Wanaume! Nimewaita, pimeni DNA watoto wenu wanapozaliwa

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,146
11,192
Niliwahi kuweka uzi hapa kuwa mpenzi wangu nilimkuta na mimba isiyoeleweka wakati nilitumia Condom kwa usahihi, akawa anataka kuitoa, nikamwambia hakuna kutoa la sivyo ningempeleka polisi, alichokuwa anakimbilia kuitoa alicheza rafu na alikubali mimba sio yangu baada ya kumbana aseme ukweli.

Sasa nyumba ya jirani yangu ana binti ambaye alikuwa anatabia za kuwapanga wanaume bila kujuana sasa, alipata mimba akajifungua lakini anachukua hela ya matunzo kutoka kwa wanaume watatu bila ya wao kujuana na wote wanatuma matumizi na kila mwanaume anakuja kwa kupangiwa muda na huyo binti na huu uhuni anaufanya kwasababu anaishi na mama yake tu na mama nae ni wale wale, Shangingi la zamani.

Nimechokaa wakuu baada ya kupata hizi habari, jamani ukiona unaishi na mwanamke haeleweki jua utakuja kulea damu isiyo yako, wanaume tuamke jamani tunapigwa vipanga na hawa wanawake, ukiona mtoto ulieambiwa ni wako kafikisha miaka miwili hana sura yako wala ya dada zako au shangazi zako hata ya mama yake haipo, kapime DNA.

Wanawake sasa hivi wanapanga wanaume bila kujuana, ikitokea mimba inapelekwa kote kote na anakula matumizi, ukiishi na mwanamke mcharuko na akizaa mtoto kapime DNA tu, now tupambane na hivi viumbe tuepuke kupigwa.

Haiwezekani mtu ulee mtoto sio wako kwa miaka 18, hiyo hela ni heri ungenunua tofali ujenge, hamna kitu kinauma kama kutoa milioni moja unamlipia mtoto shule alafu unakuta damu sio yako, mwanamke anakuchora tu.
 
Acheni undezi, unajua gharama za kumlea mtoto ambaye katoka kwenye ukoo mwingine au kazaliwa na baba mwingine.

Unajua tabia atakoonyesha ukubwani au uwezo wake kiakili, mtajikuta mnalea mazezeta kwa undezi kama huu.

Kila mtu awe na uhakika mtoto ni wake vinginevyo lea watoto wa ndugu zako au kaasili watoto yatima itajulikana sio wako.
 
Kiafrika mtoto wako ni Yule ambae mama kamwambia wewe ndo Baba yake..

DNA sio utamaduni wetu...

Na kisheria mtoto ni Mali ya Jamhuri ya Muungano..wewe Baba au Mama ni mlezi tu
Ukichunguza alacho nyuki, hutaonja asali. Na Wahenga walisema, kitanda hakizai haramu. Tukianza kuchunguza vinasaba vya watoto wanaozaliwa na wapendwa wetu hatutabaki salama.

Ogopa hasira za baadhi ya wanaume ambao wanaweza kuwafanyia wenzi wao kitu mbaya baada ya kugundua hayo matatizo ya kubambikwa watoto wasio wao. Ogopa wivu wa mapenzi.
 
Back
Top Bottom