Wanaume tuache kujiendekeza

IKARAHANSI

JF-Expert Member
Jul 30, 2019
398
479
Kuna msemo maarufu miongoni mwa wanaume wapumbavu kuwa eti "WANAWAKE HAWAELEWEKI",huku ni kujazana ujinga na kuwajaza ujinga watoto wetu wa kiume kwa maana kabla hata ya kuja kwa maandiko matakatifu, asili pekee ilionyesha na kumfanya mwanaume kuwa kiongozi na msimamizi, ndio maana bila mwanaume kusimamisha uume wake, uzao hauwezi kuendelea na wanasayansi walikuja kugundua kuwa mwanaume (kupitia mwili wake na bila hiyari yake) ndiye anayeamua mtoto wa jinsia ipi azaliwe ( maana mwanamke ana cromosome x,x wakati mwanaume ana cromosome x,y). Hivyo kwa asili Mwanaume ni kiongozi wa familia (muamuzi wa mwisho) na ikitokea akakataa anakuwa amekwepa wajibu tu na hivyo anatakiwa achukuliwe hatua.

Tabia hii ya baadhi ya Wanaume wapumbavu kutowajibika ipasavyo ndiyo iliyopelekea baadhi ya wanawake kujipa mamlaka na kiburi cha kudai haki sawa na wanaume (kitu ambacho ni upotovu kwa asili), na baadhi ya wanaume wajinga ili kuhalalisha ujinga wao wakaamua kuanzisha msemo kuwa "MWANAMKE HAELEWEKI NA UKIONA UMEANZA KUMUELEWA JUA KIFO KINAKARIBIA" kitu ambacho ni uongo.

Wazee wa kipemba wana msemo wao unasema kuwa "MAPATANO NI NCHI KAVU, BAHARINI NI KUVUA TU" hivyo kwa Wanaume waerevu mapatano na mke mtarajiwa yanaanzia kwenye urafiki hadi uchumba (nchi kavu), mkiisha funga ndoa (baharini) ni kuvua tu. Sasa wanaume wengi tunafanya makosa kwenye mapatano (nchi kavu) kwa kuzingatia vitu visivyo na msingi mfano msambwanda/chura, rangi nyeupe, chuchu saa sita nk. na kuacha vitu vya msingi mfano tabia njema, ucha MUNGU nidhamu ya mtarajiwa, uvumilivu, utu wema nk. Matokeo yake mambo yakibadilika na kuwa mabaya ndani ya ndoa tunakuja na misemo ya kujihami kumbe wakati mwingine ni uzembe wetu ndo umesababisha hayo kutokea.

Rai yangu kwa wanaume ambao hawajaoa ni kuwa mjiandae kisaikolojia kwa maana FEDHA ni jibu la mambo yote, hivyo penzi la kweli na penzi la kitapeli yote yanahitaji fedha (akili kumkichwa), hivyo unatakiwa ujue kuwa wanawake na wanaume sote tunahitaji fedha kama huna tafuta kulalamika hakusaidii zaidi ya kukudhalilisha na ukiona hupati fedha basi achana na wanawake kwanza. (Simaanishi kuwa wanawake hawana upendo, wanao ila kwao kipaumbele ni ulinzi na usalama wao, hivyo Mwanamke kuolewa na Mwanaume asiyempenda lakini mwenye ukwasi, isikushangaze maana wao wanaangalia mbele)

Hivyo basi, kwa mujibu wa wanasaikolojia na wasomi mbalimbali walio elimika (Sio wasomi vyeti), ukiwa na utulivu wa akili Mwanamke anaeleweka. Kama Mwanamke uliyenaye humuelewi na umeishi naye zaidi ya miaka mitano bora umuundie tume ya uchunguzi na wajumbe wa hiyo tume iwe ifuatavyo:- Muuza urembo/Msafisha kucha, muuza nyama, Bodaboda, wenye maduka ya jirani, wauza genge na madreva tax/Uber nina hakika majibu yao yatakushangaza (Ila hii ifanyike pale utakaposhindwa kumuelewa hata baada ya kutuliza akili na kujihoji kwa kina)

