Wanaume tunaojua mapishi tukutane hapa

Napenda kupika sana nikishindaga home lazima nipike vitamu mahanjumati na nipo vizuri, mwanamke atakaeolewa na mim kama hajui mapishi atapata tabu sana.
Tabu tena si ndio umfundishe nae awe mtalaamu.
 
katika kitu ambacho siwez fanya ni kupika masaa mawili mpaka matatu afu nakula kwa dkk 10 shenzii kbs
Masaa matatu una pika nini mkuu??

a labda una pika maharage, Ata hivyo sisi maharage tuna pika kwenye chupa ya Chai usiku kuamka siku ya tukio kama ume panga kula maharage kitu ambacho kina Nipa shida ni kula migahawani napenda kupika mwenyewe geto
 
Unapikaje maharage kwenye chupa ya chai?
Mtaalam mmoja alisema, unasafisha vizuri kiasi cha maharage unayotaka kupika kwa siku hiyo kisha unataweka katika chupa ya chai. Unachemsha maji yachemke kabisa kama chai kisha inayaweka ndani ya hiyo chupa yenye maharage na kufunga mfuniko wake vizuri.

Hayo maharage ukiyafungia ndani ya chupa asubuhi mapema na kwenda kwenye shughuli zako, hadi jioni ukirudi utakuta maharage yako yameisha iva ndani ya chupa. Hasa kama chupa yako ni makini haipoozi haraka.
 
IMG_20201008_110248_605.jpg
 
Ishu sio kupika. Kuosha vyombo baada ya kula.
Mvivu namba 1 Mimi hapa..enzi hizo naanza maisha vyombo naosha ninapotaka kupika , basi shemej yenu alikuwa akija gheto .anapitiliza moja kwa moja kuosha vyombo vyooote panakuwa pasafiiii ..alaf namwambia pumzka..naingia jikoni ....alikuwa hadi anajiramba....ila yeye akiingia jikoni huwa huwa nakula mpk navimbiwa....yuko htr Mara 1,000,000 zaid yangu...
 
Mimi vyombo ni my first priority usafi wa nyumba nazingatia sana . Ukija kwngu utasema sio bachelor
 
Dahhhh.....
Kuna mada zingine hua zinanipa wakati mgumu sana kuchangia, eababu ya ukakasi wake...😎😎
 
Back
Top Bottom