Wanaume ni kama mbwa linapokuja swala la kujihami…!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
men.png

Kama umeshawahi kufunga mbwa au kumchunguza, utagundua kwamba, mbwa dume ana kawaida ya kutoa sauti yenye kuonesha kuumia au kuhuzunika au kuomba hasa anapokutana na mbwa mwingine ambaye anajua wazi kuwa ana nguvu kuliko yeye. Lakini mbwa huyo huyo ataunguruma kwa sauti ya chini inayotoka ndani, kama vile amekasirika sana au anajitambulisha kwamba anajimudu pale anapokutana na mbwa ambaye anajua anaweza kupambana naye. Ukiwakagua mbwa utabaini sifa hiyo ya kuunguruma kwa namna tofauti kutoka mazingira flani hadi mengine. Pale ambapo anaona atashinda pambano, huwa ana mlio mmoja na pale anapoona atashindwa mlio huwa mwingine.

Lakini je, hali kama hii iko kwa mbwa tu? Hapana, watafiti wanasema binadamu naye yuko hivyohivyo. Wanasema, linapokuja suala la namna tunavyojibu hali zenye kututisha, hatuna tofauti na mbwa. Mbwa anashusha sauti na kuunguruma kutoka kooni kama anaamini kwamba, mbwa anayemkabili hamwezi. Mwanaume naye huwa na kawaida ya kushusha sauti yake na kuzungumza kama vile sauti yake ni mali sana, anapokuwa akizungumza na mtu ambaye anaamini anammudu kimwili. Kama ilivyo kwa mbwa, hata wanaume, hali hii hutokea bila wahusika kujua. Najua hata wewe mwanaume unayesoma hapa unaweza kutilia mashaka jambo hili, lakini kama ukianza kujiuliza sasa hivi ndipo ambapo utagundua kwamba, kwa wale watu ambao unaona kabisa unawamudu au ambao unaamini hawatishii usalama wako kimwili, utazungumza nao kwa sauti ya kutokea kooni au ndani, yenye kuonesha kujiamini……….

Kwenye akili ya mwanaume tafsiri ya sauti hufanyika bila wenyewe kujua. Mwanaume anapomsikia mwenzake akizungumza kwa sauti iliyotulia na inayotoka ndani, huhisi kwamba, mtu huyo anayo nafasi kubwa zaidi kuliko yeye. Mwanaume humchukulia mwanaume mwenzao wa namna hiyo kama aliye na nafasi kubwa ya kumudu au kudhibiti. Kama umewahi kuchunguza utakubaliana name kwamba, wanaume huwa na kawaida ya kupandisha sauti na kuwa na sauti yenye mawimbi makali, pale wanapozungumza na mtu ambaye wanajua anawazidi hasa kimwili na kinguvu. Kama ni mtu ambaye wanaamini kwamba, wanamzidi, sauti zao huwa ni za kushiba na zinazotoka ndani……………….

Hii ina maana kwamba, bila wanaume wenyewe kujua, wanaposikia sauti iliyotulia, yaani inayotoka kwa wanaume wenzao huhisi kwamba, hao wenzao wanawamudu. Kumbuka hapa sizungumzii kupayuka au kuzungumza kwa kelele, bali nazungumzia utoaji wa sauti. Nikisema sauti kutoka kooni nina maana ya sauti nzito na yenye aina ya mamlaka (Vijana wa siku hizi huita Ki-besi) Lakini kwa sehemu kubwa, mamlaka au kummmudu mwanaume mwingine inapimwa zaidi kimwili kuliko madaraka au sifa nyingine. Hii ikiwa na maana kwamba, pale ambapo mwanaume anahisi kwamba, kimwili anamzidi au anaweza kumdhibiti mwingine, ndipo ambapo sauti yake huwa ni ile ya kutokea kooni. Haifahamiki ni kwa nini hasa wanaume hujikuta bila hiyari yao wakiwa na mabadiliko hayo ya sauti pale wanapokabiliana na wanaume wenzao, ambao ama wanajua kuwa wanawamudu au hawawamudu. Lakini wataalamu wanadhani, hali hiyo inatokana na maumbile ya wanaume kutaka kuoneshana tofauti zao. Bila shaka umeshawahi kuona hata kwenye sinema. Wale waigizaji ambao wanaamini kwamba, wanaweza kuwazidi nguvu adui zao, wanapozungumza nao, hutoa sauti zao kutokea kooni. Kuigiza kwa namna hii kunatokana na nadharia hii, kwamba, mwanaume mwenye nguvu hatoi sauti kali………………….
 
Hahahahaaaa ni kweli kabisa, ila linapokuja swala la Man Vs Woman, mara nyingi wanaume huwa wanawapa wanawake USHINDI WA MEZANI ili kudhibitish dhima kuwa mwanaume anaepambana na mwanamke AMEFILISIKA kisera na kijamii!!! With the exception of Wakurya na Walevi ofcourse
 
Asiri ya mwanaume alivyo umbwa, ni kama uonapo kitu cha ajabu, ghafla unapata nguvu au mbio za ajabu ambazo hua hauna, kwaiyo hii utokea, ingawa si kwa wote, kwa mfano mimi hua naongea kwa sauti ya upole sana na huku nikiwa makini ninapo kua katika hari ya namna hiyo, na unijengea kujiamini na mara nyingi hua na wabwaga.. wanao kuja na vi besi.. sijui wewe kaka Mtambuzi kwa upande wako.
 
ndo utasikia mbona unaongea sana kama mwanamke fanya vitendo,any way akili yangu imeongezeka jambo kwenye huu uzi wa baba wa fikra.
 
Hahaaaa !!!!!! Huu ni ukweli kabisa ila wakati mwingine hata jeuri ya pesa hufanya baadhi ya watu wabadirishe sauti pale wanapokutana na mtu ambaye anafahamu kabisa anamzidi kifedha
 
Mkuu Mtambuzi binafsi sikuwahi kulifanyia uchunguzi jambo hili na wala sikuwahi kufahamu kuwa kuna baadhi ya wanaume wenye tabia hizi.

Kupitia ka-uzoefu ka shule, nilizoea kuwaona wanaume wale wanyonge wanapokutana na wale ambao wanahisi hawawawezi kwenye ngumi, basi hawa wasio na nguvu walikuwa wanazungumza sana na kutema "Mkwala" kumtisha mwenye nguvu kuwa akithubutu kumgusa basi atakiona cha mtema kuni!!! Ktk hali hii, nilijikuta nikifikiria tofauti kuwa wale wababe ndo huwa hawaongei sana, na wale wanyonge ndo huongea sana na kutoa sauti za "kooni" kuficha udhaifu wao au kumtisha mtu wanayemwogopa.

Asante kwa mada hii, ngoja niendelee kufuatilia kwa ukaribu kubaini ukweli huu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mtambuzi heshima yako bana HorsePower uko salama mkuu
Ni kweli mkuu Mtambuzi hii hali ipo sana japo sio rahisi kuweza kuigungua
Asante sana kwa somo lako at least nimeelewa husababishwa na nini na kwa nini hutokea hivyo
 
Last edited by a moderator:
mtambuzi siamini sana lakini ukweli utabaki pale pale wewe mwanaume kama baba mwenye mji unatakiwa kuonyesha unaweza na unajiamini kwenye familia sio anatokea kichaa fulani anakufulumsha mbele ya familia yako tafuta hata upinde unaweza kumsaidia
 
Back
Top Bottom