Wanaume na Wasichana wa Kazi za Ndani

Status
Not open for further replies.
Hebu fafanua zaidi kwani akina mama nao hawasababishi waume zao kwenda kutembea na wafanyakazi? Nitakupa mfano mwanaume anarudi kutoka kazini amechoka ukifika home haulizwi hali, matusi, chakula hajui hata kinapikwa vp, watoto wa shule wamesoma au la (kazi zote hizi hawajui kitu). Mfanyakazi anahudumia kila kitu isipokuwa kitandani.

Mr akiomba game kitanda anajibiwa na mke amechoka sana na kazi. Kimsingi sex is important as it releases frustration, tiredness etc sasa kama haipati kwa mkewe atapata wapi??? Akina mama naomba mtusaidie kwa hili maana linatokea katika nyumba nyingi if not majority of them.

Mnaweza kutulaumu sie wanaume kwa kutokuwa waadilifu but nanyie mnachangia kuyatengeneza mazingira ya kutamani mfanyakazi wa ndani either mkijua au bila ya kujua

Hayo yote uliyoyasema wala sio sababu za msingi za kukufanya wewe utoke na msichana wako wa kazi..kimsingi hakuna sababu yeyote ya kukufanya ufanye hivyo isipokuwa ni hulka tu ya wanaume tuliyojijengea ya ufuska.
 
Naona mkuu ulikutwa unajipongeza! Pole sana, acha siye tuendelee kufaidi mpaka na sisi yatukute...ng'ombe wa zizi moja na dume ni moja! unategemea nini?
 
...ehhh :eek: pole kamanda, ulimi umeniteleza tu katika harakati za kutoa mifano hai...

House girl ni mtu lakini sio wakudanganywa na boss wake..House girl ni kama mwanao hivyo ni vyme nae akaheshimiwa kama watoto wengine ndani ya nyumba.

...vipi kama huyo Hauz-geli akanogeza na kuolewa, bado ubaya ubaya tu? (kama Tiger wood vile)
 
Ni lazima ufuate kanuni:

a. Usiajiri msaidizi wa ndani wa kike ambaye ni mzuri kuliko mke wako
b. Usiajiri msaidizi wa ndani ambaye ni mwema kuliko mkeo
c. Usiajiri msaidizi wa ndani ambaye analala ndani ya nyumba yako na anasifa a na b
d. Usiajiri msaidizi wa ndani ambaye ukimwangalia unafikiria kilicho chini ya nguo zake
e. Kama wewe ni mwanamke/mke usimuache mumeo akubali kuajiri msaididi mwenye sifa hizo. Mtashindana na utashindwa.
 
Msisahau kuwa the opposite also happens, yaani mke kutembea na houseboy. Shame on those wives also.
 
Jamani akina baba kitu cha muhimu ni heshima kwani ukitembea na H.g heshima itapungua sana hasa kwa upande wa ndoa na pia anaweza akaanza kunyanyasa hata watoto
 
Ni lazima ufuate kanuni:

a. Usiajiri msaidizi wa ndani wa kike ambaye ni mzuri kuliko mke wako
b. Usiajiri msaidizi wa ndani ambaye ni mwema kuliko mkeo
c. Usiajiri msaidizi wa ndani ambaye analala ndani ya nyumba yako na anasifa a na b
d. Usiajiri msaidizi wa ndani ambaye ukimwangalia unafikiria kilicho chini ya nguo zake
e. Kama wewe ni mwanamke/mke usimuache mumeo akubali kuajiri msaididi mwenye sifa hizo. Mtashindana na utashindwa.

1.Uzuri ni subjective....fafanua - kuna uzuri wa sura ambao ni subjective, kuna uzuri uliojificha ambao hujakuonekana baada ya muda.Sasa utafanyeje kwenye hili? This applies to both men and women.

2.Hawa wasichana siyo wajinga kama watu wanavyodhania. Mke na mume kwa vyovyote lazima wanaweza kuwa na mapungufu yao, na msichana huyu anasoma mchezo wote unavyokwenda na ata capitalise on the weaknesses za mke...... sasa ukisema usiajiri aliye mwema kuliko mkeo mhhhh!!??

3.Bold 3, Huu ni mtihani.Kulala ndani na kuwa na sifa a u b.... hizi ndizo sifa ambazo humfanya hausigel aajiriwe! In short bold 1,2,3 huwa ni vigezo vya kumwajiri msichana.Hakuna mtu ataajiri msichana mkatili, asiyekuwa na sifa zozote aje amlelee watoto!u hausgel ni kazi jamani lazima iwe na vigezo.

4. Bold 4 ...hii nadhani ndio hasa chanzo cha tatizo - wanaume wengi wakware hujaribu kumvua mwanamke yeyote kwa mawazo/fikra na si ajabu kufanya hivi kwa hausigeli.
 
Wewe sema kuwa ni udhaifu wa wanaume lakini siyo usemi ati ni kosa la mke!

You can say this again and again!

Ni tabia tu ya baadhi yetu sisi wanaume. Tena ukikutana na mtu wa hivyo, utakuta ameshatembea/au kujaribu kuwarubuni shemeji zake (ndugu wa kike wa mkewe etc). Tabia ya ujinzi huwa haiangalii cha HG, bar-maid wala nani.

On the other note - wapo pia wanawake wanaotembea na houseboys wao. Ni tabia tu.
 
