wanaume nyinyi siwawezi...kha.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wanaume nyinyi siwawezi...kha....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by vkeisy2006, May 7, 2010.

 1. vkeisy2006

  vkeisy2006 JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 230
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  hii nimeitoa kwenye blog 1 hivi.....mshaurini huyu....mi nampelekea comment zenu......

  MUME WANGU ANANITEGEMEA KWA KILA KITU- LAKINI HAJATULIA HATA KIDOGO- NIMWACHE?  Du! jamani kuna wanawake wenzetu wanashida sana jamani, hebu soma hii, maana mimi imenisisimua sana, na imeniumiza pia, ametuma ndefu sana, nimejaribu kuedit kiasi, but soma kisha mshauri, yani nawaza kama ndio ningekuwa mimi sijui ingekuwaje, yani sipati majibu maana kichwani yanakuja mfururizo kama majibu kumi hivi but yote yana madhara at the end, inasikitisha sana
  [​IMG]
  Nimeolewa, miaka mitatu iliyopita, lakini nilimkuta mume wangu anawatoto watatu, binti wa miaka 16, na wa miaka 10 na miaka 6, mimi sikuwa na mtoto hata mmoja, mama wa watoto hawa alifariki.  Tumefunga ndoa ya kanisani, sikubahatika kuzaa mapema, ila kwa sasa ndio nina ujauzito wa miezi saba, Nilimpenda sana mume wangu,Mimi nafanya kazi nzuri tu, ila mume wangu hana kazi yeyote ile, maana alifukuzwa, hivyo nafanya dili zake tu za pembeni zinazofanya aishi hapa mjini, aliponioa alihamia kwangu, maana yeye alikuwa amepanga, mimi nimejenga, hivyo tulikubaliana aje kwangu na nilikubali aje yeye na familia yake,
  nilimtafutia biashara, mradi tu! Asiwe anakaakaa nyumbani , akafungua duka la nguo za kiume huko mjini, na bila hata uoga alimuweka girlfriend wake awe ndie msimamizi na muuzaji, yeye ndie controller wa kila kitu pale. nilipogundua niliifunga ile biashara. Toka siku ile niliapa kutomsadia lolote lile.


  Ni Malaya kupita kiasi, nilishawahi kumfumania na wanawake zaidi ya watatu, kuna mwingine alimpangishia na chumba akawa anaishi nae kutwa nzima, na hivi hana kazi akawa anatoka asubuhi anaenda kushinda huko, jioni anarudi kulala kwangu, nilipogundua nililia sana violet mdogo wangu niliumia sijapata kuumia vile katika maisha yangu, nilimpokonya gari nililokuwa nimempa, nikawa simpatii hata pesa. sikuona maana ya kumjali mtu asieniheshimu, lakin kama mjuavyo mapenzi tena, nikaamua kumrudishia gari ili watu wasihis kitu kwa kuona limepaki nayeye anatembea kwa miguu.


  [​IMG]

  Nashukuru Mungu watoto hawa wananiheshimu na kunipenda sana, watu wengi wanajua kuwa nimewazaa mimi mwenyewe, nami nawapenda sana, Nilimfumania kabla sijabeba hata mimba, sasa mwezi uliopita nimepigiwa simu na mwanamke mmoja akanitukana sana, isitoshe amenitishia kabisa maisha yangu, anasema ataniroga nitazaa mbuzi, na maneno mengine makali sana, yani hadi huwa najuta,


  Violet, hapa nilipo mimi ndio kila kitu, najua ni ngumu sana kuamini kuwa mimi ndie ninaesomesha hadi watoto wake, nawalipia ada na kuna mmoja huyu wa kati, nimempeleka boarding namlipia mimi, huyu mkumbwa nae yuko private (secondary) nalipa mimi. huyu mdogo mimi pia nimempeleka Tusiime ( international) namllipia mimi, moyo wangu unaniuma sana, kwanini anitese hivyo? Inamaana hanithamini mimi wala wema wngu kwa wanawe?


  Wale watoto ni damu yake yeye, watamsaidia yeye sio mimi? Niliahidi kuwasaidia kwa moyo wangu, maana nilipoolewa mimi nilikuta watoto wana hali ngumu sana, waliona kama wamepata mkombozi wao, Sasa yeye nikimuuliza kwanini ameshindwa kufanya hata kwa siri tu umalaya wake, mimi nisijuwe, kwanini ananidharirisha, mimi nampa heshima zote, nampa matumizi yake binafsi, namlelea watoto wake, gari namtilia mafuta, lakini anakwenda kuwapakia wanawake wengine, wanapanda kwenye gari yangu,

  hana cha maana anachonijibu ninapomuuliza, yeye anasema hawajui, mimi nakataa maana nilishawahi kukuta hata sms za mapenzi, anawatambua maana kuna mambo yangu mengi ya ndani tunayopanga mimi na yeye tu chubmani, cha ajabu huyo mschana anayafahamu, hilo ndilo linalonipa hofu, wasije wakayatumia hayo kuniumizia kiumbe changu, sasa naomba mnishauri, nifanye nini? Nimfukuze?


  Moyo wangu umechoka sana jamani, moyo unaniuma sana, kwanini iwe hivi? Hali hii hata kujifungua bado, nimeanza kutishiwa eti nitazaa mnyama(mbuzi) sina hata nilichowakosea,


  Ananitia aibu kwa majirani, maana mtaa mzima wameshamjuwa kuwa yeye ni malaya, cha ajabu anachukuwa visichana vya ajabu ajabu, havina kazi wala pesa, vinamtegemea yeye kwa kila kitu. vikorofi, midomo imejaa matusi, na hata elimu havina, aibu hii mimi hadi lini? inaniuma, nimekuwa nikilia kila siku!

   
 2. mabina

  mabina JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Pole sana dada kwa mkasa ulionao, ni majaribu makubwa sana hata ss wanaume anatudhalilisha labda anapepo la ngono huwezi jua,ila usiwaache hao watoto watatabika sana. Nakupa pole tena sana mno. Usilifmbie macho hebu jaribu kuwaeleza hata wazazi wake.
   
 3. Celebrity

  Celebrity Member

  #3
  May 7, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili naro jalibu
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mtimue haraka sana.......

  mwisho atakuletea na maradhi. .........labda yuko addicted maana wenye ugonjwa wa tiger woods ni wengi.
   
 5. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,481
  Likes Received: 2,082
  Trophy Points: 280
  achana nae au mfukuze kisha akija kuomba msamaha msamehe ukiendelea kumwendekeza atakuletea hao machangu mpk ndani
   
 6. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hana adabu huyo ndugu yangu, nikweli hakuna mwanaume perfect, ila cha msingi heshima ndo inayohitajika hapo. Wewe achana naye na hao watoto wake wake mwache akawalee wenyewe, ukipenda msaidie tuu kwa ajili ya upendo wa hao watoto wakiwa mikononi mwake. Duh, pole sana mwenzetu.
   
 7. vkeisy2006

  vkeisy2006 JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 230
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  avatar...hahahahahahah
   
 8. G

  Grace New Member

  #8
  May 7, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Mungu wangu! yaani wanaume wa aina hii wapo wengi sana, hivi leo kuna rafiki yangu ametoka kunisimulia kisa kinachofanana na hiki. Cha kufanya sio kuendelea kumuonea huruma huyo amfukuze bila huruma, ila hao watoto aendelee kuwasaidia Mungu atamlipa. Lakini inauma sana!
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  May 7, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ama kweli ukilia kwako kuna moto, jua kwa mwenzio kunateketea loh!!

  Dada ujumbe wangu kwako ni huu
  1.A man has the power to love a woman in a way she never been loved,and yet hurt her with the same intensity.

  2.A man has the power to treat a woman like a queen then turn around and make her wish she was never born.

  3.A man has a power to make a woman cry with happness and joy then turn around make her cry with hurt and anger.

  4.Aman has the power to let a woman feel free and wanted but also feel disgusting and unworthy

  5.A man has the power to look at woman in her face and tell her he loves her,but turn around and sleep with her best friend.

  6.A man has a power to make you fall in love with him within days,and hate him within minutes.

  7.During sex a man has the power to make a woman feel like she is in heaven and afterwards makes her feel like a *****.

  8.A man has the power to change a woman from having goals,
  to living his goals instead of her own.


  Why is it that men have such power?
  They have so much power because we give it to them,the power of a man wouldn't mean anything without a woman.

  So ladies when times are hard between you and your man and you realize that he treats you bad remember that he can only do what you allow.

