Wanaume wa Kenya kujishebedua kumbe wanadundwa na wake zao hasa wakikuyu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume wa Kenya kujishebedua kumbe wanadundwa na wake zao hasa wakikuyu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mpayukaji, Mar 16, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  [h=3]Wanawake wa Nairoberry ni kiboko ya wanaume[/h]

  [​IMG]

  Simon Kiguta akiwa kwenye Hospitali ya Nyeri Feb. 11, 2012. Alikatwakatwa mapanga usoni na mkewe baada ya kurejea nyumbani usiku akiwa amelewa. (Joseph Kanyi/Nation photo)

  Na Nkwazi Mhango

  Baada ya kutoka zangu London juzi nilipitia Nairobi kuongea mawili matatu na wanakijiwe cha River Road na Ngala. Sikukwa na mpango wa kusimama kidogo Nairobi. Ila nikiwa zangu London Mureithi ambaye ni mwenyekiti wa Kijiwe kile alinitwangia simu akiomba nipitie Nairobi lau nitoe ushauri.


  Nilifaidi sana uzuri wa mji wa London. Barabara zote zina lami, taa, zinapigwa deki usiambiwe. Nilipofika Heathrow airport, sorry, International Airport nilitaka kuzimia nilipolinganisha na jiji letu la uchafu na ufisadi liitwalo Chafusalama.

  Sikuona mgambo wa site mamantilie wala wazee wa mabao kwenye barabara za London. Kitu kimoja kilinistua sana-London kaya inachomwa hadharani na hakuna anayejali! Nilipomuuliza mvuta kaya mmoja akacheka na kusema kuwa kaya haina tatizo kwa taifa bali kwa mtu binafsi. Hivyo, nami niligundua kuwa kumbe hapa kwetu heri turuhusu watu wajichomee kaya kuliko kuruhusu ufisadi. Maana ufisadi unaumiza wengi. hata uchafu wa miji yetu ni hatari kwa kila ajae na aishie kwenye miji yetu. Ni ushahidi wa uchafu wetu wa kitabia.

  Najua nikirejea kijiweni kwangu wengi nitakaowasilimulia usafiw a London watanisuta na kuhoji kama naona hivvyo kwa wenzangu nashindwa nini kutekeleza kwangu? Najua wengi wataniona kama **** na mtalii asiyejifunza. Hata hivyo tuache utani. Tuna tatizo tena si dogo. Yaani tunashindwa kujifunza hata mambo ya msingi kama usafi, mipangilio ya miji na mambo madogo kama haya? Au nayo tunataka waje wafadhili watusaidie kama walivyofanya kutuchimbia vyoo tukaishia kuvichafua?

  Tukirejea kwenye kijiwe cha River Road Nairoberry ni kwamba siku hizi kule umeibuka mchezo wa akina mama kuwashikisha adabu waume zao. Ukichelewa kurudi unapatiwa. Wajua kupatiwa maana yake nini? Kuadhibiwa. Ukishindwa kufanya shughuli za ndani hasa za night unapatiwa. Ukitoroka kwa nyumba kwenda kula kwa hoteli, ukirudi unapatiana adhabu kama kawaida. Ukinywa sana kanywaji na kushinda kumudu idara zote, unapatiana adabu.


  Huwezi kuamini kuwa juzi nilikuwa kwenye mahakama ya Kilimani kushuhudia mama mmoja akikabiliwa na kosa la kumpiga mumewe hadi akazimia. Toka na vipigo vya hapa na pale vya mara kwa mara, walume wa nchi ya Nyayo wameamua kuanzisha chama cha kulinda haki za walume. Kunogesha stori ni kwamba kipindi nilichokuwa kule, walume wote walikuwa wamekubaliana kugoma kula chakula nyumbani ili akina mama wapunguze morali wa Kikyuki.


  Hakuna kitu kiliniua kama maongezi haya kijiweni. Mara anakuja Wagacohi na kuamkua, “Kohani atya?”
  Njoroge na Wamauseto wanaitikia, “Kutiri na kaolu.”

  Wagacohi anaendelea, “Mnajuanga kuwa Ithe wa Kinywa amepigwa na bibi yake hadi akepelekwa hosi?” Hosi maana yake ni hospitali.


  Anaendelea, “Nyina wa Kamuyu ameniambia kuwa alipokwenda kunywa akaselewa kurudi akapatiana adhabu kali sana.”