1.Uzuri ni subjective....fafanua - kuna uzuri wa sura ambao ni subjective, kuna uzuri uliojificha ambao hujakuonekana baada ya muda.Sasa utafanyeje kwenye hili? This applies to both men and women.

Uzuri wa ndani unaitwa wema; nazungumzia uzuri wa nje. Wanaume hatuvutiwi na uzuri wa ndani kwanza mara nyingi kinachotushika machoni ni uzuri wa nje (maumbilie, sauti, macho n.k). Hivyo, mwanamme mwenye akili timamu hawezi kumchukua binti ambaye ana umri wa balehe ambaye akikaa na mke wake watu wanamuangalia yeye na si mkewe! Na yeye mwenyewe anamuangalia huyo kuliko mkewe.

I'm dead serious on this. Usimletee mke wako mashindano ya attention. I have been there.

2.Hawa wasichana siyo wajinga kama watu wanavyodhania. Mke na mume kwa vyovyote lazima wanaweza kuwa na mapungufu yao, na msichana huyu anasoma mchezo wote unavyokwenda na ata capitalise on the weaknesses za mke...... sasa ukisema usiajiri aliye mwema kuliko mkeo mhhhh!!??

Maandiko yanasema mke mwema hutoka kwa bwana haisemi hausigeli mwema! Hausigeli wako akiwa mwema kuliko mkeo muoe!

3.Bold 3, Huu ni mtihani.Kulala ndani na kuwa na sifa a u b.... hizi ndizo sifa ambazo humfanya hausigel aajiriwe! In short bold 1,2,3 huwa ni vigezo vya kumwajiri msichana.Hakuna mtu ataajiri msichana mkatili, asiyekuwa na sifa zozote aje amlelee watoto!u hausgel ni kazi jamani lazima iwe na vigezo.

To tell you the truth watu wengi wanaajiri wasaidizi wa ndani kwa ajili ya kile kinachoitwa "kazi za ndani" mambo ya kupiga deki, kusafisha vyombo, kufua n.k Haya mambo baba na mama mwenye nyumba wanaweza kuyafanya pasipo kuonekana kituko.

Leo hii kila mtu akifanikiwa kidogo tu anataka kuwa na msaidizi wa ndani! Hii ni mentality ya kikoloni! Watu wanatakiwa kuwa na msaidizi wa ndani pale ambapo wao wenyewe kwa namna fulani hawawezi mambo fulani hasa kusimamia watoto wadogo wakati wao wenye nyumba wanaenda kazini. Wenye nyumba wakirudi msaidizi anatakiwa aende zake kwake.

kwanza siamini katika kumuajiri mtu kwa masaa 24! kwa kisingizio cha kumpa pa kula na pa kulala. Kama kweli watu wanaamini hivyo wawapangie hao wasaidizi wao vyumba vyao.

Hili ni muhimu kwa sababu, wakati tunafikiria mahitaji ya mume na mke ya ngono tunaignore mahitaji ya ngono ya hao wasaidizi. Mnataka akae humo ndani kama mtawa wakati kuna mwanamme!?

4. Bold 4 ...hii nadhani ndio hasa chanzo cha tatizo - wanaume wengi wakware hujaribu kumvua mwanamke yeyote kwa mawazo/fikra na si ajabu kufanya hivi kwa hausigeli.

Hii si sababu ya ukware wala nini; mwanamme/mwanamke ni mwaminifu kwa kadiri ya chaguo lililo mbele yake. A man or a woman is as faithful as the options available to him/her.
 
Ni lazima ufuate kanuni:

a. Usiajiri msaidizi wa ndani wa kike ambaye ni mzuri kuliko mke wako
b. Usiajiri msaidizi wa ndani ambaye ni mwema kuliko mkeo
c. Usiajiri msaidizi wa ndani ambaye analala ndani ya nyumba yako na anasifa a na b
d. Usiajiri msaidizi wa ndani ambaye ukimwangalia unafikiria kilicho chini ya nguo zake
e. Kama wewe ni mwanamke/mke usimuache mumeo akubali kuajiri msaididi mwenye sifa hizo. Mtashindana na utashindwa.

mbona mara nyingi wakina mama ndio wanachagua hao ma-hg?
 
Ni lazima ufuate kanuni:

a. Usiajiri msaidizi wa ndani wa kike ambaye ni mzuri kuliko mke wako
b. Usiajiri msaidizi wa ndani ambaye ni mwema kuliko mkeo
c. Usiajiri msaidizi wa ndani ambaye analala ndani ya nyumba yako na anasifa a na b
d. Usiajiri msaidizi wa ndani ambaye ukimwangalia unafikiria kilicho chini ya nguo zake
e. Kama wewe ni mwanamke/mke usimuache mumeo akubali kuajiri msaididi mwenye sifa hizo. Mtashindana na utashindwa.

.........Hebu nipe kanuni za kufuata ili nipate house boy, nina mpango wa kutafuta house boy mie.
 
Yeah hili suala ni la kweli kabisa na hili si la waume za watu tu bali hata vijana wa kiume wengi kwa kiasi kikubwa hufanya mchezo huo kwa wajakazi hao mara nyingi na mifano iko dhahiri, wengi tushapitia hizi hali na kwa hakika ni makovu yasofutika fikrani mwetu! Tuache haraka na tusofanya tusijaribu!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom