Wanaume tushiriki katika sala hii kwa ajili ya wanawake

Ombudsman

JF-Expert Member
Apr 18, 2012
3,565
3,730
Husika na kichwa cha habafi hapo juu,

Ni vizuri sisi wanaume tushiriki kufanya sala kama hawa wanawake wataweza kubadilila japo kidogo.

1. Atakua na simu yake mpo nyumbani dakika hiyo anakwambia umbip hajui kaiweka wapi.
-Tuhurumie Baba

2. Ana nguo zimejaa makabati mawili lakini hajui avae nini ukimwambia mtoke.
-Baba, ni magumu kwetu mambo haya.

3. Anakasirika ukikosa kumtumia text ya good night lakini yeye akikosa wewe inabidi uwe muelewa.
-Tuwaeleweje, Baba?

4. Ana viatu zaidi ya pea 50 lakini hana viatu vya kuvaa vya kwenda ibadani.
-Mungu uwasamehe

5. Akianza kuvaa saa moja atamaliza saa tano muda wote inabidi umsubiri tu.
-Si kupenda kwao Baba ila nasi yanatushinda Bwana.

6. Akienda saloon anakaa kuanzia asubuhi mpaka jioni na huna budi kumsubiri na usilalamike.
-Mungu wetu, tupe moyo wa kuyahimili haya.

7. Ana mafuta tofauti ya kujipaka mikono, shingo, kisogo, miguu, mpaka kisigino! Hata mdomoni
-Ee Mungu ni wewe uyajuaye mateso tuyapitiayo Baba

8. Mnaachana asubuhi akiwa na furaha na ukirudi jioni amenuna hataki hata kukusalamia na ukiuliza tu balaa.
Tupe uvumilivu ee Bwana.

9. Anajaribu ku match nguo na hereni na akiona hazifanani abadili nguo sababu tu ya hereni.
-Teremka uwashike mikono yao baba.

10. Mkitembea barabarani inabidi ukae upande wa barabara eti wewe ni mwanaume ukigongwa na Gari haina noma.
-Ee baba tuepushe na hiki kikombe ulisema hawa ni wasaidizi wetu lakini tumekuja kuwa wafanyakazi wao.

Amina Mungu tupe wepesi
 
Back
Top Bottom