  Gathuma anadandia, “Haki mimi bibi yangu akipatiana adhabu na mimi nitaua yeye.” kabla ya kuendelea, Gitau anachomekea, “Kama umeoanga Central hasa Nyeri jua unapigwanga tu. Vinginevyo uwe umeoa kibeti cha Kikamba.” Wamuseto hana mbavu. anasema, “Haki, kwetu Matuu, Mbooni na Woote bibi hapingangi bwana. Sisi wakamba bibi akipinga bwana atalaaniwa aote devu. Kibeti ya Kikamba siyo Kama hii ya Kikuyu.” Anakunywa kahawa yake na kutafuna mirungi kidogo na kuendelea, “Wajua siku moja mimi naona bibi kule Ithekahuno akitwanga bwana hadi bwana anakufa kwa muda?”
  Anamalizia, “Ukiona bibi anatwanga wewe understad wewe ni nugu-nyani.”

  Mzee Gate anachomekea, “Wacha mabo yako wewe. Bibi akiamua twanga wewe anatwanga tu. Hukuona Luse alivyopiga watu ya habari pale Nation na hakuna ameshitaki yeye? Hata Kebaki mwenyewe hasemangi Luse akileta matata.”

  “Kama munene kama Kebaki anapindwa nani wewe ulete nyoko nyoko kwa bibi ya kisasa asitwange wewe?” Mara mzee Gate ananigeukia. “Kama unataka bibi asipige wewe nenda kanunue bibi TZ. Huko nasikianga wanasema tafadhali wacha kuselewa na kurudi usiku badala ya kupatiana adhabu.”
  Wamuseto anamuunga mkono mzee Gate, “Nasikianga watz ni wapoa sana. Tena ni wabeautiful.”Mie sina mbavu.

  Tukiwa tunaendelea kupata kahawa na kutafuna miraa si alikurupuka rafiki yangu Ndirangu. Anakuja akipiga kelele, “Woi woooi, nakwa nie yaani nakufa mie.” punde si punde mkewe Wanjiku anatokea akiwa ameshika gongo akitaka ammalizie Ndirangu.

  wanjiku anahanikiza, “Rehe besha zakwa ngiri igiri na ihenya, yaani leta pesa yangu elfu mbili haraka.” msishangae kusikia elfu inaitwa ngiri. Anaendelea, “Ithe wa Katuru, nuuga rehe besha zakwa naihenya.”
  Ndirangu kuona walume wenzie tupo akajitutumua na kusema, “Dhie wega naiwe. Mutumia mworu uyu-yaani nenda salama, mwanamke mbaya huyu.”

  “Ati, kama unatusi mimi kwa vile iko mbele ya watu, ukija kwa nyumba napatiana adhabu kali saidi ya Hii. Hii mabo ya kuleta mudomo kwa bibi hapa jua italeta taabu mingi kwa wewe.” Alijibu Wanjiku kwa ukali huku akigeuza kurudi zake nyumbani tayari kumngojea mumewe ili akija ampatie discipline.

  Akiwa anaondoka alisema, “Kwa vile hutaki kuleta besha yangu, ile nyama ya roho na mukimo amepika hukulangi leo (anamaanisha nayana ya moyo na ugali). Kama unaweza shukua ngwashee uchomege ukule hapo kwa kahawa.” (Ngwashee ni viazi).
  Muiruri anamgeukia Ndirangu na kusema, “Jamba, mabo ya nyuba uwe unamaliza kwa nyuba siyo kuja hapa na kuleta matata.” Anatafuna miraa na kuendelea, “Wewe hapana kamata bibi sawa sawa hadi napata mudomo kukuja hapa na kuropoka bere ya wanaume.”

  Izo kumba za moyo sizikwa
  Nakoma mabvuto akulobeta mama ine moyo
  Moyo wanga ni mabvuto ine moyo
  Sunga wa busee
  Ndinu oletwa ambuye
  Oletwa ndinu
  Usanga zose ndinu
  Moyo moyooo
  Naona bi mkubwa kaja acha nitimke kabla hajanitia discipline.
  Chanzo: Tanzania Daima Machi 14, 2012.
   
 2. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  oldies
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Isolated incidents should not be taken as being the norm.
   
 4. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hata Tanzania hizi case zipo na wengine wamekatwa hadi nanihii zao.
   
Loading...