Wanaume tuliowahi kulelewa na majimama/ wake za watu, tutoe ushuhuda hapa

Kwa experience yangu sijawahi kudhani kuna nwanamke atakulea au hata kukuhudumia halafu akawa na furaha.
 
Haha
Nimezaliwa Mbeya maeneo ya Kabwe miongo kadhaa iliyopita, nilibahatika kupata elimu yangu ya msingi na kisha sekondari hapo hapo mjini. Nilipomaliza sekondari (form 4), sikufaulu hivyo ikabidi nijiunge katika masuala ya ufundi Wa magari (garage).

Baadaye nikawa nishasahau habari ya kusoma na nikaridhika na kidogo nilicho kuwa nakipata, basi maisha yakawa yanasonga. Ninachomshukuru Mungu Mimi sikuwa mtoto tegemezi kwa wazazi wangu kwa sababu wakubwa walio nitangulia walikua wako vizuri kwa nafasi yao.

Basi kama unavyojua mambo ya sisi vijana tukipata visenti kidogo, nikaanza kuhisi kukaa nyumbani nabanwa sana, ikabidi nitoke niende kupanga, basi baada ya kujipangia chumba maisha yaliendelea.

Basi njia niliyokuwa napita kutoka geto na kwenda kazini kulikuwa na duka ambalo nilikuwa nafika mara kwa mara kupata mahitaji muhimu kama sabuni au mkate na vitu vingine (mabachela wananielewa).

Ndani ya hilo duka muuzaji alikuwa mama mmoja mrembo kwelikweli, ila sikuwahi kumuwazia katika angle ya mapenzi maana alinizidi sana kiumri ingawaje mimi pia nimejaaliwa mwili mkubwa kidogo.

Siku zikasonga ila kuna siku ilikuwa zamu yangu kununua umeme katika nyumba niliyopanga, na nakumbuka sikuwa na pesa yoyote kwenye simu hivyo ikanibidi nitoke nikaingize pesa kwenye simu.

Akili yangu iliwaza kwenda kwenye lile duka maana lina bango pia lilikuwa limeandikwa M-PESA, hatimaye nikafika ila nilikuta foleni kubwa sana hivyo mama mwenye duka akashauri niandike namba kwenye karatasi kisha ataniingizia ili nisisubiri sana. Basi nami nikaona ni wazo zuri hivyo nikafanya kama nilivyo shauriwa.

Baadaye pesa ikaingia na nikafanikisha kununua umeme. Basi zikapita siku kama 5 hivi nikiwa garage naendelea na mitikasi yangu meseji ikaingia "MAMBO"
nikajua tu huyu atakuwa ni demu ingawaje namba ilikuwa ngeni, najua ni ngumu kwa mtoto wa kiume kuandika ujumbe wa hivyo basi nikajichekesha si unajua tena kijana damu inachemka!

Niliiacha sikujibu ujumbe ule nikiwa na dhumuni la kuujibu baadaye nitakapo tulia nikiwa geto. Kweli usiku ulipo fika nilipo tulia kitandani, ikabidi nimtafute muhusika wa ule ujumbe, nilipo jibu tu ukaingia ujumbe mwingine uliosovyema "SIJATEGEMEA KAMA UNA DHARAU HIVYO"
Nilishtuka kidogo ila kwakuwa nilikuwa najua drama za wanawake nilijua mtu yule alitaka tuwe na mazungumzo ya aina flani, basi nami nilijiongeza kusherehesha mazungumzo yale.

Ajabu ni kuwa kadiri nilipohitaji kufahamu yeye ni nani kwa jina, akawa ànanipiga chenga, basi nami nikawa naenda naye taratibu. Basi siku zilivyozidi kwenda tukajikuta mawasiliano yetu yamekuwa kama wàtu wa karibu na wanaojuana vyema. Nakumbuka siku moja ilikua Jumamosi, hiyo siku sikuenda job hivyo nikawa nimelala tu nikaamua kumpigia, hakika nilizungumza na sauti nyororo iliyo nifanya nizidi kuwa na shauku ya kutaka japo kumuona mrembo yule.