  Source: Dina Marious
   
 10. T

  Tall JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.asimtimue.........wasaidiane kulea mimba
  2.huo umalya wa huyo jamaa ndio uliosababisha na yeye akaolewa.(sio kwamba naunga mkono umalaya)
  3.ilipasa amjue kwanza kabla ya kukubali ndoa.
  4.unaweza kumpa kila kitu,mpenzi wako na bado ukasalitiwa.
  5.huyo hampendi anachopenda ni mali.
  6.mwambie shoga yako kuwa hilo gari si tu kwamba anapakia wasichana wake ila hata matusi wanafanyia humohumo,kama anabisha basi azikague vizuri seat za gari.mnyang'anye,endesha mwenyewe au liuze.
  7.yaelekea mumewe alimuua mkewe kwa ukimwi.......mwambie akapime.
  8.huyo akishakufilisi atakuua kama si kwa virusi basi hao wapenzi wake watakutoa roho.
  9.wasichana wake wanaweza kuharibu mimba yako.usigombane nae.subiri uzae kwanza then action
  10.huyo jamaa ana pepo la ngono.jini mahaba.mwombee limtoke.
  11.kuwa mople na jifanye mjinga,kusanya ushahidi wa kutosha. Baada ya kujifungua mfukuze,mpangishie chumba/vyumba akaishi huko na wanae.lakini usiache kuwatunza watoto.
   
 11. E

  Erica Furaha Member

  #11
  May 7, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hana huruma hata kidogo naasipoangalia atamuuwa kwa ugonjwa H I V achananae mpe rabo yake aende kwa hao malaya wake ,usimuonee huruma hata kidogo
  lakini naomba uendelee kuwalea hao watoto
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,608
  Trophy Points: 280
  Mmhhh! Mpe pole nyingi sana. Mwambie kama ataamua kuivunja ndoa yao hao watoto asiwaache solemba ajitahidi tu angalau wamalize shule. Ana moyo mzuri sana wa kusaidia hata wale wasiomhusu.
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,608
  Trophy Points: 280
  MJ1 siyo wanaume wote wako hivi ni baadhi tu, wengi wako tofauti sana na haya yaliyoandikwa hapa.
   
 14. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Hii noma..!
  huku unasikia mwanamke kafanyiwa hivi .. huku mwanaume kafanyiwa vile..
  mie nashindwa kuelewa haya mapenzi jamani yaani inakuwa kama unacheza kamari vile..!
  Yaani huyo jamaa hana tofauti na mke wa jirani yangu hapo ndio pananichanganya kabisaaa.!

  ingekuwa inawezekana tungewabilisha bwana apewe huyu bibie na huyo mke wa jamaa aje kwa jrani yangu.
   
 15. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  imeandikwa...Mungu anakuchukia kuachana,
  lakini kama mme/mke anakufanya umtende dhambi Mungu,
  ni heri ukatengana naye, lakini kama tamaa ya mwili
  ikikujia ni heri ukammrejea mme/mkeo, kwa maana huna
  ruhusa ya kuoa tena, maana mkeo/mmeo yu hai, nawe
  umekwisha fungwa kwa ile ndoa, ukiolewa/ukioa tena
  mkeo/mmeo angali hai, adhabu ya uzinifu na uasherati i juu yako,
  heri kuinusuru roho yako kwa mambo ya mwilini, maana mwili ni wa
  duniani na roho asili yake mbinguni, Mungu akuwezeshe
   
 16. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kosa kubwa ulilofanya ni Kukubali kuolewa nae wakati bado humjui vizuri,nadhani uliharakisha sana.Lakini usikate tamaa,na kwa hali uliyofikia peke yako hutaweza kutatua tatizo hilo.Mshirikishe Mungu jambo hilo.Huyo mumeo HAJITAMBUI hivyo usimlaumu sana.Tafuta msaada wa kiroho wa kusaidia kumtoa kwenye mateka ya adui.Neno la Mungu katika kitabu cha YEREMIA(nimesahau sura)n inasema''.....Mungu ameumba jambo jipya duniani,mwanamke atamlinda mwanaume....."Inakubidi usimame imara katika kumwombea mumeo.Tafuta mchungaji au mtu unayemuamini amesimama vizuri na Mungu na mwaminifu ili asimame na wewe.Na jambo lingine jitahidi uwe unatumia kondom wakati wa tendo la ndoa au lisitishe kwa sasa ili kuepuka maambukizi ya HIV kwa vile mumeo haaminiki.Endelea kuvumilia,usife moyo Mungu anaweza mambo yote.
   
 17. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  [​IMG] Originally Posted by nyivonduma sir [​IMG]
  hili naro jalibu

  MC Hammer - Hiyo ikiitwa : You can't TOUCH THIS!
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wema usizidi uwezo,

  samtaims siwaelewi wanawake wa namna hii, jitu halina kipato, jitu lina watoto watatu, jitu lina umalaya uliokubuhu... Mtu bado unaomba ushauri, ushauri gani kama sio ujinga kung'ang'ania ukimwi tu!!!
   
 19. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  [​IMG]yaani imenifanya nicheke ka mwendawazimu,,,,,duh jamaa naona anayarudi
   
 20. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mabreka hayoo
   
Loading...