Wanaume tuwe karibu na kuwajali wenza wetu

beevenom

JF-Expert Member
May 1, 2017
313
428
Wakuu habarini za asubuhi na kwa wale wenzangu nawatakia ibada njema kabisa.
Jamani wanaume naomba tukumbushane jambo la kuwa karibu,kuwajali hawa maua ya dunia,maana bila hivyo kumwegwa ni dk 0 kwa atakayeonyesha kujali.

Inafikirisha na kuumiza pia,yaani unamchakata mdada au mmamaa na ukimhoji inakuwaje anakutunuku kwa kiasi kile? Jibu ni rahisi kweli eti unajua kucare sana! Kweli hilo tu lifanye umpe kipusa jamaa? Inakatisha tamaa mno hasa ukijiuliza ni mara ngapi kutokana na mazingira ya kazi na mambo mengi ya dunia unakuwa bize sana hata kula tu unasahau.
Kwa hiyo jamani pamoja kuwa busy sana na kutandaza makengere yetu kwa mbwembwe kwa wenzetu hiyo haitoshi kabisa. Maana nimebaini akina zero na wenzie wanatumia fursa hiyo adhimu na adim kupembua madini yetu. Yaani ukiwa karibu tu Ke na ukaonesha kujali sana baasi nafasi ya kupembua inakuwa kubwa sana

Pamoja na ugumu/ ubize na maisha tukumbuke hili pia. Mwenye masikio na asikie na kuzingatia haya.

Wenu katika ujenzi wa vinu vya kupembua

Beevenom

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom