Wanaume na wanawake: Hakuna maendeleo yatakayoletwa na kundi moja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume na wanawake: Hakuna maendeleo yatakayoletwa na kundi moja

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Kaunga, May 28, 2011.

 1. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Tunajua kuwa duniani kuna wanawake na wanaume!
  Hakuna maendeleo yanayoletwa na kundi moja!
  Na kudharau kundi moja ni kupunguza kasi ya maendeleo!

  Sasa, hapa2 home of great thinker kauli kama hizi zinatumika; na some wanaume na wanawake au twazitumia ama kuzikubali!
  1: Wanaume kama mabinti! (huyo ni mwanaume aliyedharaulika sana; does it mean women r less human?)
  2: Mwanamke yule bwana ni dume yule! (huyu ni mwanamke, mwenye akili; aliyefanikiwa na jasiri; does it mean women are supposed to be only dumb n beautiful?
  3: Mwanamke ni ua/pambo la nyumba! (sijui wanamaanisha a piece of furniture)

  Jamani tubadilike; sidhani kama wengi wetu tunaomrefer mwanamke hivyo tunafikiria mama zetu as reference; more often ni binti fulani (ambaye atakuwa mama wa mwanaume fulani) au mke ambaye tunam-maltreat sana!

  Nasisi baadhi ya wanawake; tujue kuwa we are better than hii patriachy society inavyotaka tuwe!
   
 2. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa hapa tujadili nini na kila kitu umeuliza na kujibu mwenyewe?

  Hebu edit hii thread yako halafu utuwekee wazi tujadili nini.

  Huoni kuwa ndio maana haijapata mchangiaji?

  Samahani sana Mkuu.
   
 3. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Nimetoa mchango wangu; ambao si lazima uwe ndio final!
  Tujadili Maswali niliyouliza kwenye mabano!
  1: wanawake sio binadamu kamili? Kwani mwanaume kuwa kama binti ni tusi!
  2: wanawake wanapaswa kuwa warembo tu! Kwani akiwa na akili; maendeleo anapanfishwa cheo na kwa 'dume'
  3: wanawake wanapaswa kuwa samani za nyumba kwani ni 'ua/pambo' la nyumba!
   
 4. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Nimeona crap topics zimechangiwa hapa! Hii wanaivisit but they don't DARE to changia coz ni sensitive sana na mfumo dume umetuathiri sana both men n women na both elites na non elites!

  I did expect that!

  Na sio jinsi nilivyoweka thread!
   
 5. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi sijaona sababu ya msingi ya wewe kuwatetea wanawake. Hizo sifa zote unazoona kuwa ni mbaya dhidi ya wanawake ni sifa zao halali toka enzi na enzi. Tatizo kubwa na utawazi na haki sawa kwa wote ambazo kibiblia na kikuran hazitambuliwi. Hata kwenye Biblia au hata kwenye Koran ni kweli kuwa wanawake ndivyo walivyoumbwa na kupewa sifa hizo.
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  May 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nikweli kabisa kwamba hii hoja ni very sensitive na inahitaji sana umakini wakati mtu anatoa jibu kwa sababu wewe mwenyewe tayari umeshatoa conclusion jinsi unavyotafsiri misemo au matumizi ya baadhi ya maneno.

  Kusema kweli wanawake wanapewa sifa kubwa sana za uzuri na urembo kuliko wanaume na ktk uzuri na urembo huo ipo mienendo inayomtafsiri mwanamke kama mwanamke ki****, na muhimu sana kwanza sisi sote tukubali kuwepo na tofauti baina ya mwanamme na mwanamke kimaumbile na hata ktk mienendo.

  Hivyo, misemo mingi hutokana na mmoja baina yetu kujishabihisha na jinsia nyingine. Haina maana kuna mapungufu ktk jinsia hiyo isipookuwa mhusika anapojishabihisha na jinsia nyinge ndipo swala hili linapochukua sura mpya yaani anayetazamwa ni mtu mhusika na sio jinsia nzima.

  Kwa mfano mwanamme anapokubali ushoga, kuvaa kama mwanamke - husemwa heee mwanamme kama Binti..lakini pia mwanamme anayependa udaku na kushinda jikoni na wanawake huitwa vile vile mwanamme kama binti. sasa wapo wanawake wanaohoji hizi habari za udaku na kushinda jikoni kama tusi kwa wanawake...Hii inatokana na malezi ya mtu kwani ktk mila na desturi za kiafrika sifa ya kwanza ya mwanamke ni jiko. Wenyewe husema mwanamke JIKO kwa maana kwamba uzuri wa mwanamke huanza na mapishi ingawa the best chef in the world ni wanaume lakini kila mmoja wetu including hao best chef husema - Chakula kitamu lakini sii kama cha mama yangu..Hivyo, hii ni sifa kubwa sana kwa wanawake ikiongozwa na mama zetu.

  Na tukizungumzia Udaku kuwa ni jambo la kike mara nyingi sana neno hili limetumika kwa sababu mwanamme unatakiwa ku face matatizo kwa vitendo, habari yeyote inayokutatiza hutakiwi kubaki nayo rohoni bali kuifanyia kazi na pengine kuna ukweli kwamba wanawake hupenda au ndio hulka yao kuzungumzia kero au swala linalowatatiza ili kupoza hasira na kuondoa machungu yao badala ya kuchukua hatua haraka.

  Na mara nyingi wanawake huchukua muda sana kupitisha maamuzi ya action zao hivyo huwa kama wanapika balaa linalokuja, wanawake wana subira zaidi na wakifikia maamuzi hayo huwa balaa haswa!
  Na hata ktk ndoa utakuta kwamba wanawake hupenda sana kuzungumza na mabwana zao kero au matatizo ya kifamilia kuliko wanaume, lakini hawapewi muda wa mazungumzo kama wanavyotarajia kwa sababu wanaume kihulka hawapendi kuchukua muda kuzungumzia kero bali hutaka hitimisho na kulifanyia kazi.

  Tofauti ya tabia hizi ndio huvunja ndoa za watu kutokana na kwamba wanawake hujiona hawapewi muda hivyo kuonyesha kwamba mwanamme hamjali yaani hampi enough attention. Again Udaku kwa maana halisi sio tusi isipokuwa ni habari (media forum) inayochukua muda kuzungumzia kero au swala ambalo linahitaji action kama vile hapa JF hakika tupo jikoni tukipika udaku kuhabarishana, hivyo sijui kama ni sifa au dharau.

  Na mwisho naweza sema hata ukisikia mtu akisema mwanamke yule dume, mimi nadhani inatokana na mila na desturi zetu kwamba zipo sifa zinazomstahili mwanamke na sio mwanamme kuvaa khanga au kilemba tukasema kapendeza, hapana tutakuwa tunajidanganya. Mwanamke dume mara nyingi hutokana na mwanamke kutopenda kujiweka kike, mwanamke anayejishabihisha na mwanamme kiasi kwamba amevukiuka mila na desturi zetu. na katika hizo mila na desturi zipo mbaya na nzuri, zipo zilizopitwa na wakati na zipo zinapendeza kuzienzi kwa kujivunia na kupenda maumbile yetu...

  Mara nyingi jiepushe sana na inferiority complex hasa ktk maswala ya kijinsia..Usikubali kushushwa na mara zote jifijirie kama mwanamke na kukubali majukumu yako kama mwanamke kwani Mungu hakutuumba tofauti ubaya ila kwa sifa za maumbile haya kukimu vizuri zaidi baadhi ya mahitaji yetu na katika maajabu ya Mungu - There are so many things Woman can do man can't..
   
 7. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Mkandala!
  Nashukuru kwa mchango wako ulio very informative! Na nakupongeza kudare kuongelea hii sensitive issue!

  Nimeshaambiwa kauli ambazo wengine wangeona ni sifa; lakini mimi kuna part inanikera sana! Naomba usitafsiri kama infiriority complex! Some of those kauli ni:-

  1: hivi hiyo nyumba ni ya mwanamke kweli?
  2: my dear you r a woman and ahalf!

  Issue yangu sio sifa; lkn how mwanamke anavyokuwa expected kuwa!
  Unaweza kutake lightly lkn; sijui wewe umesoma wapi? But mimi nikiwa O'level in coedu school back in early 1990s kuna baadhi ya wasichana walizembea masomo kwa kuwa kuna wavulana wanawasomea!

  Dhana kama hizo zimetengenezwa na jamii; nina uhakika mabinti hao wangeweka bidii kidogo; wangekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi yetu!
   
Loading...