Wanaume- umeiandaa vipi familia yako pale utakapofariki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume- umeiandaa vipi familia yako pale utakapofariki?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BADILI TABIA, Mar 16, 2012.

 1. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  Habari,

  wanaume mje tusemezane....
  hivi ukifa leo umeiandaa vipi familia kukabiliana na maisha? na kama una watoto wadogo ambao wanakutegemea umeandaa vipi maisha ya watoto mara utakapotoweka?
  je watoto watasoma?
  watakula?
  wataishi kwenye nyumba gani?
  wakiugua hospitali itakuwaje?
  watakula mlo kamili?


  hivi ukiitwa leo mbele za haki mali zako zitaangukia kwenye mikono ya nani?nimeuliza hili kutokana na kesi kadhaa nilizozishuhudia....kuna kaka alifariki (bahati nzuri au mbaya mkewe alishatangulia mbele za haki, akamwachia watoto wadogo wawili) na alikuwa anaishi na hawara, siku chache kabla ya kufariki alimwachia mpunga wote girlfriend wake, ikaleta mfarakano kati ya ndugu ambao ndo walichukua malezi ya watoto....

  kuna wanaoficha mali zao kwa mke na watoto, hawa huwaonyesha mali zao marafiki/ndugu mauti yanapowakuta familia inadhulumiwa, na ndugu hawa ndo wanakuwa wa kwanza kuchukua mali zao na kudhulumu watoto, wanawaacha watoto bila nyuma wala mbele wakitanga tanga barabarani....


  • je mali zako mkeo/ wanao wanazijua?
  • umeacha wosia? na kama umeacha wosia je msimamizi wa mirathi(hapa Mungu saidia) unamwamini? atawaongoza vyema wanao? hatawadhulumu?

  • je unafamilia ngapi? moja na mkeo au familia kadhaa(ambazo huibuka ukishafariki) je unaziacha katika hali gani ili kuepuka migogoro

  ingawa nimewauliza wanaume, wanawake pia mtafakari.......
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  stori kama hizi watu naona zinawachosha. Hawataki kufikiria na kujipanga. Wanapenda za macho mazuri na hawara na mpenzi wangu... Ni habari nzuri ya kufikirisha
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa maswali mazuri mheshimiwa mleta thread. Ukiwa kama mleta thread tena mwanamke, tunaomba utuambie wewe umejiandaaje. Maswali ya nyongeza yatafata. Ahsante.
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  hadi wewe hutaki kufikiria.
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mimi nilenda RITA wakanipa ushauri juu ya mirathi na mali......nanyi nendedi
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha, ngoja tukajadili na mama Ngina.......................
   
 7. s

  sawabho JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Kwa nini Mwanaume tu ndio wa kujiandaa, ilhali kila siku mnalilia haki sawa ?
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Dah, ndo tunajitahidi hivyo kuwaandalia kidogo kidogo.
  Si unajua muda wa kushika pesa kibongo bongo ni at least 40.

  Sasa ambao bado hapo, huwezi sema umejiandaa sawasawa unavyotaka iwe.
   
 9. mtoto mpole

  mtoto mpole JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 679
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  so touching thread..... m still loading
   
 10. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  kwa kweli mi ndo nimeanza maisha. Kama Mungu ananichukua hivi punde sina jinsi. Najua familia yangu changa itateseka maana hata sifa za kupata pension sijafikisha maana muda niliochangia kwenye mfuko wa jamii ni mfupi sana. Ila akinipa muda wa miaka mitano nikia na familia yangu nitafanya tasmini ya tulivyojiandaa.
   
 11. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Swali linafikirisha sana hili..

  ngoja nitafakari.
   
 12. mgeni10

  mgeni10 JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,112
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa kwamba watu wengi, ( sio wote ) kufikiri juu ya maisha ya Baadae sio tu kwa sababu umekufa, ila hata ukipata shida itakayo kufanya ushindwe kupigana kimaisha, inakua ngumu sana, na sijui kama unaweza wafanya wakapata hamu ya kufikiri hayo
   
 13. majany

  majany JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2012
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  kwani nani kakwsmbia nwanaume ndo wa kwanza kufa???Je we mama leo ukifa,umewaandalia chochote wanao???
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280

  hus, pamoja na uanamke wangu nina kipato, pia nina will, in case of anything wanangu ndio warithi....mali zangu (zile nilizochuma mwenyewe kabla ya ndoa, na tunzochuma ndoani zinajulikana kwangu na mwenzangu )zipo wazi wanangu na mume wangu pamoja na mama yangu wanazijua......

  Na mume wangu pia amefanya hivyo, ingawa siwezi kuusemea moyo.....
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  hakuna ajuae ataanza nani, just in case umekufa familia unaiachaje? Au wewe na mwenzio mnaachaje familia?
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa, watu hawataki kuwaza kifo.....pamoja na kutopenda kuwaza hayo bado kinatokea........hakuna jinsi ya kukikimbia....na tunasahau kikitokea watoto tunaowapenda na kuwalinda kupita mboni za macho yetu hatutakuwa na uwezo wa kuwalinda wala kuwatetea tena

   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280

  tafakari urudi mkuu, mchango wako ni muhimu sana....
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa, hakuna anayetaka kusikia kuhusu kifo....loh!!!!!!!


   
 19. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Kumbe kwenye ndoa kuna mali ambazo hazihusiki na ndoa yenu halafu ndio kuna zile mali za ndoa!!??.....kweli hakukosea yule aliyesema Mwanamke siyo ndugu yako, ni sahihi kabisa.
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kweli RITA wanashauri..... Natamani watanzania wengi wangejua ili kuwalinda watoto wao...
   
Loading...