Wanaume, siyo wakati wote ni wa kuwalaumu wanawake, kuna wakati sasa ni wa kuutumia 'uanaume' wenu

Carleen

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
7,503
25,116
Hi guys,

Ni imani yangu mmekuwa sawa watu wa Mungu..!

Kuna hii issue huwa inatokea mara kwa mara, wanaume hulalamika kuwa baada ya Ndoa, Cheo, Elimu ama Uwezo wa kifedha (hasa kuwazidi waume zao) hushangaa asilimia kubwa sana ya wanawake hubadilika kitabia, huwa na dharau na 'qibri' flani hivi ambacho mwanzo hakikuwepo.!

Hapa ndipo wanaume huanza kutuponda sana wanawake na kutuona viumbe wa ajabu na ndiyo mwanzo wa kutunukiwa majina yasiyo staha..!

Mnachosahau wanaume ni kuwa, kiasili mwanamke hakuumbwa kuwa na 'mamlaka', sababu kiukhalisia mwanamke hawezi control hiyo 'power', mara nyingi huwa hiyo mamlaka inamzidi nguvu, ndipo haposa mnaanza kuona mwanamke anabadilika na kuanza kuvimba,

Na si kwamba eti 'ataplan' kuwa sahii nianze kuvimba, Hell No'..! In a very automatic way, kuna kitu kina trigger kwenye akili yake kuwa 'wewe ni mkubwa sana, kuna namna unapaswa kuheshimiwa na hawa wote wako chini yako na hakuna wa kukuambia lolote kwani hakuna aliye kama wewe'..!

Lilipaswa kuwa ni jambo la ku control that 'overgrowing ego', lakini sangapi wakati huo uwezo wenyewe wa ku-control unajipata hauko nao?? Mwisho wa siku hiyo ego inakomaa hapo sasa hakuna atakayeweza kukuambia kitu tena mara nyingi kama ilikuwa ni Ndoa huishia kuvunjika kwani mafahali wawili kamwe hawakai zizi moja..!

Kuna ile namna mke anaanza kukuvimbia mpaka wewe mumewe, unashangaa hichi kiburi katoa wapi mbona hakuwa nacho kabla.? Kumbe tayari ile kujua tu 'Mimi ndiye Mkewe tena halali wa Ndoa', hiyo tu itamfanya mwanamke 'avimbe' tena mapema sana.! Yaani tunataka uielewe 'mamlaka ya kuwa mke tuliyonayo' kila mtu ajue Mimi ndiye mke wake na aheshimu hilo, kwanza ukifahamu kuwa ni mke halali tunatamani hata ushtuke japo utetemeke kidogo (kinda funny eeh!?)..!

Hapa pia ndipo pahala mliambiwa muishi na mwanamke kwa akili, ile akili sasa ikuwe applied na hapa..!!
Jitahidi kumkumbusha mwanamke wako nafasi yake mara kwa mara, kuwa hata kama dunia itageuka kichwa chini miguu juu bado nafasi yake ni ile ile yeye ni mke tu hakuna kitakachobadilisha hilo hata akiimiliki dunia yote.!

Tutabishana hapa na baadhi ila hata msipoamini hili nadhani mnajionea mengi yanayoendelea huko duniani, mwanamke hakuumbiwa kuwa na mamlaka kubwa kumliko, na akiwa nayo pengine awe na muongozo toka kwa mwanaume anayemuheshimu tofauti na hapo, we're doomed, real doomed..!

Enweiz, sijui hata nilikuwa nawaza nini, hebu mkuwe tu na weekend iliyobarikiwa..!
 
Dunia ipo busy kumpa nguvu(empower) binti, human rights kwa sasa zimelalia upande wa binti.

Tumesahau kuwa kumpa nguvu binti kunaendana na kumsaidia kijana wa kiume kujua nafasi yake katika jamii, jinsi ya kuishi na huyo binti.

Na bado, vijana watazidi kulia sana coz ni kama wanaona wamenyang'anywa nafasi yao, hawajafundishwa kuishi na huyu binti.
 
Ya kwamba tunafundishwa na mwanamke huyohuyo..😂

Dealing with human behavior isn't easy!, wengine wanaendeshwa na mambo yanayowapata wachache wanajua hili na wachache wanaweza ku control hili.

Kuna mapenzi,Kuna kupata mpenzi na Kuna kupata mpenzi wa kukufaa!.
Akili ya mwanadamu kuishi nje ya hulka yake ni kazi sana, wanawake wengine hupenda tu kupanda watu kichwani aidha kwa kujua au kutokujua!.
Kila kitu kinachokuja kwenye maisha yako kina namna fulani ya kuibua hulka zako!,Sasa ni upeo wako wa akili ktk kutambua na ku handle jambo husika.

Elimu,kazi na pesa bila kuangalia jinsia hivi vyote huwabadili watu ila kwa mwanamke humbadili zaidi maana wanawake ni walimbukeni wa hivi vitu na ulimbukeni huo ni kwasababu mwanzo hivi vitu havikuwa chini yao!.
Mpaka bongo zao zitakapoweza kumudu ndio watatulia!.

Mweka mada umeandika kwa upeo wako isipokuwa haujaandika kutushauli tufanye nini!!,kutumia uanaume wetu inaweza kuwa na tafsiri nyingi kila mtu na ufahamu wetu na usifikiri kila mwanamke utakaekutananae utafanya vilevile!..

Nijuavyo ukijua akili ya mwanamke inavyofanya kazi umefaulu point moja, ukiweza ku handle/kontro utafaulu point ya pili,tatu kwanini ujishughulishe na ubongo wa mwanamke!!!!!..😄

Hicho cha mwisho nimeandika kifumbo.
 
Unayksema ni kweli. Lakini nafikiri matatizo yanaanzia mbali kabisa. Kwenye ile courtship na uchumba na mahusiano beforr ndoa ndo wengi wanapokosea.

Unapopata mwanamke, hata kama alikua na watu wengine befor you, ni muhimu kuformat hard disk ya akili ake na uweke ambayo inaendana na utaratibu wako. Carleen amesema ukweli, wanawake hawakuumbwa kuweza kucontrol power kubwa. Hivo ni jukumu lako kama mwanaume kumuonyesha njia inayopasa kufuatwa ndani ya maisha yenu. Mwanamke anaejielewa lazima atafuata, na pia ukimpa room for improvement mtatengeneza utaratibu mzuri sana unaofaa ndani.

Shida n kwamba tukipata mwanamke submissive tunavimba kichwa na kusahau kumtreat kama binadam na mpenz, tunaanza kumtreat kama kijakazi. Lazma akipata nguvu alete kisebengo kikali.

But mwanaume akiweza kusimama na kumuonyesha mwanamke kua yeye mwanaume ni kiongozi na mkewe ni msaidizi wake, they all make a great team
 
Hi guys,
Ni imani yangu mmekuwa sawa watu wa Mungu..!

Kuna hii issue huwa inatokea mara kwa mara, wanaume hulalamika kuwa baada ya Ndoa, Cheo, Elimu ama Uwezo wa kifedha (hasa kuwazidi waume zao) hushangaa asilimia kubwa sana ya wanawake hubadilika kitabia, huwa na dharau na
Mtulipie mahari na kutuoa kabisa maana ndicho kilichobaki kwa sasa
 
Back
Top Bottom