Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,295
- 33,079
Je utafanya nini wewe kuhusu hii Aya hapa:
Al-Nuur 63 ''Let those who violate his (Muhammad peace be upon him) command beware of being struck by Fitna or by a severe punishment''
Mkuu umetowa aya lakini umeielewa lakini Aya inavyosema? Nankuu
24. SURATUN NUR Aya 63 63. (Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu anawajua miongoni mwenu wanao ondoka kwa uficho. Basi nawatahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu.)
hii Aya uliyotowa mkuu Sideeq haiusiani na Mambo ya Kufuga Ndevu. Aya uliyotowa inahusiana na aya ya juu yake hebu nikusaidie vizuri,maana nakuona hujuwi kusoma vizuri Qur'ani kazi yako wewe ni ku COPY na Ku PASTE unakuwa hodari sana Mkuu Sideeq. hebu soma aya hii ya juu pamoja na chini
24. SURATUN NUR AYA 62 NA 63
62. Hakika Waumini wa kweli ni walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake; na wanapo kuwa pamoja naye kwa jambo la kuwakhusu wote hawaondoki mpaka wamtake ruhusa. Kwa hakika wale wanao kuomba ruhusa, hao ndio wanao muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na wakikuomba ruhusa kwa baadhi ya kazi zao, mruhusu umtakaye miongoni mwao, uwaombee msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemmu
Nakutafsiri Vizuri Anasema Mwenyezi mungu subhana wataala (Waumini kweli) maana yake ni wale Waislam wanaomuamini Mwenyeezi Mungu na Mtume wake Muhammad Swala llahu alaye wasalaam. Wanapokuwa pamoja na Mtume kwenye Mkutano wa mambo ya Dini hawaondoki mpaka wamuombe Mtume ruhusa na awape ruhusa kwa anaye Mtaka. Hao Mwenyeezi Mungu amesema hao ndio Waislam wa kweli. Sio tu ukitaka kutoka katika Mkutano wa Mtume kwa ruhusa yako. Unakuwa kama umemvunjia heshima Mtume. Haya inayofuta ni hiii
63. Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu anawajua miongoni mwenu wanao ondoka kwa uficho. Basi nawatahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu.
Nakutafsiria hii aya ya pili,Anaposema Mwenyeezi mungu nanukuu (Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi) Unajuwa amekusudia kitu gani? Anapokuwiteni Mtume wa Mwenyeezi Mungu tofauti na mnapoitana nyinyi kwa nyinyi Waislam. Kwa sababu Mtume yoyote wa Mwenyeezi Mungu anacho cheo kikubwa kupita Binadamu yoyote hapa duniani. Na hutakiwi kupinga amri ya Mtume Akikuita lazima uende kwake Mtume. Sasa aya hiyo uliyoitowa inafutana na hiyo ya juu yake, haiusiani na mambo ya Kufuga Ndevu jamani Acheni kutowa aya wakati hamna ushahidi wowote ule.
Toeni aya inayosema kuwa Lazima kila Mwanamme aliye muislam Afuge ndevu nataka Mutowe aya hiyo sio kuleta Mashindano ya Ligi Simba na Yanga Leteni Ushahidi wenu.