Wanaume na wasifu wa kike ze origal comedy TBC1

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Naangalia ze origino comedy TBC1 ila natiwa kichefuchefu na jinsi msanii wa kiume alivyouvaa wasifu wa kike! Amefanikiwa lengo kuwa aonekane mwanamke, tena mrembo! Lakini hii maana yake nini kwa mtazamo na dhamira katika mzio wa ustaarabu wa watz? Je kweli huyu riziki ya Jalali? Sijui labda ni taaluma! Naomc ufafanuzi!
 
Rahisi tu badili channel, usiangalie chochote kinachokuudhi.
 
Ni sanaa tu...na nia ya sanaa ni kuburudisha...kuna mamia ya watu wanaovunjika mbavu na ile maneno...suppose ungemweka mwanamke pale, wala asingeweza ku'deliver kile walaji wanachotaka.
 
Ni sanaa na wasanii wanaweza kufanya lolote lile ili kufikisha ujumbe na kufurahisha.
 
Ukistaajabu ya mussa Filauni is on the way.The commedy ITV mbona mzuka tu, usijipe shida mzeee
 
Naangalia ze origino comedy TBC1 ila natiwa kichefuchefu na jinsi msanii wa kiume alivyouvaa wasifu wa kike! Amefanikiwa lengo kuwa aonekane mwanamke, tena mrembo! Lakini hii maana yake nini kwa mtazamo na dhamira katika mzio wa ustaarabu wa watz? Je kweli huyu riziki ya Jalali? Sijui labda ni taaluma! Naomc ufafanuzi!

Ndio maana wanaitwa ze comedy!!Kazi yao ni kufurahisha watu....na hiyo ndo style yao!!!Kama hupendi badilisha chanel....
 
haina haja ya kubadili chanel bali vumilia utajifunza kitu ndani yake kuna ujumbe wa kisani
 
Nilikua nawasikia tu hao jamaa mpaka jamaa yangu aliponitumia dvd ya maigizo waliyoonyesha kwenye TV.
Nilicheka mpaka nikajisahau, hasa pale wanaposema churaaaaa.
 
Ubunifu ni kitu kigumu sana, kama unahusika kwa namna moja au nyingine ndipo unaweza kujua namaanisha nini katika kusema hivi.
Cha msingi hapo ni kwamba ni vigumu sana kushona koti likavaliwa na kijiji kizima (kwa maana ya saizi) maana yangu hapo ni kwamba kisicho kupendeza wewe wengine burudani, ndio maana waswahili husema kuishi ni kuvumiliana.
 
hata mimi SIPENDI mwanamme aigize kama mwanamke au mwanamke aigize kama mwanaume. HAIPENDEZI. Watoto wanaharibika sana kwa kuiga!!!!
 
ubunifu = mwanaume kuvaa wingi na kurembua macho?

anaglia Mr Bean au Charle chaplin ah utasema naongelea watu wa nje basi angalia enzi za King majuto na mzee small ili kujua ubunifu maana ake nini
 
ubunifu = mwanaume kuvaa wingi na kurembua macho?

anaglia Mr Bean au Charle chaplin ah utasema naongelea watu wa nje basi angalia enzi za King majuto na mzee small ili kujua ubunifu maana ake nini

Weye kila kitabu na zama zake, enzi za majuto zimepitwa na wakati, hebu cheki movie ya WHITE CHICKS, sio mnaongea tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom