wenye rutuba.
 
Labda bwana Mshua atakuwa anasumbuliwa aidha na umri mdogo au alitendwa vibaya na wadada wa Dar zaidi ya mmoja. Pole kwa yote hayo.

Ukweli ni kuwa wanawake wote Tanzania kwa ujumla wao wana tabia sawa kama tulivyo wanaume wao. Tabia za kimaeneo sasa zimekufa na sote tumebaki na tabia za Uswahili ambazo ki ujumla huwa na mwenendo wa MOTO CHINI! Hii ndiyo hali halisi hivyo kuoa ni PALE ULIPO.
 
701064668.jpg

Katika uzi wake wa “Dar hakuna mwanamke wa kuoa, mnaohitaji kuoa, mkaoe mikoani” Mshua's amedai kuwa “wanawake wa Dar hawana sifa za kuolewa na kuishi katika maisha ya ndoa hadi kufa na kuzikana”. Hayo ni kwa mujibu wa uzoefu wake wa kushuhudia na kusimuliwa na watu mbalimbali juu ya familia zikifarakana kutokana na kuoa mwanamke aidha aliyezaliwa na kukulia Dar au kuishi miaka mingi na hatimaye kuwa na tabia za wanawake wa Dar. Ili kuondokana na tatizo hilo ameshauri kuwa kama mwanaume anataka kuishi na mwanamke kwa muda mrefu basi ni bora akaoe mkoani, japokuwa hakutoa ushauri wanawake wa Dar wakatafute wapi wanaume wa kuwaoa.

Baadhi yetu tulishajadili suala kama hili lakini kwa utani na kutokuwa serious katika thread mbalimbali. Mfano ni ule uzi wa mariantonia aliyedai kuwa “Huko dar kila duka la dawa baridi (small pharmacy) lazima ukute wanauza dawa za kuongeza NGUVU ZA KIUME na kukuza uume wakati wanapenda kuwatusi wanawake mchina,mchina,mchina,…. Umemchukuwa [mwanaume] kuwa mgeni wako usiku na bila aibu anakula chips, hata kuku robo hawezi kumaliza..” Kapwani nae akasema "sasa nimejua kwanini asilimia 60% watoto ndani ya ndoa sio wa mume ...nadhani wanawake waligundua siku nyingi ila wakaamua wasiseme!....Unajua mfumo dume unasaidia sana kuficha abouts za kina baba na kina mama nao wako clever/stupid... they know how to deal with these kind of problems...having children with other men hahaaaaaaa." Michelle akashauri "serikali ichukue jukumu la kupiga marufuku mashine za DNA, manake asilimia kubwa ya wanaume wenye watoto wamerutubishiwa na wenzao wenye uwezo....huu utafiti uwe siri aisee....Dar itachimbika!"

Watu wengi wanalichukulia hili tatizo kimzaha mzaha, lakini ni tatizo sugu na linaloendelea kuwaathiri wanaume wengi. Lakini wapo watu wengi wamejaribu kutoa mifano hai. Kwa mfano, kwenye uzi wake wa “Wanaume Wagumba”, The Boss alisema kuwa kuna watu wawili tofauti anawajua na inasemekana hao watu ni wagumba lakini “licha ya kuoa mda mrefu hawakufanikiwa kupata watoto”. Akadai kuwa hata hivyo “wake zao walikuja kuzaa watoto....na inaonekana ni watoto wa nje....au watoto wenye baba wengine.....” Sasa hapo akabaki na “maswali kibao ya kujiuliza.... kwa nini wanaume wengi hawataki kwenda hospitali kupimwa”wakati “inasemekana asilimia 90 ya matatizo ya ugumba yana tiba”?

Suala la wanaume wengi wa Kibongo kutokuwa au kupungikiwa na nguvu za kiume ni nyeti sana hasa kwa wale wanaume wa Dar na miji mingine na inabidi walichukulie suala hili kwa uzito unaostahili hasa wakielekea katika mwaka 2014. Mengi yameshaandikwa humu JF lakini katika huu uzi wangu wa kufungia mwaka 2013, nitayaunganisha mengi ya yaliyokwishasemwa hapa ili katika kuelekea mwaka 2014 wanaume tuaanze angalao kulichukulia kwa uzito hili tatizo na kupima afya zetu mara kwa mara. Inabidi ifike mahali tukubali kuwa wakati mwingine mfume dume unatufanya kuwa vipofu na viziwi hasa katika masuala ambayo tunayaona ni nyeti sana kwetu.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wanaume wa Kitanzania wenye mbegu za uzazi zisizorutubisha hivyo kutoweza kurutubisha yai la mwanamke na kusababisha mimba. Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen toleo la Jumamosi Julai 17,2010 zaidi ya asilimia 35 ya wanaume waliofanya vipimo vya rutuba za mbegu za uzazi wamegundulika kuwa hawana.

Mara nyingi lawama za kukosa mtoto katika familia zimekuwa zikielekezwa kwa mwanamke kutokana na wanaume wengi kutokuwa na ujasiri wa kujitokeza kupima rutuba zao. Mazingira ya kazi, mtindo wa maisha na hata kukaa kwa muda mrefu kwenye chumba chenye mvuke ni baadhi ya sababu zinazodaiwa kuchangia wanaume kupungikwa rutuba za mbegu za uzazi.

Katika jiji la Dar pekee, inaaminika kuwa ni asilimia 24.9 tuu ya wanaume wa Dar walio na mbegu za uzazi zenye rutuba, hivyo, wenye uwezo wa kurutubisha yai la mwanamke na hivyo basi, mimba kutokea. Utafiti huo umefanywa na Idara ya Jinikolojia ya Hospitali ya Taifa Ya Muhimbili. Zaidi pitia uzi wa NGULI https://www.jamiiforums.com/habari-...-wanaume-wa-dar-wenye-mbegu-zenye-rutuba.html

Of course, wapo ambao hawakubaliana na huo utafiti hasa wanaume, jambo ambalo siyo la kushangaza kabisa. Utafiti unasema wastani wa asilimia 30 hadi 35 ya wanaume walioenda kufanya check up Muhimbili kati ya mwaka 2010-2011 kwa ajili ya vipimo vya ugumba wamejulikana hawana nguvu za kiume. Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za Kitengo cha Masuala ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake cha hospitali hiyo. Of course, wanaoenda Muhimbili kutibiwa sio wale wanaoishi Dar tuu.

Lakini kuna utafiti mwingine uliofanyika na Dk Yahaya Kapona wa Muhimbili wakati alipokuwa katika Hospitali ya Tumaini, Upanga, Dar es Salaam mwaka 2003 ambapo ulibainisha kuwa asilimia 24.9 tuu ya wanaume wanaoishi Dar walikuwa na nguvu za kiume zenye uwezo wa kuzalisha kwa asilimia 100. Akiohojiwa mwaka 2011, Dk Kapona alisema kuwa utafiti huo ni wa muda mrefu na hali inaweza kuwa imebadilika lakini akasisitiza kuwa katika utafiti wake huo unaoitwa: “Utasa kwa wanaume Dar es Salaam,” ulibaini kuwa hata wanaume wanaobahatika kuzalisha, mbegu zao si imara kwa asilimia 100.

Kuhusu mikoa mingine kuna utafiti ulifanyika Moshi mwaka 2006 na Dk G. Marseng ulioitwa: “Utasa katika jamii na kliniki ya misingi ya sampuli ya wanandoa katika Wilaya ya Moshi.” Utafiti huo ambao ulifanyika kwa wanandoa 269, ulibaini kuwa asilimia 30 ya wanaume walikuwa wanakabiliwa na matatizo ya ugumba. Overall, tukubali tusikubali hili ni tatizo kwa nchi nzima, lakini no doubt that Dar inaongoza na sababu zinajulikana. Sababu mojawapo inayotajwa mara kwa mara ni uvaaji wa nguo za ndani zinazobana.

Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dk Cyril Massawe, wanaume wanaoishi maeneo ya joto hapa nchini hususan Dar es Salaam, wanapaswa kutumia nguo za ndani zilizotengenezwa kwa pamba halisi ili kutunza uwezo wa manii kiuzalishaji. Anadai “Mpaka sasa [wana]pokea kesi nyingi kama hizo, idadi kubwa ya wanaume wanaokosa sifa za kuzalisha inazidi kuongezeka na ndiyo maana watu wanaotafuta watoto hivi sasa ni wengi”.

Wapo watakaouliza au waliowahi kuuliza mwanaume wa Dar ni mwanaume gani? Whether or not huyo mwanaume ni Mmasai aliyehamia Dar miaka 20 iliyopita, hakuondoi ukweli wa kuwepo kwa tatizo. Tatizo la wanaume wagumba ni kubwa sana lakini taifa letu huwa haliangalii matatizo ya kijamii kama haya, ukizingatia bado ni taifa la mfumo dume. Tafiti zinadai nusu ya matatizo ya ugumba yanasababishwa na wanaume. Hata hivyo, wakati idadi ya wanawake wanaonenda kuwaona gynaecologists imeongezeka, wanaume wengi hawaangaiki hata pale madaktari wanapowashauri wake zao wawalete hosipitali. Hii inakuwa ngumu sana kwa gynaecologists kutatua hili tatizo. Matokeo yake mwanamke anaenda kuzaa na mwanaume mwingine, huku mumewe akidhani ni mtoto wake kwa sababu tuu huwa anamwaga shahawa kila anapojahimiana na mkewe.

Ni muhimu kwa pande zote kupimwa. Wanaume wengi wanaona aibu, lakini ni rahisi kupata matibabu kama tatizo likigunduliwa mapema. Bahati mbaya jamii yetu inaamini kuwa mwanaume anayetoa shahawa anaweza kumpa mwanamke yoyote mimba. Hii sio kweli. Kama alivyosema SHIEKA, “Mimi ninayo mifano kama mitano hivi ya wanaume kuwa mbogo kabisa kwenda kupimwa. Mmoja kati ya hao ninaowafahamu alitoa sababu. Alisema hivi: "Wanawake ndiyo wenye matatizo ya kuzaa sie wanaume hayo matatizo yatatoka wapi? Kitandani natimiza wajibu wangu; napanda mbegu na kila kitu. Mianawake mingi bwana haizai…Kwa mtu mwelewa utaona wazi kwamba baadhi ya wanaume wakiona jogoo lao linawika na kuweza kuliingiza kwa mwanamke, basi lazima ana uwezo wa kuzaa. Science ya sperm counts na mambo kama hayo hawajui. Kwa hiyo mtu kama huyu ukimwambia akapime hospitali atakutukana matusi ya kuli wa bandarini.”

Pia watafiti wanadai wanaume wanachanganya kati ya erectile dysfunction and infertility. The fact that a man’s penis doesn’t function while in sterility, doesn't mean such man cannot ejaculate. Lakini tatizo wanaume wengi hawaendi kupima afya zao ili wafundishwe kwa udani haya mambo. Mwulize mwanaume yoyote hata hao walioshauri kwenda kuoa mkoani, lini walienda kupima afya zao kwa ujumla? I mean general check up na sio lazima uwe unaumwa. Mtu anajahimiana na mwanamke anatoa shahawa basi anadhani anaweza kumpa mwanamke ujauzito.

Hakuna mwanaume, hata wale ambao hawana hili tatizo wanaweza kudhibitisha moja kwa moja kuwa mtoto ni wao, lakini wanawake wenye watoto wana siri nyingi sana. Labda, ndiyo maana Ofisi ya Mkemia Mkuu ilisema hivi karibuni kuwa asilimia 48.3 ya waliojitekeza kupima DNA ili kubaini uhalali wa watoto wao walikuta kuwa hawakuwa wazazi halisi wa hao watoto. Hii haiwezi kuwakilisha population yote ya Tanzania, lakini inaweza kuwa indication kuwa kuna uwezekano wa wanaume wengi “kusingiziwa” watoto au kulea watoto wasio wa kwao.

Kwa hiyo basi katika kuelekea mwaka 2014, wanaume tuachane na dhana potofu. Kama unatoa shahawa unapongonoka haina maana kuwa lazima utakuwa na uwezo wa kumpa mwanamke mimba. Kama huwezi kuzaa na mwanamke wa Dar basi hutaweza kuzaa na mwanamke wa mkoani pia. Tusikwepe tatizo, bali tulikubali, tulikabili na kulitatua. Katika kuelekea mwaka 2014, ni muhimu sana kupima afya zetu hasa katika miaka hii ambapo asilimia 50 ya wagonjwa wanaotibiwa Muhimbili, kitengo cha Fiziotherapia, wanaumwa magonjwa yasiyoambukiza, yakiwemo yale ya uchakavu wa viungo. Magonjwa yasiyoambukiza yameshika kasi na yanapoteza uhai wa watu wengi kutokana na kushindwa kutambua njia za kuzuia magonjwa hayo yasiwatokee. Tupime afya zetu. Ni ushauri tuu.

Nawatakia heri ya mwaka mpya wenye rutuba.
Mkuu umesema ukweli mtupu,nakutakia kheri ya mwaka mpya.
 
Dah! sasa si bora nichukue wa hawa hawa ambao tunakula nao hizo chips ninaweza kusurvive kidogo kuliko kuchukua machine kubwa za mikoani zenye engine ya scania si nitashushwa kifuani mtoto wa watu mie niumbuke bure,naona mshua hakutafakari hili kwa kina
 
duh, mimi sijui hata kama niko salama kwa kweli
Ndo uende ukapimwe ili ujue mbivu na mbichi. Mkuu EMT umeeleza kwa kina sasa mwenye macho na asome na kuelewa kisha wachukue hatua. Huu mfumo dume ni ugonjwa sijui utatibika lini . Wanandoa wenye matatizo ya uzazi mara nyingi husukumiwa mama tena mpaka ndugu humwandama mwanamke . Wanaume badilikeni tunapoelekea 2014.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
Mimi imani yangu siko kwenye kundi la wasiozalisha,research yangu inaonyesha nikikugusa within 3 months lazima kijibu uanze kujisikia kichefuchefu

Lakini kupitia uzi huu nawashauri wanaume wenzangu tuache mfumo dume na tuonyeshe ushirikiano kwenye suala la Kupima uwezo wetu wa kuzaa kwani uzazi unahusisha jinsia zote mbili,usijione unatoa madini yanaweza yakawa fake na wapo ambao wanatoa madini ya dhahabu ya ukweli hapa methali ya ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi inatumika ,nini kinathibitisha ni kufanya "SPERM ANALYSIS" maabara
 
Dah inabidi nichukue hatua sasa ila Mshua alichozungmzia wanawake wa Dar sio maswala ya uzazi ni tabia zao may be vinamahusiano ila sidhani kama ni upungufu wa nguvu za kiume unasababisha moja kwa moja wanawake wa Dar kuwa hivi walivyo kuna haja ya kufanya uchunguzi mwingine.
 
kwa mwendo wa
-slice mbili za mkate na kijikombe cha kahawa asbh,mchana chips na sausage mbili,jioni kati bia na mishkako ya firigisi,usiku mamito kapika spaghetti na mayai
-kazini gari,ofisini AC,chumba cha kulala AC,
-masigara hayakauki mfukoni
-stress za foleni masaa manne
-stress za kulipa kodi nyumba mbili sijui tatu japo unalala kwneye nyumba moja zingine unakaa masaa mawili tu
-ada za shule zinazopanda kila kukicha
-mke asiye na kiasi kila fasheni anaitaka na kila kitchen party lazima aende
-vyakula vya supermarket mpka kitunguu swaumu
-kwenda kanisani na msikitini ni mpka xmas na iddi
-ndugu wasioelewa kuwa una familia sasa unahitaji muda kuhudumia familia yako
-visasi vya kudhulumiana dili za maofisini na kwenye biashara
aaaaargh LAZIIIIIIMA MWANAUME UKOSE KUWA NA UWEZO WA KIJINSIA ULIOKAMILIKA!
laaaaaazimah!
HURUKI KAMBA!,unarukaje sasa?
happy being a woman asee!
 
Tatizo sio wanaume ila wanawake wengi wa Dar wanaongoza kwa Kunyofoa Mimba. Pia hivyo vizazi vyao vimepitia misukosuko ya kufa mtu kutokana na kusukumwa ovyo mara kwa mara kila wanapokutana na mguu wa mtoto. Hapo sijajumlisha madawa ya Uzazi wa Mpango, Magonjwa ya zinaa wanayoyatibu kila kukicha.

Asilimia kubwa ya hao wanaume wanaoenda kupima uzazi ni kuwa tayari wanajigundua wana matatizo ndio maana figures zimekaa hivyo.

Mi ntajiolea binti Mbichiiii mkoani, Kitoto cha miaka 18 chenye bikra na kizazi freshhhhhh kabisaaaa. Kizazi chepesiiii ukigusa tu kwenye siku kitu na box.
 
Mkuu umesema ukweli mtupu,nakutakia kheri ya mwaka mpya.

mkuu kuquote thread ndefu kama hizi mnatuumiza sana sisi tunaotumia device ndogo! plea jamani ni bora mtu u-reply kawaida kuliko kureply with quote.. please wana jf tusikilizane kwa hili!
 
kwa mwendo wa
-slice mbili za mkate na kijikombe cha kahawa asbh,mchana chips na sausage mbili,jioni kati bia na mishkako ya firigisi,usiku mamito kapika spaghetti na mayai
-kazini gari,ofisini AC,chumba cha kulala AC,
-masigara hayakauki mfukoni
-stress za foleni masaa manne
-stress za kulipa kodi nyumba mbili sijui tatu japo unalala kwneye nyumba moja zingine unakaa masaa mawili tu
-ada za shule zinazopanda kila kukicha
-mke asiye na kiasi kila fasheni anaitaka na kila kitchen party lazima aende
-vyakula vya supermarket mpka kitunguu swaumu
-kwenda kanisani na msikitini ni mpka xmas na iddi
-ndugu wasioelewa kuwa una familia sasa unahitaji muda kuhudumia familia yako
-visasi vya kudhulumiana dili za maofisini na kwenye biashara
aaaaargh LAZIIIIIIMA MWANAUME UKOSE KUWA NA UWEZO WA KIJINSIA ULIOKAMILIKA!
laaaaaazimah!
HURUKI KAMBA!,unarukaje sasa?
happy being a woman asee!

So unashauri nini ?
 
Back
Top Bottom