Wanaume tuwe makini kwa mabinti tulionao kwenye mahusiano

Alwatanbhai

Member
May 1, 2013
74
77
Kama una date na binti wa umri wa kuanzia miaka 23 kuendelea na hauna mpango wa kumuoa fanya jambo la kiungwanana kumuambia ukweli.
Sikuambii umuambie kua humtaki na hutaki kuoa bali muambie kua wewe si muoaji na unaona kama utampotezea muda wake bure na kuja kumuumiza.

Ongea kiungwana na ikishindikana muache hata kibabe. Hii ni kwasababu mwanamke anawekeza vitu vingi katika mahusiano, anawekeza akili yake, mali zake, hisia na kubwa kabisa anawekeza umri wake katika mahusiano

Unampunguzia uwezekano wa kukutana na mtu sahihi kwa kuendelea kumdanganya. Kwa Mwanamke, Age is not just a Number Age is Everything
Wakati ukimuacha wewe utatafuta Binti mdogo zadi yake, yeye atalazimika kutafuta Kijana mwenye Umri Mkubwa zaidi yake. Ndiyo ilivyo sote Wanaume na Wanawake huangalia Umri katika Mahusiano.

Ukimchezea na kumuacha akiwa katika Umri wa Miaka 30, inamaana atafute kijana mwenye Umri kuanzia Miaka 32 ambaye bado ni Single.Wako wachache sana wa namna hiyo, sisemi kua hawezi kupata, hapana Nasema utampa Wakati Mgumu na Uhuru wa Kuchagua.

Kuna Umri ambao Mabinti wengi huamua Kuolewa tu, si kwasababu ya Mapenzi bali kwakua hawana namna wanaona kusubiri Mtu Sahihi watapishana na Kalenda
Badilika, haikufanyi Mwanaume zaidi kwa kumpotezea Binti wa watu Miaka Mitano halafu unamuambia Wewe si Type yangu Fanya jambo la Kiungwana na Malizaneni Mapema.

Lakini najua kuna Mabinti ambao hawasikii wakiambiwa kuwa mambo yameisha, Mlazimishe asikie na Usimtumie na Kumuumiza kwakua anakupenda.
Women have many possibilities from 12 to 24,but from 25 and above,the graph starts to fall down whether they like it or not,
Dear,Women ,men love by reasons


Mungu awaguse wanaume somo liwaingie
 
Mwanamke kama ni miss independent haya tunayohisi yana umuhimu kwake wala haipo hivyo.
 
Wanawake wengi ndio wao wanapaswa kuwa makini sana kwa kila hatua wanayopigaa mana akiwa na mwanaume tuu lazima mwanamke amuulize mwanaume huyoo nini dhumuni la mahusiano yetu ili ajue kama hit and run au ndio mapenzi mungu akipenda ndoa ...


Sasa unakuta msichana kazi yake kutoa papuchi tuu hajawahi hata siku moja kuja kuuliza kuwa nini hitimisho la mahusiano yetu


Unafikiria nn hapooo
 
humanity based talk. SAWA
lakini lazima ukumbuke kuwa wanaume wengi wa sasa wanataka kitu EXTRA kwa mwanamke.
si tu mapenzi na heshima kama ilivyokuwa mwanzoni...la hasha.
mwanamke wa sasa ili aolewe na mwanaume smart lazima ajipambanue kuwa na msaada kwa mume wake ikibidi awe na uwezo wa kufikiria 3/4 ya fikra za mume
mambo ya kusubiri mume apange, aamue na afanye yamepitwa na wakati
 
Si kila mahusiano yanazaa ndoa. Hilo halipo hivyo. Kuna kosa kubwa wasichana wanafanya. Wana assume mapenzi yale ni transition period to marriage. Hatuoi kwa sababu tu ya kulala kitandani. Kuna mambo mengi tunachunguza pale hadi nifikie kutamka naoa.

Na kama kuna mwanaume anamfuata mwanamke na kutamka moja kwa moja anataka kukuoa, watch out. Ni mwongo. Labda awe aliwapa kazi wazazi wake kukuchunguza muda mrefu. Na wao wakasema anafaa. Ndoa nyingi zinazopatikana siku hizi ni zile tunazotafuta wenyewe kwa kitambo kirefu.

Wanawake wengi hivi sasa ukimtokea tu anakupa au kukuambia mambo mawili. Moja, uhumdumie hata kabla hujapata. Pili anakuambia ndiye mumewe. Unashangaa inakuwaje mimi just first Day napewa bill au kulazimishwa kusaini cheki ?

Ni kosa kubwa. Kingine uaminifu kwa sasa haupo tena. Mwanamke unakuwa nae na anataka umuoe lakini hapo hapo ana mpenzi mwingine kwa siri. Hii ni kusema analinganisha au anafanya mtego. Kukiharibika huku aende kule. Tumeshtuka. Hatuingii kichwa kichwa.

Tunahitaji heshima, uaminifu, uchapa kazi sehemu zote mbili, ujue kupika, kufua, kufanya usafi wa sehemu zote. Wanawake mtafute ndoa halali msitafute harusi za mapambo. Mkitafuta harusi tu hamtadumu. Mtaachika. Kwa wakristu ndio itakuwa adios hiyo. Hutapata mume. Kumbukeni mwanaume anao uwezo kuoa mwanamke hata akipita miaka 50 ,bado atapata kinda au ndama mtoto. Wewe huwezi kamwe.
 
Back
Top Bottom