Mwisho japo siyo kwa umuhimu tambua kuwa Mwanaume ni kiongozi kwa asili (Siyo kwa kuwa misahafu imeandika bali tulikuwa hivyo kabla ya misaafu kuja), hivyo tunatakiwa kujua kujiongoza wenyewe kwanza na pia tunatakiwa tujipende kwanza sisi wenyewe ili iwe rahisi kuwaongoza na kuwapenda wenzi wetu na familia kwa ujumla,tabia ya kujiliza-liza bila utaratibu na kuwalaumu wanawake kwa makosa ambayo tumeshindwa kuyazuia kizembe ni kujidhalilisha. Ukikosea ni bora kuomba msamaha kuliko kutafuta mtu wa kumtwishwa zigo lako.

UKIONA HUMUELEWE MWANAMKE ULIYENAYE JUA WEWE NDIYO HUJIELEWI KWA MAANA JUKUMU MOJA WAPO LA KIONGOZI NI KUWAJUA NA KUWAFAHAMU ANAOWAONGOZA.

#Mitandao ya kijamii
 
Karibu Chief!! utoe japo neno kwa Wanaume wenzetu!!
Ulichokisema hapo juu kinaukweli kwa asilimia kubwa, miaka ya sasa wanaume tumekuwa LAINI SANA, kwasababu kipindi cha nyuma wazee wetu walikuwa majabali kwelikweli, maamuzi yalitoka kwa wakati bila kujali ila kipindi hichi chetu sio siri vijana tumepoteza dira sana .

Mwanamke ni mtu wa kuongozwa kweli na inapaswa mwanamke akusikilize na akuheshimu ikitokea mwanamke hafanyi mambo tajwa hapo juu hana maana ya kuendelea kubaki kwako hatakama ana umbo au sura ya namna gani Mwanaume lazima uwe na maamuzi magumu na msimamo.

Pili utandawazi umeathiri sana kizazi cha sasa wanawake wamekuwa kama wanaume , hushindana na wanaume kwa kila nyanja kwanzia uchumi , elimu nk..... hivyo mwanaume unapaswa kuchagua kwa makini sana mtu utakaye mwongoza katika safari yenu.
 
Ulichokisema hapo juu kinaukweli kwa asilimia kubwa, miaka ya sasa wanaume tumekuwa LAINI SANA, kwasababu kipindi cha nyuma wazee wetu walikuwa majabali kwelikweli, maamuzi yalitoka kwa wakati bila kujali ila kipindi hichi chetu sio siri vijana tumepoteza dira sana .

Mwanamke ni mtu wa kuongozwa kweli na inapaswa mwanamke akusikilize na akuheshimu ikitokea mwanamke hafanyi mambo tajwa hapo juu hana maana ya kuendelea kubaki kwako hatakama ana umbo au sura ya namna gani Mwanaume lazima uwe na maamuzi magumu na msimamo.

Pili utandawazi umeathiri sana kizazi cha sasa wanawake wamekuwa kama wanaume , hushindana na wanaume kwa kila nyanja kwanzia uchumi , elimu nk..... hivyo mwanaume unapaswa kuchagua kwa makini sana mtu utakaye mwongoza katika safari yenu.
Chief umeongea ukweli kabisa, Vijana wengi wa kiume wamekuwa laini na utandawazi umewadumaza kwa kuwaaminisha kuwa eti, ulaini na kulia lia mbele za wanawake ndio usasa na kwenda na wakati. Lakini kiukweli Wanawake wanaojielewa wanataka kuwa na mwanaume mgumu na imara anayejiamini anayeweza kuonyesha dira nani wapi familia inatakiwa kwenda.

Mwanamke anajivunia kuwa na mwanaume anayejua mahitaji yake na kuyahangaikia hata kama atakwama lakini juhudi zionekane.
 
Back
Top Bottom