Na ni hiyo siku akaniambia kuwa anaitwa JANE basi nilifurahi kumfahamu kwa jina pia nikapata nafasi ya kujitambulisha kwake pia, nilimuuliza tena namba yangu aliipata vipi akanijibu kuwa yeye alikuwa moja yawateja waliokuwa foleni ile siku nimeacha namba pale dukani ile siku nilipoenda kuingiza pesa, hivyo baada ya kuachwa namba yangu katika kile kipande cha karatasi aliikariri kwa kuwa alikuwa amevutiwa na mimi.

Duh! Nilistaajabu kidogo na pia nilipojaribu kukumbuka huenda kwa mbali nitaikumbuka sura yake lakini sikufanikiwa na ni kwasababu sikuwekea umakini kwa wateja niliowakuta siku ile.

Sasa ikawa muda wa kukaribishana majumbani kwetu; kama ilivyo desturi za Kiafrika, nilianza kwa kumpa ratiba yangu kwamba kesho yake pia ambayo ilikuwa Jumapili ningelikuwa nyumbani maana siyo siku ya kazi kwangu, basi akanijulisha kuwa atanijulisha iwapo angepata wasaa kunitembelea.

Basi nakumbuka ile siku nilitamani niwe na mamlaka ya kulishusha jua katika kiza kinene. Basi niliamka mapema sana na kufanya usafi kama wote huku kichwani kwangu nikijenga picha tofauti za kimuonekano za mgeni ninaye mngojea.

Majira ya kama SAA 1 usiku aliniambia yupo karibu na nyumbani kama nilivyo muelekeza basi na mimi nikatoka ili kwenda kumchukua, sikuamini nilichokiona kwa kuwa nilicho kiona kilikuwa tofauti na nilicho fikiria hapo kabla, nikaogopa sanaaa.

Ila sikuwa na namna ikabidi nimkaribishe geto nilicho shukuru giza lilikuwa limeingia hivyo hatukuonekana na mtu mpaka alipo ingia ndani. Shughuli, mtihani ulianzia hapo...

Nitaendeleza ushuhuda huu kesho, bandugu.
Hahaha ukiendelea unitag bro
 
Punguza ujinga ongeza werevu.
Dunia ya leo mtu una namba yake halaf unashindwa kujua jina lake!!?

Nikiwa na namba ya cm ya mtu na nikaamua kumfuatilia aisee nita come up na details zake nying sanaaaaa sio jina tu.INFORMATION AGE

NB: labda awe ame fake official formation zake.
 
Wewe kweli ni Chizi drama, yaani tangu novemba 11 hadi leo disemba 9 iyo kesho yako haijafika?
Ebu ukuje apa umalizie stori yako ya kizinzi
 
Eeeh endelea mzee baba, mabaharia tupo
Nimezaliwa Mbeya maeneo ya Kabwe miongo kadhaa iliyopita, nilibahatika kupata elimu yangu ya msingi na kisha sekondari hapo hapo mjini. Nilipomaliza sekondari (form 4), sikufaulu hivyo ikabidi nijiunge katika masuala ya ufundi Wa magari (garage).

Baadaye nikawa nishasahau habari ya kusoma na nikaridhika na kidogo nilicho kuwa nakipata, basi maisha yakawa yanasonga. Ninachomshukuru Mungu Mimi sikuwa mtoto tegemezi kwa wazazi wangu kwa sababu wakubwa walio nitangulia walikua wako vizuri kwa nafasi yao.

Basi kama unavyojua mambo ya sisi vijana tukipata visenti kidogo, nikaanza kuhisi kukaa nyumbani nabanwa sana, ikabidi nitoke niende kupanga, basi baada ya kujipangia chumba maisha yaliendelea.

Basi njia niliyokuwa napita kutoka geto na kwenda kazini kulikuwa na duka ambalo nilikuwa nafika mara kwa mara kupata mahitaji muhimu kama sabuni au mkate na vitu vingine (mabachela wananielewa).

Ndani ya hilo duka muuzaji alikuwa mama mmoja mrembo kwelikweli, ila sikuwahi kumuwazia katika angle ya mapenzi maana alinizidi sana kiumri ingawaje mimi pia nimejaaliwa mwili mkubwa kidogo.

Siku zikasonga ila kuna siku ilikuwa zamu yangu kununua umeme katika nyumba niliyopanga, na nakumbuka sikuwa na pesa yoyote kwenye simu hivyo ikanibidi nitoke nikaingize pesa kwenye simu.

Akili yangu iliwaza kwenda kwenye lile duka maana lina bango pia lilikuwa limeandikwa M-PESA, hatimaye nikafika ila nilikuta foleni kubwa sana hivyo mama mwenye duka akashauri niandike namba kwenye karatasi kisha ataniingizia ili nisisubiri sana. Basi nami nikaona ni wazo zuri hivyo nikafanya kama nilivyo shauriwa.

Baadaye pesa ikaingia na nikafanikisha kununua umeme. Basi zikapita siku kama 5 hivi nikiwa garage naendelea na mitikasi yangu meseji ikaingia "MAMBO"
nikajua tu huyu atakuwa ni demu ingawaje namba ilikuwa ngeni, najua ni ngumu kwa mtoto wa kiume kuandika ujumbe wa hivyo basi nikajichekesha si unajua tena kijana damu inachemka!

Niliiacha sikujibu ujumbe ule nikiwa na dhumuni la kuujibu baadaye nitakapo tulia nikiwa geto. Kweli usiku ulipo fika nilipo tulia kitandani, ikabidi nimtafute muhusika wa ule ujumbe, nilipo jibu tu ukaingia ujumbe mwingine uliosovyema "SIJATEGEMEA KAMA UNA DHARAU HIVYO"
Nilishtuka kidogo ila kwakuwa nilikuwa najua drama za wanawake nilijua mtu yule alitaka tuwe na mazungumzo ya aina flani, basi nami nilijiongeza kusherehesha mazungumzo yale.

Ajabu ni kuwa kadiri nilipohitaji kufahamu yeye ni nani kwa jina, akawa ànanipiga chenga, basi nami nikawa naenda naye taratibu. Basi siku zilivyozidi kwenda tukajikuta mawasiliano yetu yamekuwa kama wàtu wa karibu na wanaojuana vyema. Nakumbuka siku moja ilikua Jumamosi, hiyo siku sikuenda job hivyo nikawa nimelala tu nikaamua kumpigia, hakika nilizungumza na sauti nyororo iliyo nifanya nizidi kuwa na shauku ya kutaka japo kumuona mrembo yule.

Na ni hiyo siku akaniambia kuwa anaitwa JANE basi nilifurahi kumfahamu kwa jina pia nikapata nafasi ya kujitambulisha kwake pia, nilimuuliza tena namba yangu aliipata vipi akanijibu kuwa yeye alikuwa moja yawateja waliokuwa foleni ile siku nimeacha namba pale dukani ile siku nilipoenda kuingiza pesa, hivyo baada ya kuachwa namba yangu katika kile kipande cha karatasi aliikariri kwa kuwa alikuwa amevutiwa na mimi.

Duh! Nilistaajabu kidogo na pia nilipojaribu kukumbuka huenda kwa mbali nitaikumbuka sura yake lakini sikufanikiwa na ni kwasababu sikuwekea umakini kwa wateja niliowakuta siku ile.

Sasa ikawa muda wa kukaribishana majumbani kwetu; kama ilivyo desturi za Kiafrika, nilianza kwa kumpa ratiba yangu kwamba kesho yake pia ambayo ilikuwa Jumapili ningelikuwa nyumbani maana siyo siku ya kazi kwangu, basi akanijulisha kuwa atanijulisha iwapo angepata wasaa kunitembelea.

Basi nakumbuka ile siku nilitamani niwe na mamlaka ya kulishusha jua katika kiza kinene. Basi niliamka mapema sana na kufanya usafi kama wote huku kichwani kwangu nikijenga picha tofauti za kimuonekano za mgeni ninaye mngojea.

Majira ya kama SAA 1 usiku aliniambia yupo karibu na nyumbani kama nilivyo muelekeza basi na mimi nikatoka ili kwenda kumchukua, sikuamini nilichokiona kwa kuwa nilicho kiona kilikuwa tofauti na nilicho fikiria hapo kabla, nikaogopa sanaaa.

Ila sikuwa na namna ikabidi nimkaribishe geto nilicho shukuru giza lilikuwa limeingia hivyo hatukuonekana na mtu mpaka alipo ingia ndani. Shughuli, mtihani ulianzia hapo...

Nitaendeleza ushuhuda huu kesho, bandugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom